Sababu Za Kuwa Na Miezi Mitukufu

Sababu Za Kuwa Na Miezi Mitukufu

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI

 

nilikuwa na masuala yafuatayo.

katika kuran tukufu suratul tawbah aya 35 kumetajwa kuhusu miezi mitukufu nayo ni 4,dhul qaidah(huu uloanza leo),dhul hijjah,muharam na rajab. sualalangu,nataka kujua    a)jee kuna kisa gani kulitokea mpaka ikawa mitukufu hiyo miezi.b) kuna ibada za sunna za kufunga ktk miezi hii,jee zikoje duas za kuomba n.k

shukrani sana.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kuhusu ‘ibaadah za kutekeleza katika miezi mitukufu, maelezo na faida tele zinapatikana katika kiungo kifuatacho:

 

 'Amali Za Kutenda Na Mambo Ya Kujiepusha Nayo Katika Miezi Mitukufu

 

 

 

Miezi mitukufu ilijulikana kuwa ni mitukufu tokea zama za ujaahiliyyah (Kabla ya Uislamu):

 

 عن أبي بَكْرَةَ رضي الله عنه عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أنه قَالَ:  ((إن الزَّمَانَ قَدْ اسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ يَوْمَ خَلَقَ اللَّهُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ السَّنَةُ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ثَلاثٌ مُتَوَالِيَاتٌ ذُو الْقَعْدَةِ وَذُو الْحِجَّةِ وَالْمُحَرَّمُ وَرَجَبُ مُضَرَ الَّذِي بَيْنَ جُمَادَى وَشَعْبَانَ))

Imepokelewa kutoka kwa Abu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mgawano wa zama umerudi katika hali yake ya asili siku Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili; minne miongoni ya hiyo ni mitukufu, mitatu inafuatana pamoja; Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na Al-Muharram, mwengine ni Rajab wa (kabila la) Mudhwarr ambao uko baina ya Jumaadaa na Sha'baan))  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefananua katika Hadiyth hiyo  kwamba ‘Rajab ya Mudhwarr’ ni kwa ajili ya kuthibitisha kauli ya kabila la Mudhwarr wanayosema kwamba Rajab ni mwezi baina ya Jumaadah na Sha’baan na sio kama walivyodhani kabila la Rabiy’ah kwamba uko baina ya Sha’baan na Shawwaal ambao ni Ramadhwaan katika kalenda ya sasa.

 

Miezi mitatu katika hiyo inafuatana ili iwezekane kutekelezwa fardhi ya Hajj kwa wepesi.

 

Dhul-Qa’adah: Mwezi wa kabla ya Hajj umefanywa mtukufu kwa sababu watu walijizuia kupigana katika mwezi huo.

 

Dhul-Hijjah: Umefanywa mtukufu kwa sababu fardhi na taratibu za Hajj zinatekelezwa na kukamilishwa humo.

 

Al-Muharram: Unafuata baada ya Hajj, umefanywa mtukufu ili watu waweze kurudi makwao kwa usalama baada ya kutekeleza Hajj.

 

Rajab: Uko katikati ya mwaka, umefanywa mtukufu ili watu waliokuwa wanakuja kutoka pande za mbali za bara la Arabuni waweze kufanya ‘Umrah na kutembelea Al-Ka’bah kisha warudi makwao kwa usalama.  [Tafsiyr Ibni Kathiyr]

  

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share