109-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uzito wa Uharamu wa Uchawi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب التغليظ في تحريم السحر

109-Mlango Wa Uzito wa Uharamu wa Uchawi

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ  ﴿١٠٢﴾

Na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru, wanafundisha watu sihiri [Al-Baqarah: 102]

 

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ )) . قالوا : يَا رسولَ اللهِ ، وَمَا هُنَّ ؟ قَالَ : (( الشِّرْكُ باللهِ ، وَالسِّحْرُ ، وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتي حَرَّمَ اللهُ إِلاَّ بِالحَقِّ ، وأكْلُ الرِّبَا ، وأكْلُ مَالِ اليَتِيمِ ، وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ ؛ وَقَذْفُ المُحْصَنَاتِ المُؤْمِنَاتِ الغَافِلاَتِ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jiepusheni na madhambi saba yanayoangamiza." Watu wakauliza: "Ee Rasuli wa Allaah ni yapo hayo?" Akasema: "Kumshirikisha Allaah, na uchawi, na kuua nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na kula riba, kula mali ya yatima, kukimbia siku ya vita na kuwatuhumu kwa zinaa wanawake waliohifadhiwa na Allaah, Waumini wasiyo na habari ya zinaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share