112-Al-Ikhlaasw: Utangulizi Wa Suwrah
112-Al-Ikhlaasw: Utangulizi Wa Suwrah
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 4
Jina La Suwrah: Al-Ikhlaasw
Suwrah imeitwa Al-Ikhlaasw (Ikhlasi), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila na kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) kwa ibaada na ukamilifu, na Kumtakasa kutokana kuzaa au kuwa na mwana, na kufanana na yeyote. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba Yeye Ni Mkusudiwa wa kila kitu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imethibitisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Yeye Ni Mmoja Pekee, Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki. Naye Ndiye Asw-Swamad; Mweza na Mkusudiwa Pekee wa kukidhi haja za waja. Wala Hana Mwana wala mzazi wala mke; Ametakasika na kuhitaji hayo. Wala hakuna yeyote katika viumbe Vyake (سبحانه وتعالى) mwenye kufanana wala kushabihiyana na Yeye katika Majina Yake, Sifa Zake wala Vitendo Vyake.
Fadhila Za Suwrah:
Suwrah hii ina fadhila nyingi mno. Miongoni mwa fadhila zake ni:
1-Sunnah Kuisoma Katika Swalaah Za Sunnah Kama Sunnah Ya Alfajiri na Magharibi, Swalaah Ya Witr, Swalaah Katika Maqaam Ibraahiym Baada Ya Twawaaf: Rejea Suwrah Al-Kaafiruwn (109) kulikotajwa fadhila hizi.
2- Thawabu Za Kuisoma Ni Kama Thawabu Za Kusoma Thuluthi Ya Qur-aan:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ أَنَّ رَجُلًا سَمِعَ رَجُلًا يَقْرَأُ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ يُرَدِّدُهَا، فَلَمَّا أَصْبَحَ جَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ ، وَكَأَنَّ الرَّجُلَ يَتَقَالُّهَا أي يراها قليلة فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّهَا لَتَعْدِلُ ثُلُثَ الْقُرْآن))
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Mtu mmoja alimsikia mtu akisoma
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
na akiikariri. Asubuhi yake akamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamtajia hilo na alidhania kuwa ni kisomo kidogo tu. Lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hiyo ni sawa na thuluthi ya Qur-aan.” [Al-Bukhaariy]
na pia:
عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَقْرَأَ فِي لَيْلَةٍ ثُلُثَ الْقُرْآنِ " قَالُوا : وَكَيْفَ يَقْرَأْ ثُلُثَ الْقُرْآنِ ؟ قَالَ : " قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ تَعْدِلُ ثُلُثَ الْقُرْآنِ "
Amesimulia Abuu Ad-Dardaa (رضي الله عنه) : Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
“Kuna yeyote kati yenu anayeishindwa kusoma thuluthi ya Qur-aan usiku?” Swahaba wakauliza: Vipi mtu aweze kusoma thuluthi ya Qur-aan? Akasema:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
Ni sawa na thuluthi ya Qur-aan. [Al-Bukhaariy na Muslim]
3-Kuisoma Katika Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni Na Adhkaar Za Kulala Kumkinga Mtu Na Kila Shari.
عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ.
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoingia kitandani kila usiku, alikuwa akikusanya vitanga vyake vya mikono na kupuliza juu yake baada ya kusoma:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾
Kisha akipangusa kwa mikono yake sehemu za mwili wake ambazo alikuwa anaweza kuzipangusa, akianza na kichwa chake, uso wake na sehemu yake ya mbele ya mwili. Alikuwa akifanya hivyo mara tatu. [Al-Bukhaariy]
Na pia
عَنْ مُعَاذِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ خُبَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّهُ قَالَ خَرَجْنَا فِي لَيْلَةِ مَطَرٍ وَظُلْمَةٍ شَدِيدَةٍ نَطْلُبُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لِيُصَلِّيَ لَنَا فَأَدْرَكْنَاهُ فَقَالَ " أَصَلَّيْتُمْ " . فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا فَقَالَ " قُلْ " . فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا ثُمَّ قَالَ " قُلْ " . فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا ثُمَّ قَالَ " قُلْ " . فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ مَا أَقُولُ قَالَ " قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ حِينَ تُمْسِي وَحِينَ تُصْبِحُ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ تَكْفِيكَ مِنْ كُلِّ شَىْءٍ " .
Amesimulia Mu’aadh Bin ‘Abdillaah Bin Khubayb kutoka kwa baba yake (رضي الله عنهما): Tulitoka usiku mmoja wenye mvua nyingi na giza kilotanda, kwenda kumtafuta Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ili atuongoze katika Swalaah. Tulipomkuta aliuliza: “Je, mmeswali?” Lakini mimi sikusema chochote. Akasema: “Sema.” Lakini mimi sikusema chochote. Akasema tena: “Sema.” Lakini mimi sikusema lolote. Kisha akasema: “Sema.” Basi nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, niseme nini? Akasema:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
Na Al-Mu’awwidhatayni, mara tatu asubuhi na jioni, zitakutosheleza na kila kitu. [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3575), Swahiyh Abiy Daawuwd (5082)]
Al-Mu’awwidhatayni ni Suwrah Al-Falaq (113) na An-Naas (114).
4-Kupenda Kuisoma Ni Sabababu Mojawapo Ya Kupata Mapenzi Ya Allaah:
عَنْ عَائِشَةَ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم بَعَثَ رَجُلاً عَلَى سَرِيَّةٍ، وَكَانَ يَقْرَأُ لأَصْحَابِهِ فِي صَلاَتِهِ فَيَخْتِمُ بِ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ فَلَمَّا رَجَعُوا ذَكَرُوا ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " سَلُوهُ لأَىِّ شَىْءٍ يَصْنَعُ ذَلِكَ ". فَسَأَلُوهُ فَقَالَ لأَنَّهَا صِفَةُ الرَّحْمَنِ، وَأَنَا أُحِبُّ أَنْ أَقْرَأَ بِهَا. فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " أَخْبِرُوهُ أَنَّ اللَّهَ يُحِبُّهُ "
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alituma kikosi cha jeshi chini ya uongozi wa mtu aliyekuwa akiwaongoza Swahaba zake katika Swalaah. Akawa katika Swalaah zake zote alizokuwa akiswalisha wenzake, akikhitimisha kwa kusoma:
قُل هُوَ الله أَحَدٌ
Waliporudi (Madiynah), Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitajiwa hilo, naye akawaambia: "Muulizeni ni kwa sababu gani anafanya hivyo?" Wakamuuliza, naye akasema: Kwa sababu humo ndani zipo Sifa za Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), nami napenda kuzisoma. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Mpeni khabari kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anampenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]
5-Kuisoma Katika Duaa Ni Sababu Ya Kutaqabaliwa Duaa:
عن عَبْدِ اللَّهِ بن بُرَيْدَةَ الأسْلَمِيِّ عن أبِيهِ (رضي الله عنهما) قال: سَمِعَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) رَجُلاً يَدْعُو وَهُوَ يَقُولُ: "اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أحَدٌ" فقال: ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَدْ سَألَ اللَّهَ بِاسْمِهِ الأعْظَمِ الَّذِي إذَا دُعِيَ بِهِ أجَابَ وَإذَا سُئِلَ بِهِ أعْطَى))
Amesimulia ‘Abdullaah bin Buraydah Al-Aslamiyy, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimsikia mtu akiomba:
"اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أحَدٌ"
Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa kushuhudia kwamba hakika Wewe ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Mmoja Pekee, Aliyekamilika Sifa za Utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote, Ambaye Hakuzaa wala Hakuzaliwa, na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, amemuomba Allaah kwa Jina Lake Adhimu kabisa Ambalo Anapoombwa kwalo (duaa) Anaitikia na Anapotakwa kwalo (jambo) Hutoa)) [Swahiyh Ibn Maajah (3125) Swahiyh At-Tirmidhy (3475), Swahiyh Abi Daawuwd (1493), Swahiyh At-Targhiyb (1640)]
6-Kupenda Kuisoma Ni Sababu Ya Kuingizwa Jannah:
Rejea Hadiyth Za Al-Bukhaariy Namba (774B) katika Mlango Wa Kusoma Suwrah Mbili Katika Rakaa Moja Katika
7-Ni Sunnah Kuisoma Kila Baada Ya Kumaliza Swalaah Za Fardhi Pamoja Na Al-Mu’awwidhatayni [Suwrah Al-Falaq (113) na An-Naas (114)]