Ardhi Iliyosahaulika

 

Ardhi Iliyosahaulika

 

Muhammad Al-Ma'awy

 

Alhidaaya.com

 

Utangulizi

 

Ardhi hii iliyosahaulika ilikuwa na migongano mingi sana baina ya staarabu tofauti, baina ya Uislamu na Ukafiri, baina ya haki na batili na baina ya Tawhiyd na Shirki. Migongano hii ilikuwa ya kutumia silaha au baridi kwa kuelezea, kujadiliana na kulingania. Mgongano wa mwisho ni ule ulioletwa na maandishi ya Mkataba wa Sykes – Picot ulioandikwa 1916 baina ya Uingereza na Ufaransa.Ardhi hii inatajwa ana lakini haipo kwenye ramani na imesahaulika sana na hususan sisi Waislamu. Allaah, Nabiy Wake na historia imetupatia sifa tofauti ya ardhi hii. Sifa hizi zimefanya kila taifa kuigombea.

 

Itikadi Ya Muislamu Juu Ya Ardhi Hii

 

1.     Ardhi Tukufu:

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

يَا قَوْمِ ادْخُلُوا الْأَرْضَ الْمُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَرْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ ﴿٢١﴾

Enyi kaumu yangu! Ingieni ardhi iliyotakaswa ambayo Amekuandikieni Allaah kwenu, na wala msirudi kugeuka nyuma kukimbia (kupigana) hapo mtageuka kuwa wenye kukhasirika. 

 [Al-Maaidah:21]

 

Je, hii aya imewapatia Mayahudi urithi wa moja kwa moja kwenye ardhi ya Palestina? Je, huu ni urithi wa majukumu au wa dam?

Allaah Anasema yafuatayo kuhusu Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam):

 

وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾

Na pindi Alipojaribiwa Ibraahiym na Rabb wake kwa amri nyingi, naye akazitimiza. Akasema: Hakika Mimi Nakufanya uwe Imaam kwa watu. (Ibraahiym) Akasema: Na katika kizazi changu? (Allaah) Akasema: Haiwafikii ahadi Yangu madhalimu. [Al-Baqarah:124]

 

Kuna dhulma gani kuliko ya Mayahudi kuwafanyia ndugu zetu Palestina. Hususan angazia yaliyotokea kuanzia tarehe 29 Machi 2002 mpaka wakati wetu huu wa sasa.

 

2.     Ardhi Iliyobarikiwa:

 

Ardhi hii imebarikiwa kiroho na kirutba. Ni jambo hili ndilo lililowafanya watu na staarabu tofauti kuigombania. Agano la Kale inatuhadithia ya kuwa ardhi hii ilibubujika asali na maziwa. (Hesabu, 13:27) Na katika kitabu cha Hesabu Sura ya 13 inatueleza kuwa majasusi wa Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) walipata humo matunda ya makudhumani, tini na zaituni ambayo yalikuwa makubwa na kila tunda kubebwa na watu wawili. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ ... ﴿١﴾

"...mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake;...."

[Al-Israa:1].

 

Lakini ardhi yote ya Palestina imebarikiwa. Allaah Anasema:

 

وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾

Na Tukamuokoa na Luutw kuelekea ardhi ambayo Tumeibariki humo kwa walimwengu.[Al-Anbiyaa: 71]

 

3.     Ardhi ya Rusuli:

 

Katika ardhi hii Mitume tofauti ima walihamia au walizaliwa na kuishi utotoni mwao au walifanya Da’wah na kuzikwa katika sehemu hii au walizuru japokuwa kwa muda mfupi. Miongoni mwao ni Manabii kama Ibraahiym, Ismaa’iyl, Is-haaq, Ya’quub, Luut, Daawuud, Sulaymaan, Zakariyyaa, Yahyaa, ‘Iysaa na Muhammad.

 

4.     Ardhi ya Wahyi:

 

Wahyi ndio uliokuwa na mpaka sasa unajenga ustaarabu na utamaduni za watu tofauti. Miongoni mwa Vitabu vilivyoteremshwa kutoka kwa Allaah katika ardhi hii ni Suhuf za Nabiy Ibraahiym, Zaburi ya Nabii Daawuud, Injiyl ya Nabiy ‘Iysa na pia baadhi ya aya katika Suwrah Al- Zukhruf katika Qur-aan.

 

5.     Ardhi ya Israa Wal Mi’iraaj:

 

Hii ni safari ya usiku aliyopelekwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Israa ni safari ya kutoka Msikiti Mtukufu wa Makkah mpaka Baytul Maqdis. Mi’iraaj ni ngazi ya kutoka Baytul Maqdis mpaka wingu wa saba. Natija mzuri kabisa ya safari hii ni kufaridhiwa Ummah huu Swalaah tano, mchana na usiku. Swalaah ya kwanza ya jama’a h ilifanyika katika Msikiti Mtukufu wa ‘Aqswaaa ambapo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwasalisha Rusuli wote (‘Alayhim-salaam). hii inatukumbusha kila tunaposwali mahusiano yetu ya karibu sana na ardhi hii.

 

6.     Ardhi ya Msikiti wa ‘Aqswaa:

 

Msikiti huu ulikuwa kibla cha kwanza kwa Waislamu. Kwa miezi 16 au 18 baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake kuhamia Madiynah walikuwa wakielekeza nyuso zao kwa upande wa Baytul Maqdis mpaka Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Alipokibadilisha kwa kuteremsha aya ya 144 na 150 ya Suwrah Al-Baqarah. Msikiti huu ni wa tatu kwa utukufu baada ya Msikiti Mtukufu wa Makkah na Msikiti wa Nabiy Muhammad Madiynah. Swalaah moja katika Msikiti huu ina thawabu mara 500 kuliko Misikiti mingine ila Msikiti wa Makkah na Madiynah. (At-Twabaraaniy)

Kwa hivyo kila Muislamu ulimwenguni ana hamu sana ya kwenda kuuzuru na kuswali ndani yake. Lakini je, tunaujua Msikiti huu ni upi? Wengi wetu tunaujua ule Msikiti ambao unachapishwa katika magazeti na majarida, kuonyeshwa katika televisheni, kuwepo kwenye makalenda, picha zinazotundikwa majumbani, n.k. Huu Msikiti ninaouzungumzia una sifa ya kipekee na unajulikana kwa kuwa na Qubba rangi ya njano au ya dhahabu. Lakini ndugu zangu wapendwa, Masjidul ‘Aqswaa ni eneo lote ambalo lipo katika kuta nne ikiwemo Masjid Qubbatus Swakhraa (Msikiti wa Qubba ya Jabali au Dome of the Rock), Masjidul ‘Aqswaa (huu ulijengwa baada ya ule wa Qubbatus Swakhraa), Masjid Marwani, miti ambayo imo ndani, shule na kuta zenyewe. Sehemu hii yote ni tukufu na ndio Msikiti wa ‘Aqswaa bila ya tofauti yoyote baina ya wanavyuoni wote wa Kiislamu.

 

7.     Ardhi ya Maswahaba:

 

Swahaba watukufu waliipigania ardhi hii na kuweza baada ya taufiki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kuitawala. Swahaba 200 walioshiriki katika Vita vya Badr walikuwa katika msitari wa mbele wa kuuteka mji wa al-Quds. Takribani makaburi 18,000 ya Swahaba yanapatikana katika ardhi hii.

 

8.     Ardhi ya Jihadi, Ribati na Vita vya Mwisho:

 

Vita vitagavyopiganwa baina ya Waislamu upande mmoja na Mayahudi upande mwengine. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatueleza:

"Qiyaama hakitofika mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi. Mayahudi watakuwa wanauliwa na kuwafanya wajifiche nyuma ya miti na mawe ambayo itasema: ‘Ee Muislamu! Ee mja wa Allaah! Njoo nyuma yangu yupo Yahudi umuue …" [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hitimisho

Ndugu zetu wanauliwa kila saa na dakika. Je, tufanyeje ili kuwasaidia ndugu zetu katika ardhi hii yetu?

1.     Tumjue Allaah vilivyo na tuongeze Iymaan yetu kwa kufuata mafundisho ya Uislamu na kuacha makatazo yake. Tujipinde na 'Ibaadah.

 

2.     Tuanze kususia bidhaa za Israeli na Marekani ambaye ni rafiki yake wa chanda na pete na wa hali na mali. Kwa mfano tusinunue soda za kampuni ya coca-cola na pepsi cola, rangi ya kiwi na bidhaa nyenginezo. Kampuni za coca-cola na pepsi zinamsaidia vilivyo Israeli, pamoja na maduka ya Sainsbury, Debenham, Marks & Spenser na kula kwenye kwenye migahawa ya McDonald, Kentucky na zingine nyingi ambazo ni nyingi sana kuziorodhesha hapa.

 

3.     Tusiwasahau ndugu zetu katika Du’aa hata baada ya kujiombea nafsi zetu hususan tunapokuwa katika sijdah, tunaposafiri, tunapofunga, tunapoinuka usiku kwa Swalaah ya Tahajjud, n.k.

 

Kumbukeni Ni Jihadi Pekee Inayoweza Kuikomboa Ardhi Hii 

 

 

Share