Supu Ya Brokoli (Broccoli)

Supu Ya Brokoli (Broccoli)

 

Vipimo

Brokoli - 1 msongo (bunch)

Parlsely - 3 misongo

Karoti - 2

Viazi - 2

Vitunguu - 1 – 2

Nyanya - 1

mraba wa supu ya nyama au kuku - kidonge 1 (au supu yenyewe kiasi kidogo tu cha kutia ladha lakini hakikisha supu isizidishe kipimo)

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Ndimu - 1 kijiko cha chai

Mafuta - 2 kijiko cha supu

Zaytuni - kiasi

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Chambua brokoli, katakata karoti, viazi, vitunguu na nyanya.
  2. Chemsha brokoli, karoti na viazi.
  3. Tia mafuta katika sufuria kaanga vitunguu hadi vilainike, tia nyanya, endelea kukaanga.
  4. Tia pilipilimanga, chumvi na kidonge cha supu.
  5. Mimina vitu ulivyochemsha na supu yake katika mkaango.
  6. Tia katika mashine ya kusagia (blender).
  7. Tia parselye usage kidogo tu, kisha rudisha katika sufuria urejeshe katika moto na ipike kidogo kwa muda wa 1 tu.
  8. Onja chumvi, ndimu ikiwa tayari kuliwa pekee au na mkate na zaytuni.

 

Share