37-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Hakika Allaah Kaandika Hasanaat Na Maovu

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 37

 

إِنَّ الله كَتَبَ الحَسَنَاتِ وَالسَّيئَاتِ

 

Hakika Allaah Kaandika Hasanaat Na Maovu

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

'

 

 

عَن ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا عَنِ النبي صلى الله عليه وسلم فِيْمَا يَرْوِيْهِ عَنْ رَبِّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالى أَنَّهُ قَالَ: (إِنَّ الله كَتَبَ الحَسَنَاتِ وَالسَّيئَاتِ ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ؛ فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِمائَةِ ضِعْفٍ إِلىَ أَضْعَاف كَثِيْرَةٍ. وَإِنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً،وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً)) رَوَاهُ البُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ في صَحِيْحَيْهِمَا بِهَذِهِ الحُرُوْفِ

 

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kutokana na yale aliyoyapokea kwa Rabb wake Tabaaraka Wa Ta’aalaa kwamba amesema: “Hakika Allaah Ameandika hasanaat (mazuri) na maovu kisha Akayabainisha. Basi atakayetilia hima kufanya hasanah (zuri) moja, kisha asiweze kuifanya, basi Allaah Atamwandikia (thawabu za) hasanah moja kamilifu. Na ikiwa ametilia hima kuifanya kisha akaifanya, basi Allaah Atamwandikia hasanaat kumi hadi mara mia saba maradufu zaidi ya hayo. Na akitilia hima kufanya ovu moja kisha asifanye, basi Allaah Atamuandikia hasanah moja kamilifu. Na ikiwa akitilia hima akalifanya, basi Allaah Atamuandikia ovu moja.” [Al-Bukhaariy na Muslim kwa matamshi hayo]

 

 

 

 

Share