Watoto Wa Kiume Wa Wifi Ni Mahaarim Wangu?

 

Watoto Wa Kiume Wa Wifi Ni Mahaarim Wangu?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Assalam Aleikum Warahmatullahi Wabarakatu.

 

Mimi nimeolewa na mjomba wao je? Nivae hijab mbele ya watoto wa wifi yangu. JazakAllaahu alf kheri.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Tunakushukuru kwa Swali hili muhimu lenye mas-ala ambayo watu wengi hawayatilii manani kwa kufeli kutambua hukmu yake na umuhimu wa kufuata amri za Hijaab. Mfano vile vile wengi huona kwamba mwanamke anaweza kukaa mbele ya shemeji zake, ikiwa ni mume wa dada au kaka wa mume au pia inavyojulikana zaidi kwa neno la Kiingereza 'cousin' yaani  mtoto wa ammi au mtoto wa mjomba au mtoto wa shangazi. Na jamaa wengine wote ambao wanaouhusiana kwa ukaribu.

 

Madamu wote hao wanaweza kukuoa basi hao sio Mahaarim (Maharimu) wako bali mahaarim wako ni wale tu waliotajwa katika Aayah ifuatayo:

 

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣١﴾

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao, na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wao (wa Kiislamu), au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio ya jimai miongoni mwa wanaume au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake. Na wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao. Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu. [An-Nuwr: 31]

 

 

Kwa hiyo watoto wa wifi yako sio Mahaarim wako kwani wao hawakutajwa hapo na wanaweza kukuoa.  Basi inakupasa ujifunike na kujisitiri vizuri kwa kuficha kila aina ya mapambo yako mbele yao.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share