Kutumia Toilet Paper Kwa Kujisafisha Choo

Kutumia Toilet Paper Kwa Kujisafisha Choo

 

 

 

 

SWALI: 

 

Inafaaa kujisafisha haja ndogo (mkojo) kutumia toilet paper? 

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho 

 

 

Kutumia toilet paper au karatasi, Shariy’ah iko wazi ikiwa maji yamekosekana basi ni  ya Istijmaar (kutumia mawe kujisafisha) na karatasi inachukua mahali pa mawe. Hata maji yakiwepo unaweza kujisafisha na karatasi kwanza kisha ukatumia maji ili usafi uwe mzuri zaidi, na hivyo ni bora zaidi.

 

Lakini tena kwenye suala hilo la kutumia makaratasi, tunavyojua vyoo vilivyopo nchi za kigeni ni kweli hawaweki vyombo vya maji kwa ajili ya kujisafishia, lakini tunavyofahamu kuwa hakatazwi mtu kuingia na chupa yake au kikombe chake cha kutumia na kutupa ‘disposable cups’ na kutumia kwa haja yake.

 

Kinachowazuia wengi kufanya hivyo, si makatazo, bali ni kuwaonea hayaa wazungu  ndio kunawapelekea wengi kutafuta njia za mkato na hali hakuna dharura hiyo. 

 

Ama ikiwa hakuna maji kabisa sehemu hiyo, basi hukatazwi kutumia toilet paper. Na kama kuna maji lakini umekosa kabisa chombo cha kutumia kutekea maji na kujisafishia, basi unaweza kuzitumia hizo toilet paper na kuzichovya kwenye maji kisha ukajisafishia ili kupatikane usafi zaidi na kutakatike na kuhakikishike kuwa hakujabaki aina yoyote ya uchafu.  

 

Hata hivyo kwa zama za sasa imebainika kwamba vyoo vingi vya nchi za kigeni wanatumia maji.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share