34-Malaika: Malaika Wana Sifa Ya Kuona Haya

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

34:  Malaika Wana Sifa Ya Kuona Haya

 

Malaika wana hisia ya kuona haya.  Hadiyth hii ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) inathibitisha: 

 

"أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ جَالِسًا كَاشِفًا عَنْ فَخِذِهِ ، فَاسْتَأْذَنَ أَبُو بَكْرٍ فَأَذِنَ لَهُ وَهُوَ عَلَى حَالِهِ ، ثُمَّ اسْتَأْذَنَ عُمَرُفَأَذِنَ لَهُ وَهُوَ عَلَى حَالِهِ ،‏ ثُمَّ اسْتَأْذَنَ عُثْمَانُ فَجَلَسَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَسَوَّى ثِيَابَهُ ، فَلَمَّا خَرَجَ ‏ قُلْتُ‏:‏ يَا رَسُولَ اللهِ، دَخَلَ أَبُو بَكْرٍ فَلَمْ تَهَشَّ وَلَمْ تُبَالِهِ، ثُمَّ دَخَلَ عُمَرُ فَلَمْ تَهَشَّ وَلَمْ تُبَالِهِ، ثُمَّ دَخَلَ عُثْمَانُ فَجَلَسْتَ وَسَوَّيْتَ ثِيَابَكَ‏؟‏ قَالَ‏:‏ أَلاَ أَسْتَحِي مِنْ رَجُلٍ تَسْتَحِي مِنْهُ الْمَلاَئِكَةُ‏؟"

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ameketi huku akiwa amelifunua paja lake.   Abu Bakr akapiga hodi, akamruhusu kuingia akiwa hivyo hivyo (akazungumza naye halafu akatoka).  Kisha ‘Umar naye akapiga hodi, akamruhusu kuingia akiwa hivyo hivyo (akazungumza naye kisha akatoka).  Halafu ‘Uthmaan akapiga hodi, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaketi sawa, akaiweka vizuri nguo yake. Alipoondoka nilimuuliza:  Ee Rasuli wa Allaah!   Abu Bakr ameingia, ukabaki ulivyokuwa wala hukujali, kisha ‘Umar akaingia, ukabaki hivyo hivyo, lakini ‘Uthmaan alipoingia, uliketi sawa na kuiweka vizuri nguo yako.  Akasema:  “Iwaje nisimwonee haya mtu ambaye Malaika wanamwonea haya?!”   [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2401)].

 

 

Share