093-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Al-Wiswaal katika Funga, Nayo ni kwa Mtu Kufunga Siku Mbili au Zaidi Wala Hali Chakula wala Hanywi Chochote Baina Yake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تحريم الوصال في الصوم

وَهُوَ أنْ يصوم يَومَينِ أَوْ أكثر وَلاَ يأكل وَلاَ يشرب بينهما

093-Mlango Wa Uharamu wa Al-Wiswaal katika Funga, Nayo ni kwa Mtu Kufunga Siku Mbili au Zaidi Wala Hali Chakula wala Hanywi Chochote Baina Yake

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة وعائشة رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم نهى عن الوِصَالِ .متفق عَلَيْهِ.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah na 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza funga ya Al-Aiswaal (kuunganisha). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : نَهَى رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم عَنِ الوِصَالِ . قالوا : إنَّكَ تُواصِلُ ؟ قَالَ : (( إنِّي لَسْتُ مِثْلَكُمْ ، إنِّي أُطْعَمُ وَأُسْقَى )) . متفق عَلَيْهِ . وهذا لفظ البخاري .

Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza Al-Wiswaal Akaulizwa: "Mbona wewe unaunganisha?" Akajibu: "Hakika mimi si kama nyinyi, ninalishwa na kunyweshwa (yaani na Allaah)." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy]

 

 

Share