08-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuharamishwa Liwati

 

 

Imekatazwa mwanamume kumuingilia mkewe kwa nyuma. Hii inafahamika kutokana na Aayah iliyotajwa hapo juu (kwa vile 'konde zenu' inakusuduwa ni sehemu inayotoa mazao tu). Na kutokana na usimulizi ulioelezewa hapo juu. Vile vile kuna Hadiyth nyingine kuhusu maudhui kama zifuatazo:

 
Kwanza:

 

عن أم سلمة قالت: لما قدم المهاجرون المدينة على الأنصار تزوّجوا من نسائهم، وكان المهاجرون يجبون وكانت الأنصار لا تجبي، فأراد رجل من المهاجرين امرأته على ذلك، فأبت عليه حتى تسأل رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالت: فأتته فاستحيت أن تسأله، فسألته أم سلمة فنزلت ((نساؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنّى شِئْتُم)) وقال: «لا إلاّ في صَمَّامٍ واحِدٍ»  

Imetoka kwa Ummu Salamah رضي الله عنها kwamba: Muhaajiriyn walipokuja Madiynah kwa Ma-Answaar waliwaoa wanawake wao. Wanawake wa Muhaajiriyn walikuwa wakilala kifudifudi (wakati wa kujimai na waume zao) na wanawake Ma-Answaar hawakuwa wakifanya hivyo. Mwanamume mmoja Muhaajir alitaka mkewe afanye hivyo akakataa. Akaenda kwa Mtume lakini aliona hayaa kumuuliza swali hilo, kwa hiyo Ummu Salamah alimuulizia kisha Aayah ikateremshwa inayosema: ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo)). Mtume akasema: ((Hapana! (Sio kila njia upendayo) bali isipokuwa ni pale penye tundu)) (la mbele) [1]

 
 

Pili:

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال:  جاء عُمَر بن الخطاب إلىٰ رسول الله فقال: يا رسول الله، هلكتُ! قال: ((وما الذي أهلكك؟)) قال: حَوَّلْتُ رَحْلِي الليلة، فلم يردَّ عليه شيئاً، فأُوْحِيَ إلىٰ رسول الله هذه الآيةُ:  ((نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنىٰ شئتم)) يقول: ((أَقْبِلْ، وأَدْبِرْ، واتقي: الدُّبر، والحَيضة))

Imetoka kwa Ibn 'Abbaas رضي الله عنهما ambaye amesema: Alikuja 'Umar ibnul-Khatwtwaab kwa Mjumbe wa Allaah akasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, Nimeangamia! Akasema: ((Nini kilichokuangamiza?)) Akasema: Nimepindua kipando changu usiku. Lakini (Mtume) hakumjibu kitu.

Akateremshiwa Aayah hii ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo)) Akasema: ((Kwa (mtindo) wa mbele, nyuma lakini chunga kumuingilia (sehemu ya maumbile ya nyuma) na akiwa katika hedhi))[2]

 
 

Tatu:

عن خُزَيْمَةَ بنِ ثابتٍ أَنَّ رجلاً سَأَلَ النبيَّ عن إتيانِ النساءِ في أَدْبَارِهِنَّ أو إتيانِ الرجلِ امْرَأَتَهُ في دُبُرِهَا، فقالَ النبيُّ: «حلالٌ»، فلمَّا وَلَّى الرجلُ دعاهُ أَوْ أَمَرَ بِهِ فدُعِيَ فقالَ: «كيفَ قلتَ، في أيِ الخُرْبَتَيْنِ أَوْ فِي أَيِّ الخُرْزَتَيْنِ أو في أيِّ الخُصْفَتَيْنِ أَمِنْ دُبُرهَا في قُبُلِهَا فَنَعَمْ، أَمَّا مِنْ دُبُرِهَا في دُبُرِهَا فَلاَ، إنَّ اللَّهَ لا يَسْتَحْيِي من الحقِّ، لا تَأْتُوا النساءَ في أَدْبَارِهِنَّ»

Imetoka kwa Khuzaymah ibn Thaabit رضي الله عنه "Mtu mmoja alimuuliza Mtume kuhusu kuwaingilia wanawake kwa nyuma au mwanamume kumuendea mkewe kwa nyuma yake. Akasema Mtume kuwa ni ((Halaal)). Alipoondoka Mtume alimwita au aliamrisha aitwe, akasema: ((Ulisema nini? Njia gani kati ya tundu mbili umemaanisha? Ikiwa ulimaanisha kutoka kwa nyuma na kumuingilia mbele (sehemu yake ya siri ya mbele) basi sawa. Lakini ikiwa umemaanisha nyuma katika sehemu yake ya siri ya nyuma basi hapana! Hakika Allaah Haoni hayaa katika haki. Msiwaingilie wake zenu katika njia zao za nyuma))[3]

 
Nne:

((لا يَنْظُرُ اللَّهُ إلى رَجُلٍ أَتَى امْرَأَةً في دُبُرِهَا))

((Allaah Hatomtazama mwanamume anayemuingilia mwanamke kwa nyuma))[4]

 
 

Tano:

 (( مَلْعُون مَنْ ياَتِي النِّسَاءَ فِي مَحَاشِهِنَّ)) ( يعني : أدبارهن)

 

((Amelaaniwa anayewaendea wanawake katika njia zao za nyuma))[5]
 

Sita:

((مَنْ أَتى حَائِضاً أَوِ امْرَأَةً فِي دُبُرِها أَوْ كَاهِناً فَصَدَقَهُ بِمَا يَقُولُ  فقدْ كَفَرَ بمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ))

((Atakayemuingilia mwenye hedhi au mwanamke kwa nyuma au atakayemuendea kahini (mtabiri) akamuamini anayomwambia atakuwa amekufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammad))[6]

 

 

 

[1] Ahmad, At-Tirmidhiy na wengineo ikiwa ni Swahiyh

[2] An-Nasaaiy katika “‘Ishratun-Nisaa” ikiwa ni isnaad hasan, At- Tirmidhiy na wengineo

[3] Ash-Shaafi'iy, Al-Bayhaaqiy na wengineo ikiwa ni Swahiyh

[4] An-Nasaaiy ikiwa ni isnaad hasan, na imetiliwa nguvu katika "Al-Ishrah", At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan

[5] Abu Daawuud, Ahmad na wengineo ikiwa ni isnaad hasan na imetiliwa nguvu

[6] Abu Daawuud, At-Tirimidhiy na wengineo: Swahiyh

Share