20-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuhalalishwa ‘Azl (Kuchopoa Kabla Ya Kushusha)

Kwanza:

عن جابر رضي الله عنه قال:  كنّا نَعزلُ والقرآنُ يَنزِل.  وفي رواية:  كُنَّا نَعْزِلُ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم  :فَبَلَغَ ذلِكَ نَبِيَّ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَلَمْ يَنْهَنَا عَنْهُ

Imetoka kwa Jaabir رضي الله عنه amesema: "Tulikuwa tunafanya 'azl wakati tunawaingilia wake zetu (hatumwagi ndani; tunachomoa utupu na kumwaga nje) na Qur-aan ilikuwa ikiteremshwa"[1]

 
Na katika riwaaya nyingine amesema: "Tulikuwa tukifanya tendo la ‘azl wakati wa maisha ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na hakutukataza kufanya hivyo".[2]

 
 

Pili:

 

عن أبي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قال: جآء رَجُلٌ إِلى رَسُولِ الله صَّلى الله عليه وسلم فَقَال: إِنَّ لِي وَلِيدة وَأنا أعْزِلُ عَنْها  وَأَنَا أُرِيدُ ما يُرِيدُ الرِّجَالُ وَإنَّ الْيَهُودَ  زَعَمُوا أَنَّ الْمَوءُودَةُ الصُّغْرَى  الْعَزْلُ؟ فَقَالَ رَسُولُ الله: ((كَذَبَتْ يَهُودُ، لَوْ أَرَادَ اللَّهُ أَنْ يَخْلُقَهُ لَمْ تَسْتَطِعْ أَنْ تَصْرِفَهُ))

 

Imetoka kwa Abu Sa'iydil-Khudriy amesema: "Alikuja mtu kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: 'Ninaye  kijakazi (unaomiliki mkono wa kulia) na nilikuwa nikifanya ‘azl kwake, na mimi ninataka yale watakayo wanaume, na Mayahudi wanadai kuwa, 'Azl ni aina ndogo ya uuaji'. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Mayahudi wameongopa, Mayahudi wameongopa. Allaah Angelitaka kuumba mtoto usingeliweza kuzuia))[3]

 

Tatu:

 

عَنْ جَابِرٍ أَنَّ رَجُلاً أَتَى رَسُولَ اللّهِ فَقَالَ: "إِنَّ لِي جَارِيَةً هِيَ خَادِمُنَا وَسَانِيَتُنَا، وَأَنَا أَطُوفُ عَلَيْهَا وَأَنَا أَكْرَهُ أَنْ تَحْمِلَ". فَقَالَ: ((اعْزِلْ عَنْهَا إِنْ شِئْتَ. فَإِنَّهُ سَيأْتِيَهَا مَا قُدِّرَ لَهَا)) فَلَبِثَ الرَّجُلُ. ثُمَّ أَتَاهُ فَقَالَ: "إِنَّ الْجَارِيَةَ قَدْ حَبِلَتْ". فَقَالَ ((قَدْ أَخْبَرْتُكَ أَنَّهُ سَيَأْتِيهَا مَا قُدِّرَ لَهَا))

Imetoka kwa Jaabir kwamba alikuja mtu kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: 'Ninaye kijakazi ambaye anatuhudumia na kumwagia maji mitende yetu. Wakati mwingine humuendea (humuingilia) lakini sikupenda ashike mimba yangu. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: ((Fanya ‘azl kwake, lakini kilichokadiriwa kwake huwezi kukizuia, kitakuwa)). Baada ya muda yule mtu akaja kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na akasema: 'Ameshika mimba!' Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamuambia, ((Nilikuambia kuwa vyovyote ilivyokadiriwa itakuwa))[4]
 

 

[1] Al-Bukhaariy na Muslim

[2] Muslim, An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy

[3] An-Nasaaiy katika "Al-Ishraah", Abu Daawuud na wengineo: Swahiyh

[4] Muslim, Abu Daawuud na wengineo

Share