Juisi Ya Mabungo

Juisi Ya Mabungo

 

Vipimo: Kupata takriban gilasi 6

Mabungo - 3

Maji -  6 au 7 Gilasi

Sukari - kiasi upendacho

Chumvi - kidogo sana

Namna Ya Kutayarisha:

  1. Kata mabungo na toa nyama yake tia katika mashine ya kusagia.
  2. Tia maji, sukari na chumvi usage kidogo tu.
  3. Chuja kisha mimina katika jagi uweke katika friji.
  4. Mimina katika gilasi.
Share