Hii Ndiyo ‘Aqiydah (Itikadi) Sahihi Ya Kiislamu

 

 

Hii Ndiyo ‘Aqiydah (Itikadi) Sahihi Ya Kiislamu

 

Imeandikwa Na:  Imaam Muhammad Bin Swaalih Al-'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

Imetarjumiwa Na: Muhammad Faraj Saalim As-Sa'y (Rahimahu Allaah)

Na Kupitiwa Na: Abu 'Abdillaah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بسم الله الرحمن الرحيم

 

  

 

Utangulizi

 

‘Aqiydah (Itikadi) Yetu

 

Sifa Ya Kusema

 

Sifa Ya Kuwepo Kwake Juu 'Al-'Uluw

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anayo 'Arsh

 

Sifa Ya Kushuka

 

Sifa Ya Iraada (Atakavyo,  Apendavyo Allaah)

 

Sifa Ya Kupenda

 

Wajihi Wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

Mikono

 

Macho

 

Tanbihi

 

Malaika

 

Vitabu

 

Manabii

 

Dini Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

Khalifa Waongofu

 

Siku Ya Mwisho (Qiyaamah)

 

Ash-Shafaa’ah (Uombezi)

 

Hodhi Na Swiraatw

 

Jannah (Pepo) Na Moto

 

Masuali Ya Kaburini

 

Adhabu Ya Kaburini

 

Qadar

 

Mashiy'atu-Allaah (Kutaka Kwa Allaah)

 

Baadhi Ya Faida

 

Matunda Ya Kuamini Malaika

 

Matunda Ya Kuviamini Vitabu

 

Matunda Ya Kuamini Manabii

 

Matunda Ya Kuiamini Siku Ya Qiyaamah

 

Matunda Ya Kuamini Qadar

 

 

 

 

Utangulizi

 

Shukrani zote ni zake Rabb wa uliwengu wote, na mwisho mwema ni wa wamchao Allaah, na hapana uadui isipokuwa kwa madhalimu.

Nashuhudia kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah Peke yake Asiye na mshirika mwenye Ufalme na haki iliyo wazi. Na nashuhudia kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mjumbe wake na Rasuli wake na mwisho wa Rusuli wake na ni kiongozi wa wenye taqwa. Rabb wetu mswalie na msalimie Nabiy wako huyu pamoja na Swahaba wake na kila atakayemfuata kwa wema na uongofu mpaka Siku ya Qiyaamah.

 

 

Amma baad,

Hakika Allaah amemtuma Rasuli wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awe dalili iliyo wazi juu ya waja wake, na awabainishie yale aliyoteremshiwa katika Kitabu, na awe mfano mwema wa kuigwa na walimwengu wote, na ili watu wapate kuwa na muongozo mwema katika dini yao na dunia yao.

 

Ametumwa kutufundisha ‘Aqiydah (Itikadi) sahihi pamoja na hekima kwa ajili ya kutengenea hali ya umati wake, na pia kuwaweka juu ya njia safi na sahihi, ili watu wawe juu ya kitanga cheupe, mchana wake sawa na usiku wake, na asiende kinyume na njia hiyo isipokuwa mpotofu.

 

Wakaifuata njia hiyo Swahaba wake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na wale waliokuja baada yao na waliowafuatilia kwa wema. Wakaisimamisha shari’ah ya Allaah na kuyakamata vizuri mafundisho hayo kwa magego yao kwa kuifuata ‘Aqiydah (itikadi) hii iliyo sahihi, na ibada na mwenendo na tabia. Na sisi Alhamdulillah tunaendelea kuufuata mwenendo wao huo kwa kufuata dalili zilizomo ndani ya Qur-aan na zilizomo ndani ya mafundisho yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na tunamuomba Allaah Atuthibitishe juu ya njia hiyo sisi na ndugu zetu wote wa Kiislamu kwa kauli iliyo thabit katika maisha ya duniani na ya Aakhirah na atumiminie rehma Zake kwani yeye ni Mwenye kutoa kwa wingi.

 

 

Kutokana na umuhimu wa maudhui haya, na kutokana na tofauti iliyokuja baadaye, baada ya kuingizwa matamanio ya watu ndani ya ‘Aqiydah (Itikadi) hii, nilipenda kuiandika iwe kama ndiyo ‘Aqiydah yetu. ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah, nayo ni imani ya kuwepo kwa Allaah na Malaika Wake na vitabu Vyake na Manabii Wake na Siku ya Qiyaamah na Qadar (qudra) kheri yake na shari yake.

Namuomba Allaah Aijaalie kazi hii iwe halisi kwa ajili yake, Aridhike nayo na iwe funzo kwa waja Wake.

 

 

 

 

‘Aqiydah (Itikadi) Yetu: 

 

‘Aqiydah (Itikadi) yetu ni kumuamini Allaah na Malaika Wake na Rusuli Wake na Vitabu Vyake na Siku ya Mwisho na kila kinachotokea au kutusibu (Qadar) kheri na shari, vyote vinatoka kwa Allaah.

 

Kwa hivyo sisi tunaamini kuwa Yeye (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ndiye Aliyeumba na Ndiye Mfalme Mwenye kukiendesha kila kitu, na ni Yeye Peke Yake Anayestahiki kuabudiwa, na kila kinachoabudiwa kisichokuwa Yeye ni baatwil (upotofu, hakina faida).

 

Tunaamini pia kuwa Allaah Anayo majina mazuri mazuri na sifa nzuri nzuri na njema, sifa za ukamilifu, na tunaamini kuwa Yeye ni mmoja Asiye na mshirika katika kuumba Kwake na katika kuabudiwa Kwake na katika majina Yake mazuri na katika sifa Zake njema.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾

Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake; basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)? [Maryam 19: 65]

 

 

Na tunaamini kuwa Yeye ndiye:

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kuzunguka chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa, Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah 2: 255]

 

 

Na tunaamini kuwa:

 

هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾

Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Hashr 59: 22-24]

 

 

Na tunaamini kuwa:

 

لِّلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ يَهَبُ لِمَن يَشَاءُ إِنَاثًا وَيَهَبُ لِمَن يَشَاءُ الذُّكُورَ﴿٤٩﴾  أَوْ يُزَوِّجُهُمْ ذُكْرَانًا وَإِنَاثًا ۖ وَيَجْعَلُ مَن يَشَاءُ عَقِيمًا ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ قَدِيرٌ﴿٥٠﴾

 

Ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anaumba Atakavyo. Humtunukia Amtakaye wana wa kike, na Humtunukia Amtakaye wana wa kiume. Au Huwachanganya wa  kiume na wa kike, na Humjaalia Amtakaye kuwa ni tasa, hakika Yeye ni Mjuzi wa yote, Muweza wa yote. [Ash-Shuwraa: 49 – 50]

 

 

Na tunaamini kuwa:

 

فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَمِنَ الْأَنْعَامِ أَزْوَاجًا ۖ يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ ۚ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿١١﴾ لَهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٢﴾

 

Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Amekujaalieni kutokana na nafsi zenu mume na mke na katika wanyama wa mifugo dume na jike. Anakusambazeni humo. Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote Ni Zake funguo za mbingu na ardhi, Anamkunjulia riziki Amtakaye na Anazuia (kwa Amtakaye). Hakika Yeye ni Mjuzi kwa kila kitu. [Ash-Shuwraa: 11 - 12]

 

 

Na tunaamini kuwa:

 

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا ۚ كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴿٦﴾

Na hakuna kiumbe chochote kitembeacho katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah; na (Allaah) Anajua mahali pake pa kustakiri na pa kuhifadhiwa kwake. Yote yamo katika Kitabu kinachobainisha [Huwd: 6]

 

 

Na tunaamini kuwa:

 

 وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩﴾

Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua, na wala punje katika viza vya ardhi, na wala kilichorutubika na wala kikavu isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha wazi. [Al-An’aam: 59]

 

 

Na tunaamini kuwa:

 

إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾

Hakika Allaah Ana elimu ya Saa (Qiyaamah), na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika tumbo la uzazi, na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Luqmaan: 34]

 

 

 

Sifa Ya Kusema

 

Tunaamini kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema wakati wowote Anapotaka na kwa njia yoyote Anayotaka.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا ﴿١٦٤﴾

“Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja.” [An-Nisaa: 164]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ… ﴿١٤٣﴾

“ Na alipokuja Muwsaa katika muda na pahala pa miadi Yetu, na Rabb wake Akamsemesha…” [Al-A’raaf: 143]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا ﴿٥٢﴾

Na Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri. [Maryam: 52]

 

 

Na tunaamini kuwa:

 

قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا ﴿١٠٩﴾

Sema: Kama bahari ingelikuwa ni wino wa (kuandika) maneno ya Rabb wangu, basi ingelimalizika bahari kabla ya kumalizika maneno ya Rabb wangu, japokuwa Tungelileta mfano wake kujaza tena. [Al-Kahf: 109]

 

 

Na tunaamini kuwa:

 

وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِن بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَّا نَفِدَتْ كَلِمَاتُ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٧﴾

Na lau kama miti yote iliyomo katika ardhi ingekuwa ni kalamu, na bahari (ikafanywa wino), ikaongezewa juu yake bahari saba; yasingelimalizika Maneno ya Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Luqmaan: 27]

 

 

Na tunaamini kuwa maneno Yake ni ya ukamilifu uliokamilika na ya ukweli uliokamilika na yenye uadilifu uliokamilika.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١١٥﴾

Na limetimia neno la Rabb wako kwa kweli na uadilifu. Hakuna mwenye kuyabadilisha maneno Yake. Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Al-An’aam: 115]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا ﴿٨٧﴾

Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah? [An-Nisaa: 87]

 

 

Na tunaamini kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah, Aliyeyatamka kwa uhakika kabisa kwa kumfundisha Jibriyl aliyeiteremsha ndani ya kifua cha Rasuli wa Allaah Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ  

Sema: Ameiteremsha Ruwhul-Qudus (Jibriyl) kutoka kwa Rabb wako kwa haki [An-Nahl: 102]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

 وَإِنَّهُ لَتَنزِيلُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٩٢﴾ نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ ﴿١٩٣﴾ عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنذِرِينَ ﴿١٩٤﴾ بِلِسَانٍ عَرَبِيٍّ مُّبِينٍ ﴿١٩٥﴾

 

Na hakika hii (Qur-aan) ni uteremsho wa Rabb wa walimwengu. Ameiteremsha haya Ar-Ruwh (Jibriyl) mwaminifu. Juu ya moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwe miongoni mwa waonyaji. Kwa lugha ya Kiarabu bayana. [Ash-Shu’araa: 192 – 195]

 

 

 

Sifa Ya Kuwepo Kwake Juu ‘Al-Uluw

 

Tunaamini kuwa Allaah yupo juu kabisa mbali na viumbe vyake kwa dhati Yake na kwa sifa Zake, na hii inatokana na kauli Yake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anaposema:

 

وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

Naye ni Mwenye Uluwa; Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah (2): 255]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ﴿٤﴾

Malaika na Ar-Ruwh (roho za viumbe au Jibriyl) wanapanda Kwake katika siku kadiri yake ni miaka khamsini elfu. [Al-Ma’aarij: 4]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ﴿١٦﴾ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ﴿١٧﴾

Je, mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu. [Al-Mulk: 16 – 17]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١٨﴾

Naye ni Asiyepingika, Aliye Mkuu kabisa juu ya waja Wake; Naye ni Mwenye hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-An’aam: 18]

 

 

Na imekuja katika Sunnah (Mafundisho ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Mrehemu aliye ardhini Atakurehemu aliye mbinguni."

[Abu Ya’ala na Atw-Twabaraaniy na Al-Haakim]

 

 

Na kuwepo mbinguni hakuna maana kuwa yupo katika mojawapo ya sayari zilizopo juu kama baadhi ya watu wanavyoweza kudhania, bali dunia yetu ukiilinganisha na mbingu ni mfano wa doa dogo sana, bali hata haionekani. Kwani huko juu kuna nyota na sayari zilizoenea hata kama mtu atasafiri kwa kasi ya kupita kiasi (speed of light) basi atachukuwa mamilioni ya miaka na hatoweza kufika mwisho wake, na hata kama ataufikia mwisho wake, basi atakuta kuwa bado ipo anga isiyo na mwisho. Kwa hivyo ni Allaah Peke Yake ndiye Mwenye kuelewa mfano ya kuwa juu Kwake Subhaanahu wa Ta’ala.

 

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Anayo 'Arsh

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ

Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu (Istawaa) ya ‘Arsh.  [Yuwnus: 3]

 

 

Na kuwa juu ya ‘Arshi Yake ni kuwa kunakonasibiana na utukufu wake Subhaanahu wa Ta’ala, hapana anayejua mfano wake isipokuwa Yeye.

 

 

Na tunaamini kuwa Allaah Akiwa juu ya ‘Arshi Yake, Yupo pamoja na viumbe Vyake kwa elimu Yake.  Anasikia kauli zao na kuona vitendo vyao, huku Akiyaendesha mambo yao. Anamruzuku fakiri na Anampa ufalme Amtakaye na Anamuondolea ufalme amtakaye, Anamnyanyua amtakaye na Anamuangusha amtakaye, na tunaamini kwamba kheri yote imo mikononi Mwake Subhaanahu wa Ta’ala, na kwamba Yeye ni muweza wa kila jambo.

 

 

Na Yeyote mwenye uwezo huo, basi bila shaka yupo pamoja na viumbe vyake kikweli huku akiwa juu ya Arshi yake kikweli, na ni Yeye Peke yake ndiye mwenye kuujuwa uhakika wake.

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿١١﴾

Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Ash-Shuwraa: 11]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَالْمَلَكُ عَلَىٰ أَرْجَائِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَانِيَةٌ﴿١٧﴾

Na Malaika watakuwa pembezoni mwake, na watabeba ‘Arsh ya Rabb wako juu yao siku hiyo (Malaika) wanane. [Al-Haaqah: 17]

 

 

 

Sisi hatusema kama wanavyosema wengine kuwa eti Allaah yupo ardhini pamoja na viumbe Vyake, kwani tunaona kuwa kusema hivyo ni kukufuru au ni upotofu, kwa sababu kumpa Allaah wasfu usiolingana naye ni kupunguza katika sifa Zake.

 

 

 

 

Sifa Ya Kushuka

 

Tunaamini pia yale aliyotujulisha Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa Allaah Anashuka katika mbingu za dunia kila usiku katika thuluthi ya mwisho na kusema:

"Nani mwenye kuniomba nimkubalie, nani mwenye kuniomba nimpe, nani mwenye kuniomba maghfira nimghufirie."

 

Alipoulizwa Imaam Ash-Shaafi’iy:

'Vipi Allaah Anashuka?'

Akajibu:

'Kwani vipi Alipanda?'

 

Na tunaamini kuwa Allaah Atakuja Siku ya Qiyaamah kuwahukumu viumbe vyake.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا ﴿٢١﴾ وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ﴿٢٢﴾

Laa hasha! Pale ardhi pale itakapo vunjwavunjwa na kupondwapondwa.   Na Atakapokuja Rabb wako, na Malaika safusafu. [Al-Fajr: 21 – 122]

 

 

 

 

Sifa Ya Iraadah (Atakavyo, Apendavyo Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa) )

 

Tunaamini kuwa Allaah Anatenda Atakavyo.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ ﴿١٦﴾

Mwingi wa kufanya Atakalo. [Al-Buruwj: 16]

 

 

Na tunaamini kuwa zipo Irada namna mbili. 

 

Ya kwanza Anatujulisha katika kauli Yake:

 

  وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿٢٥٣﴾

Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Ayatakayo. [Al-Baqarah: 253]

 

 

Na hapa maana yake ni ‘kutaka’, kama ilivyo katika kauli Yake:

 

وَلَا يَنفَعُكُمْ نُصْحِي إِنْ أَرَدتُّ أَنْ أَنصَحَ لَكُمْ إِن كَانَ اللَّـهُ يُرِيدُ أَن يُغْوِيَكُمْ ۚ هُوَ رَبُّكُمْ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٣٤﴾

Na wala haitokufaeni nasaha yangu nikitaka kukunasihini ikiwa Allaah Anataka kukuacheni kupotea. Yeye ndio Rabb wenu, na Kwake mtarejeshwa.  [Huwd: 34]

 

 

Na uwezo mwingine ni wa kishari’ah, na Hamtakii isipokuwa Anayempenda, kama ilivyo katika kauli Zake Subhaanahu wa Ta’alaa:

 

يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمْ وَيَهْدِيَكُمْ سُنَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ وَيَتُوبَ عَلَيْكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦﴾ وَاللَّـهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ وَيُرِيدُ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الشَّهَوَاتِ أَن تَمِيلُوا مَيْلًا عَظِيمًا ﴿٢٧﴾ يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا ﴿٢٨﴾

Allaah Anataka kukubainishieni na kukuongozeni nyendo za wale walio kabla yenu, na Apokee tawbah kwenu. Na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote. Na Allaah Anataka kupokea tawbah kwenu; na wale wanaofuata matamanio wanataka mkengeuke, mkengeuko mkubwa mno. Allaah Anataka kukukhafifishieni (tabu zenu); kwani insani ameumbwa dhaifu [An-Nisaa: 26 – 28]

 

 

(Na maana yake hapa ni kuwa 'Hivi Ndivyo Anavyotaka Allaah' lakini kakupeni uhuru wa kuchagua wenyewe mnakotaka kwenda.)

 

 

Na tunaamini kuwa Atakacho Allaah katika mambo ya kilimwengu na ya kishari’ah yote ni katika hekima Yake, na hafanyi kitu bila ya kuwa na hekima kubwa ndani yake, na sisi huenda tukaijua hekima hiyo au tusiijuwe kutokana na upungufu wa akili zetu.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴿٨﴾

Je, kwani Allaah Si Mwadilifu zaidi wa wanaohukumu kuliko mahakimu wote?   [At-Tiyn: 8]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

   وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٥٠﴾

Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini. [Al-Maa’idah: 50]

 

 

 

 

Sifa Ya Kupenda

 

 

Na tunaamini kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anawapenda waja Wake wenye taqwa nao wanaompenda.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.  [Aal-‘Imraan: 31]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

  فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ  

Basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; [Al-Maaidah: 54]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَاللَّـهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٦﴾

Na Allaah Anapenda wanaosubiri. [Aal-‘Imraan: 146]

 

 

 

Na tunaamini kuwa Allaah Huridhika zinapofuatwa shari’ah Zake na huchukizwa zisipofuatwa.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنكُمْ ۖ وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ ۖ ..﴿٧﴾ 

Mkikufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwenu, na wala Haridhii kufuru kwa waja Wake. [Az-Zumar: 7].

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

  وَلَـٰكِن كَرِهَ اللَّـهُ انبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ اقْعُدُوا مَعَ الْقَاعِدِينَ﴿٤٦﴾

Na ingelikuwa wametaka kutoka, bila shaka wangeliandaa maandalizi yake, lakini Allaah Amekirihika kutoka kwao, basi Akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanaokaa. [At-Tawbah: 46]

 

 

Na tunaamini kuwa Allaah Huridhika na wale wanaoamini na kufanya mema.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ رَبَّهُ ﴿٨﴾

Allaah Ataridhika nao, nao wataridhika Naye; hayo ni kwa yule anayemkhofu Rabb wake. [Al-Bayyinah: 8]

 

 

Na tunaamini kuwa Allaah Anamkasirikia kila mwenye kustahiki kukasirikiwa katika makafiri na wasiokuwa makafiri.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الظَّانِّينَ بِاللَّـهِ ظَنَّ السَّوْءِ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۖ وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ

Wanaomdhania Allaah dhana ovu.  Utawafikia mgeuko mbaya; na Allaah Awaghadhibikie, [Al-Fat-h: 6]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

   وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٠٦﴾

Lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao juu yao ni ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kuu. [An-Nahl: 106]

 

 

 

Wajihi Wa Allaah

 

Na tunaamini kuwa Allaah Anao wajihi wenye utukufu na ukarimu.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾

Na utabakia Wajihi wa Rabb wako Mwenye Ujalali na Taadhima. [Ar-Rahmaan: 27]

 

 

 

Mikono

 

 

Tunaamini kuwa Allaah Anayo mikono miwili mitukufu.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ

Bali Mikono Yake (Allaah) imefumbuliwa Hutoa Atakavyo. [Al-Maaidah: 64]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٦٧﴾

Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria; na hali ardhi yote itatekwa Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’aalaa (Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa) kutokana na yale yote wanayomshirikisha. [Az-Zumar (39:67)]

 

 

(Siku ya Ridhwaan Waislamu walipofungamana na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) chini ya mti kwa kumpa mkono wote kwa pamoja, mmoja baada ya mwengine, na Allaah Akateremsha kauli Yake:

 

إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّـهَ يَدُ اللَّـهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ  

Hakika wale waliofungamana ahadi ya utiifu nawe, hakika hapana ila wanafungamana ahadi ya utiifu na Allaah, Mkono wa Allaah Uko juu ya mikono yao.  [Al-Fat-h: 10]

 

 

Ieleweke kuwa Allaah Anaposema Anayo mikono au macho, haina maana kuwa mikono Yake ni sawa na mikono yetu, au macho Yake ni sawa na macho yetu - AstaghfiruLlaah. Meza inayo miguu na viti vina miguu, lakini miguu ya viti na ya meza ni tofauti na miguu ya mwanaadamu aloitengeneza meza ile, kwani sifa ya mtengenezaji lazima iwe tofauti na sifa ya kilichotengenezwa, ama sivyo mtengenezaji na kilichotengenezwa watakuwa kitu kimoja. Na Allaah Ndiye mwenye kupigiwa mifano bora, Sifa Zake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) haziwezi kufananishwa na sifa zetu. Lakini wakati huo huo lazima tukikubali kila Alichojinasibisha nacho Subhaanahu wa Ta’ala.)

 

 

 

 

Macho

 

Na tunaamini kuwa Allaah Anayo macho mawili kikweli, na hii inatokana na kauli Yake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Aliposema kumwambia Nuwh (‘Alayhis-Salaam):

 

وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا  

Na unda jahazi mbele ya macho Yetu na ufunuzi wa Wahy Wetu [Huwd: 37]

 

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa  sallam) amesema: "Pazia yake ni nuru, na lau kama Ataiondoa basi nuru ya Wajihi Wake ingeunguza kila kilichokifikia."

 

Na alipokuwa akihadithia juu ya Ad-Dajjaal alisema: "Dajjaal ana chongo na Rabb wenu Hana chongo."

 

 

Na tunaamini kuwa macho yetu hayamfikii kumuona Allaah.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote; Naye ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana [Al-An’aam: 103]

 

 

 

Waislamu Watamuona Allaah Qiyaamah

 

Na tunaamini kuwa Waislamu watamuona Rabb wao Siku ya Qiyaamah.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ﴿٢٢﴾ إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ﴿٢٣﴾

 

Nyuso siku hiyo zitanawiri. Zikimtazama Rabb wake. [Al-Qiyaamah: 22 – 23]

 

 

Na tunaamini kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hana mfano Wake katika ukamilifu wa Sifa Zake.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿١١﴾

Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Ash-Shuwraa: 11]

 

 

Na tunaamini kuwa Allaah Hashikwi na usingizi wala halali.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ  

Haumchukui usingizi wala kulala. [Al-Baqarah 2: 255]

 

Na tunaamini kuwa Allaah Hamdhulumu mtu, na hii inatokana na ukamilifu wa uadilifu Wake Subhaanahu wa Ta’ala, na kwamba hapana Asichokijua katika matendo ya waja Wake, na kwamba Hashindiwi na chochote, kwani Anapotaka chochote kiwe hukiambia tu; 'Kuwa' na kikawa.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾

Hakika amri Yake Anapotaka chochote hukiambia: Kun! (Kuwa), nacho huwa. [Yaasiyn: 82]

 

 

Na tunaamini kuwa Allaah Haguswi na machofu wala tabu ya aina yoyote ile.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ﴿٣٨﴾

Na kwa yakini Tumeumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, na wala Haukutugusa uchovu wowote. [Qaaf: 38]

 

 

Na tunakiamini kila Alichojithibitishia Allaah ('Azza wa Jalla) Nafsi Yake, Ansema kuwa Anacho, basi sisi tunaamini kuwa Anacho kwa uhakika, na tunaamini pia kila alichotujulisha Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya Rabb wake, katika Majina Yake Mazuri na Sifa Zake Nzuri.

 

Lakini tunakataa mambo mawili, nayo ni:

 

  1. Kufananisha (kushabihisha). Nako ni kutamka kwa ulimi au kwa moyo kuwa wasfu wa Allaah unafanana na wasfu wa viumbe Vyake.
  2. Na pia tunakataa kukisia. Nako ni kujisemeza moyoni au kutamka kwa ulimi kuzikisia sifa za Allaah kuwa labda ni hivi au vile.

 

Na tunakanusha kila Allaah Alichojikanushia nafsi Yake, au kile alichokikanusha Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na tunakinyamazia kila Alichokinyamazia, na tunaamini kuwa hii ndiyo njia sahihi, kwani kila Alichojikanushia nafsi Yake ni habari kutoka Kwake, na Yeye (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ndiye Mwenye kuijua Nafsi Yake na Ndiye Msema kweli kupita wote, Mwenye mazungumzo bora kupita wote, waja Wake hawana uwezo wa kujua chochote juu Yake bila Yeye kuwajulisha.

 

 

 

 

Tanbihi:

 

 

Kila tulichokitaja katika sifa za Allaah, iwe kwa urefu au kwa ujumla, katika kuthibitisha au katika kukanusha, yote tumeyanukuu kutoka katika kitabu cha Allaah (Qur-aan) au mafundisho ya Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (Sunnah) iliyo sahihi nayo pia ni ‘Aqiydah (Itikadi) waliyokuwa nayo Maimamu wetu wema waliotangulia.

 

 

Tunaona kuwa inawajibika kuzifasiri nassw (dalili) zilizomo ndani ya Qur-aan kwa uhakika wake kama Anavyozistahiki Allaah, na tunajitenga mbali na njia ya wageuzaji wa maana wale waliozigeuza maana na kuzifasiri kwa njia Asiyoitaka Allaah Subhaanahu wa Ta’ala, na tunajitenga mbali na njia ya wabadilishaji waliobadilisha, mbali na maana iliyokusudiwa, na pia tunajitenga mbali na wazidishaji waliozidisha na kuzifanya sifa zake kuwa ni za kumfananisha.

 

 

Tuna hakika kuwa yale yaliyomo ndani ya Kitabu cha Allaah na ndani ya mafundisho ya Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni haki isiyopingana, na hii inatokana na kauli Yake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anaposema:

 

أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا ﴿٨٢﴾

Je, hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka kwa asiyekuwa Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi. [An-Nisaa: 82].

 

 

Na kwa vile kauli zinazopingana huwa zinasutana, na hili ni jambo lisiliowezekana katika habari Anazotupa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na anazotupa Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na yeyote anayedai kuwa ndani ya Kitabu cha Allaah au ndani ya mafundisho ya Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yamo maneno yanayopingana, akasema hayo kwa kukusudia au kwa vile moyo wake umekwenda upande, basi huyo anatakaiwa atubu kwa Rabb wake na atoke ndani ya upotofu wake.

 

 

Na yeyote anayedhani kuwa mna upungufu wowote ndani ya Kitabu cha Allaah au ndani ya mafundisho ya Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au baina yao, basi huyo ima ana upungufu wa elimu au uchache wa fahamu au ana upungufu katika kuzingatia kwake, kwa hivyo aitafute elimu na ajitahidi katika kuzingatia mpaka ukweli utakapombainikia. Na kama haukumbainikia, basi amtafute mwenye elimu kupita yeye na aachane na upotofu wake, na aseme kama wanavyosema wale waliobobea katika elimu:

 

  آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ  

 Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu.  [Aal-‘Imraan: 7]

 

 

Na ajue ya kuwa Qur-aan na Sunnah haviwezi kugongana wala kupingana wala hapana hitilafu baina yake.

 

 

 

 

Malaika

 

 

Na tunaamini juu Malaika wa Allaah kama ulivyokuja wasfu wao ndani ya Qur-aan kwamba wao ni:

بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ ﴿٢٦﴾ لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ ﴿٢٧﴾

 

Bali (hao) ni waja waliokirimiwa. Hawamtangulii (Allaah) kwa kauli, nao kwa amri Yake wanatenda. [Al-Anbiyaa: 26 – 27]

 

Allaah Amewaumba ili wamuabudu na kumtii.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

  لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ ﴿١٩﴾ يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ ﴿٢٠﴾

 

Hawatakabari kumwabudu Kwake na wala hawachoki. Wanasabihi usiku na mchana wala hawazembei. [Al-Anbiyaa: 19 – 20]

 

Allaah Akatujaalia tusiweze kuwaona, na Aliwafanya wengine kati ya waja Wake kuweza kuwaona, kwani Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) akiwa katika umbile lake la kweli ana mbawa mia sita, akiwa ameizinga anga yote juu yake.

 

 

Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) aliwahi pia kuonekana na Bibi Maryam akiwa katika umbile la binaadamu aliyekamilika, akazungumza naye, na aliwahi pia kumjia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa pamoja na Swahaba wake (Radhwiya Allaahu anhum) akiwa katika umbile la mwanamume asiyejulikana wala hapakuwa na ishara yoyote usoni mwake kama ni mtu aliyetoka safari ndefu, akaliegemeza goti lake juu ya goti la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuuweka mkono wake juu ya paja la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kisha akazungumza naye huku Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akimjibu, na baada ya kuondoka ndipo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia Swahaba wake (Radhwiya Allaahu anhum) kuwa yule alikuwa Jibriyl (‘Alayhis-Salaam).

 

 

Na tunaamini kuwa Malaika wana kazi zao maalum walizopewa na Rabb wao. Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) ni mletaji wahyi kwa Rusuli. Anawateremshia kutoka kwa Allaah na kuwafikishia anaotumwa kuwafikishia katika Rusuli Wake Subhaanahu wa Ta’ala. Na yupo Mikaaiyl aliyepewa kazi ya kuteremsha mvua na ya mazao anapopewa amri na Allaah. Na yupo Israafiyl mwenye kazi ya kupuliza parapanda (baragumu) siku ya Qiyaamah. Na yupo Malaika wa kifo aliyepewa kazi ya kutoa roho wakati wa kufa, na yupo Malaika wa majabali, na yupo Malik mlinzi wa mlango wa Motoni, na wapo Malaika wanaowashughulikia watoto wachanga matumboni mwa mama zao, na wengine waliopewa kazi ya kuwahifadhi wanaadamu na wengine wenye kuandika ‘amali zao, na kila mtu ana Malaika wawili.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ﴿١٧﴾ مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾

 

Pale wanapopokea wapokeaji wawili (Malaika) wanaokaa kuliani na kushotoni. Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf: 17 – 18]

 

 

Na wengine wana kazi za kuwauliza maiti baada ya kufikishwa kaburini, wanajiwa na Malaika wawili na kumuuliza Nani Rabb wake, nini dini yake, nani Rasuli wake?

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ﴿٢٧﴾

Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah Anafanya Atakavyo. [Ibraahiym: 27]

 

 

Na wapo Malaika waliopewa kazi ya kuwashughulikia watu wa Jannah (Peponi).

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَالْمَلَائِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ ﴿٢٣﴾ سَلَامٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ ۚ فَنِعْمَ عُقْبَى الدَّارِ ﴿٢٤﴾

 

Na Malaika wanawaingilia katika kila milango. Salaamun ‘Alaykum! (Amani iwe juu yenu) kwa yale mliyosubiri. Basi uzuri ulioje khatima njema ya makazi ya Aakhirah. [Ar-Ra’d: 23 – 24]

 

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitujulisha kuwa ndani ya 'Baytul Ma’amuur', iliyopo mbinguni wanaingia na kuswali ndani yake kila siku Malaika elfu sabini wakishamaliza hawaipati fursa ya kurudi humo tena.

 

 

 

 

Vitabu

 

 

Na tunaamini kuwa Allaah Amewateremshia Rusuli Vitabu ili viwe hoja na mwangaza kwa walimwengu kwa ajili ya kuwafundisha hekima na kwa ajili ya kuwatakasa.

 

Na tunaamini kuwa Allaah Amemteremshia kila Rasuli Kitabu.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ ۖ  

Kwa yakini Tuliwapeleka Risuli Wetu kwa hoja bayana, na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na Miyzaan (shariy’ah) ili watu wasimamie kwa uadilifu [Al-Hadiyd: 25]

 

 

Na katika vitabu hivyo tunavyovijua ni:

 

1. Tawraat (Taurati); Allaah Alimteremsia Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-Salaam), na hiki ni Kitabu kitukufu kupita vyote vya Bani Israaiyl.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ ۚ  

 Hakika Tumeteremsha Tawraat humo mna mwongozo na nuru; ambayo kwayo, Nabiy waliojisalimisha (kwa Allaah), waliwahukumu Mayahudi. Na (kadhalika) wanachuoni waswalihina na wanachuoni mafuqahaa wa dini kwa sababu waliyokabidhiwa kuhifadhi Kitabu cha Allaah; na wakawa mashahidi juu yake. [Al-Maaidah: 44]

  

 

 

2. Injiyl (Injili); Allaah alimteremshia Nabiy ‘Iysaa (‘Alayhis-Salaam), na hiki kinakisadikisha Taurati na kukikamilisha.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

 

وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٦﴾

Na Tukatuma kufuatisha nyao zao (Manabii hao), ‘Iysaa mwana wa Maryam akisadikisha yale yaliyoko kabla yake katika Tawraat. Na Tukampa Injiyl iliyomo ndani yake mwongozo na nuru; na isadikishayo yale yaliyokuwa kabla yake katika Tawraat, na mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa. [Al-Maaidah: 46]

 

 

3.  Zabuwr (Zaburi); Aliyopewa Nabiy Daawuwd (‘Alayhis-Salaam).

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

وَلَقَدْ فَضَّلْنَا بَعْضَ النَّبِيِّينَ عَلَىٰ بَعْضٍ ۖ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿٥٥﴾

Na kwa yakini Tumewafadhilisha baadhi ya Manabii juu ya wengineo. Na Tukampa Daawuwd Zabuwr.  [Al-Israa: 55]

 

 

 

4. Swahiyfah (Suhuf); Walizoteremshiwa Nabiy Ibraahiym na Muwsaa (‘Alayhimas-Salaam).

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ هَـٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ ﴿١٨﴾ صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ ﴿١٩﴾

Hakika haya bila shaka yamo katika maandiko tukufu ya awali. Maandiko tukufu ya Ibraahiym na Muwsaa. [Al-A’laa: 18 -1 9]

 

 

5. Qur-aan tukufu; Aliyoteremshiwa Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwisho wa Manabii.

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ  

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili).  [Al-Baqarah: 184]

 

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 

 

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ   

Na Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki kinachosadikisha Vitabu vilivyokuwa kabla yake na chenye kudhibiti, kushuhudia na kuhukumu juu yake (hivo Vitabu).  [Al-Maaidah 5: 48]

 

 

Kwa Kitabu hiki Allaah Akavifuta vilivyotangulia na Akachukua Yeye mwenyewe jukumu la kukilinda ili kibaki kuwa hoja kwa viumbe wote mpaka siku ya Qiyaamah.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾

Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka ndio Wenye kuihifadhi. [Al-Hijr: 9]

 

 

Ama Vitabu vilivyotangulia, vilikuwa vikiletwa kwa ajili ya wakati maalum, na ukishamalizika wakati wake vinaletwa vingine kuchukua nafasi yake, na hii ndiyo maana havikuwa na uwezo wa kujilinda kutokana na ubadilishaji.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ  

Katika Mayahudi wako wanaobadilisha maneno kuyatoa mahali pake [An-Nisaa: 46]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾

Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao; kisha wakasema: ”Hiki ni kutoka kwa Allaah” ili wabadilishe kwa thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma [Al-Baqarah: 79]

 

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩١﴾

Sema: Nani aliyeteremsha Kitabu ambacho amekuja nacho Muwsaa, (chenye) nuru na mwongozo kwa watu. Mnakifanya kurasa kurasa mkizifichua na mkificha mengi. Na mkafunzwa yale mliyokuwa hamuyajui nyinyi na wala baba zenu. Sema: Allaah (Ameiteremsha); kisha waachilie mbali katika shughuliko la porojo lao wakicheza [Al-An’aam: 91]

 

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُم بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٨﴾ مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ﴿٧٩﴾

 

Na hakika miongoni mwao kuna kundi wanaopotosha Kitabu kwa ndimi zao (wanaposoma) ili mdhanie kuwa hayo ni yanayotoka katika Kitabu, na hali hayo si yenye kutoka katika Kitabu, na wanasema: Hayo ni kutoka kwa Allaah; na hali hayo si kutoka kwa Allaah na wanamsingizia uongo Allaah na wao wanajua. Ni mustahili kwa mtu kwamba Allaah Amempa Kitabu na Al-Hukma na Unabii kisha awaambie watu: Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah Bali (atawaambia): Kuweni Wanachuoni waswalihina kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyadurusu. [Aal-‘Imraan: 78 – 79]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

Enyi Ahlal-Kitaab! Hakika amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anasamehe mengi. Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah Nuru na Kitabu kinachobainisha [Al-Maaidah: 15]

 

 

 

 

Rusuli

 

Na tunaamini kuwa Allaah Amewatuma kwa waja Wake Rusuli ili wawe wabashiri na waonyaji.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٦٥﴾

Rusuli ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa) Rusuli. Na Allaah daima ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [An-Nisaa: 165]

 

 

Na tunaamini kuwa Muhammad ni mbora wa Manabii wote, kisha Ibrahim kisha Muwsaa kisha Nuh kisha ‘Iysaa mwana wa Maryam, na hawa ndio waliohuswa katika Aayah ifuatayo.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۖ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٧﴾

Na pale Tulipochukua kutoka kwa Manabii fungamano lao na kutoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na kutoka kwa Nuwh, na Ibraahiym, na Muwsaa, na ‘Iysaa mwana wa Maryam; na Tukachukua kutoka kwao fungamano gumu. [Al-Ahzaab: 7]

 

 

Na tunaamini kuwa shari’ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imekusanya fadhila zote walizokuja nazo Manabii waliotangulia.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ  

Amekuamuruni katika Dini yale Aliyomuusia kwayo Nuwh, na ambayo Tumekufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na Tuliyomuusia kwayo Ibraahiym, na Muwsaa na ‘Iysaa kwamba: Simamisheni Dini na wala msifarikiane humo.  [Ash-Shuwraa: 13]

 

 

Na tunaamini kuwa Rusuli wote  ni watu, viumbe na hawana uwezo wowote wa kuumba au kugawa rizki wala hawajui ghaibu nk.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ إِنِّي مَلَكٌ  

Na wala sikuambieni kwamba mimi nina hazina za Allaah, na wala sijui ya ghayb; na wala sikuambieni kwamba mimi ni Malaika [Huwd: 31]

 

 

 

Allaah Alimuamrisha Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atamke maneno yafuatayo:

 

قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ  

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah; na wala kwamba najua ya ghayb; na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Sifuati ila yale nilofunuliwa Wahy. [Al-An’aam: 50]

 

 

Na akaamrishwa pia atamke:

 

قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ …﴿١٨٨﴾

Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. [Al-A’raaf: 188]

 

 

Na atamke:

 

 قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا﴿٢١﴾ قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا﴿٢٢﴾

Sema: Hakika mimi sikumilikieni dhara na wala uongofu. Sema: Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allaah na wala sitoweza kupata mahali pa kukimbilia. [Al-Jinn: 21 – 22]

 

 

Na tunaamini kuwa wao ni waja wa Allaah Aliowakirimu kwa kuwapa Risaala:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّـهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّـهَ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٣٩﴾

 

Wale wanaobalighisha ujumbe wa Allaah na wanamkhofu Yeye na wala hawamkhofu yeyote isipokuwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye kuhesabu. [Al-Ahzaab (33: 37]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَآتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَجَعَلْنَاهُ هُدًى لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ أَلَّا تَتَّخِذُوا مِن دُونِي وَكِيلًا ﴿٢﴾ ذُرِّيَّةَ مَنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَبْدًا شَكُورًا ﴿٣﴾

 

Na Tumempa Muwsaa Kitabu na Tukakifanya mwongozo kwa wana wa Israaiyl kwamba: Msimfanye yeyote badala Yangu kuwa ni mtegemewa. Enyi kizazi cha ambao Tuliowabeba pamoja na Nuwh (katika jahazi)! Hakika yeye   alikuwa mja mwenye shukurani. [Al-Israa: 2 – 3]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake pambanuo (la haki na batili) ili awe muonyaji kwa walimwengu. [Al-Furqaan: 1]

 

 

Na juu ya Manabii wengine Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي وَالْأَبْصَارِ ﴿٤٥﴾

Na wakumbuke waja Wetu; Ibraahiym, na Is-haaq, na Ya’quwb, wenye nguvu na busara. [Swaad: 45]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَوَهَبْنَا لِدَاوُودَ سُلَيْمَانَ ۚ نِعْمَ الْعَبْدُ ۖ إِنَّهُ أَوَّابٌ ﴿٣٠﴾

Na Daawuwd Takamtunuku Sulaymaan; uzuri ulioje wa mja! Hakika yeye ni mwingi wa kurudiarudia kutubia.  [Swaad: 30]

 

 

Na juu ya ‘Iysaa mwana wa Maryam Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاهُ مَثَلًا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ﴿٥٩﴾

Yeye (Nabiy ‘Iysaa) si chochote isipokuwa ni mja Tuliyemneemesha, na Tukamfanya ni mfano kwa wana wa Israaiyl. [Az-Zukhruf: 59]

 

 

Tunaamini pia kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amekamilisha Risaalah (Ujumbe) Wake kwa kumleta Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ni Rasuli kwa watu wote.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٥٨﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu nyinyi nyote. (Allaah) Ambaye Pekee Anao ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Anahuisha na Anafisha. Basi mwaminini Allaah na Rasuli Wake; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye anamwamini Allaah na maneno Yake, na mfuateni ili mpate kuongoka. [Al-A’raaf: 158]

 

 

 

 

Dini Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

Na tunaamini kuwa dini alokuja nayo ni Islam aliyoridhika nayo Allaah kwa waja Wake. Na kwamba Allaah Haikubali dini nyingine isipokuwa hii.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ﴿١٩﴾

Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu. [Aal-’Imraan: 19]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ  

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu. [Al-Maaidah: 3]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika [Aal-‘Imraan: 85]

 

 

Na tunaamini kuwa yeyote atakayedai kuwa ipo dini nyengine inayokubaliwa na Allaah isiyokuwa Islamu, kama vile dini ya Kiyahudi au ya Kinasara au dini nyengine yoyote, huyo anakuwa amekufuru, na lazima atubu kwa kufru yake hiyo. Akitubu anasamehewa, ama asipotubu huyo anauliwa kama ni Murtaddi, kwa sababu anakuwa ameikadhibisha Qur-aan tukufu.

 

 

Na tunaamini kuwa hapana tena Nabiy baada ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na yeyote atakayejidai utume baada yake au akamsadiki mwenye kujidai utume anakuwa kafir, kwa sababu anakuwa amemkadhibisha Allaah na Rasuli Wake na Waislamu wote.

 

 

 

 

Khalifa Waongofu

 

 

Na tunaamini kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anao Khalifa waongofu waliouongoza ummah baada ya kufa kwake kwa kueneza elimu na da’awah na uongozi, na kwamba mbora wao ni Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akifuatiwa na ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kisha ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu), kisha ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu), na huu ndio mpangilio wao katika kufadhilishwa kwao.

 

 

Na tunaamini kuwa ummah ule ndio umma bora kupita zote, na hii inatokana na kauli yake Allaah Alipowaambia:

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ  

Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. [Aal-‘Imraan: 110]

 

 

Na tunaamini kuwa walio bora kupita wote ni Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum), kisha waliokuja baada yao, kisha waliokuja baada yao, na kwamba wangali wapo watu wenye kuidhihirisha haki bila kujali lawama za wanaowalaumu, mpaka siku Allaah atakapoleta amri Yake.

 

 

Na tunaitakidi kuwa yaliyotokea baina ya Swahaba (Radhwiya Allaahu anhum) katika fitna na mapambano, yanatokana na jitihada zao katika uamuzi. Wapo waliosibu na wapo waliokosea, na kama alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"Mwenye kujitahidi na kusibu anapata ujira mara mbili, na mwenye kukosea anapata ujira mara moja."

 

Na kwamba Allaah Atawaghufuria makosa yao, na tunaamini kuwa lazima tuache kuwasema vibaya, na badala yake tuwaseme kwa wema, na tusiwataje isipokuwa kwa kuzitaja sifa wanazozistahiki, na tuziondoe chuki zetu juu yao.

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

  لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ

Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi (wa Makkah) na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baadae na wakapigana.  Na wote Allaah Amewaahidi malipo mazuri kabisa.  [Al-Hadiyd: 10]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٠﴾

Na wale waliokuja baada yao wanasema: Rabb wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini; Rabb wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu. [Al-Hashr: 10]

 

 

 

 

Siku Ya Mwisho (Qiyaamah)

 

 

Tunaamini kuwa Siku ya Mwisho ndiyo Siku ya Qiyaamah, ambapo hapana tena siku nyingine baada yake, na siku hiyo Allaah Atawafufua waja wake kwa ajili ya kuwaingiza katika nyumba ya neema 'Jannah (Peponi)', au katika nyumba ya adhabu iumizayo 'Motoni'.

 

Tunaamini kuwa watu watafufuliwa baada ya baragumu kupigwa, kama Allaah Alivyosema:

 

وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ﴿٦٨﴾

Na itapulizwa katika baragumu; watazimia wale walioko mbinguni na ardhini isipokua Amtakaye Allaah. Kisha litapulizwa humo jengine tahamaki hao wanasimama wakitazama. [Az-Zumar: 68]

 

 

Kisha watu watasimamishwa mbele ya Allaah wakiwa kama siku waliyozaliwa bila viatu wala nguo (kama ilivyoelezwa katika Swahiyh Al-Bukhaariy na Muslim – Imepokelewa kuwa Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anha) alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Watu watafufuliwa wakiwa uchi kila mmoja anamtizama mwenzake?" Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Ee ‘Aaishah! mambo siku hiyo yatakuwa magumu kuliko hivyo."

 

Watu hawatakuwa na wakati wa kutazamana - mambo yatakuwa magumu sana - Ya Rabbi Sallim.)

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَوْمَ نَطْوِي السَّمَاءَ كَطَيِّ السِّجِلِّ لِلْكُتُبِ ۚ كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَا ۚ إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ ﴿١٠٤﴾

Siku Tutakapozikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi zilizoandikwa. Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu Yetu. Hakika Sisi ni Wenye kufanya. [Al-Anbiyaa: 104]

 

 

Na tunaamini kuwa watu watapewa madaftari yao kwa mkono wa kulia au nyuma ya migongo yao au kushotoni mwao.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ ﴿٧﴾ فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ﴿٨﴾ وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿٩﴾ وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ ﴿١٠﴾ فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا ﴿١١﴾ وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا ﴿١٢﴾

 

Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia. Atahesabiwa hesabu nyepesi. Na atageuka kwa ahli zake mwenye kufurahi. Na ama yule atakayepewa kitabu chake nyuma ya mgongo wake. Ataomba kuteketea. Na ataingia aungue moto uliowashwa vikali mno. [Al-Inshiqaaq: 7 – 12]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَكُلَّ إِنسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ ۖ وَنُخْرِجُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كِتَابًا يَلْقَاهُ مَنشُورًا ﴿١٣﴾ اقْرَأْ كِتَابَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا ﴿١٤﴾

 

13. Na kila bin Aadam Tumemuambatanishia majaaliwa ya ‘amali zake shingoni mwake. Na Tutamtolea Siku ya Qiyaamah kitabu akutane nacho kimekunjuliwa. (Ataambiwa): Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosheleza leo kukuhesabu. [Al-Israa: 13 – 14]

 

 

Na tunaamini kuwa mezani zitawekwa Siku ya Qiyaamah na kwamba hapana atakayedhulumiwa.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾

 

Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe (au sisimizi) ataiona. Na yule atakayetenda shari uzito wa chembe (au sisimizi) ataiona. [Al-Zalzalah: 7 – 8]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٢﴾ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿١٠٣﴾ تَلْفَحُ وُجُوهَهُمُ النَّارُ وَهُمْ فِيهَا كَالِحُونَ ﴿١٠٤﴾

 

Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni ambao wamekhasirika nafsi zao; katika Jahannam ni wenye kudumu.   Moto utababua nyuso zao; nao humo watakuwa ni wenye midomo iliyosinyaa na kuvutika mbali na meno. [Al-Muuminuwn: 102 – 104]

 

 

 

Ash-Shafaa’ah (Uombezi)

 

Na tunaamini kuwa ipo Ash-Shafa’ah (uombezi wa msamaha) kubwa ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atakapowaombea umma wake baada ya kupewa idhini hiyo na Rabb wake Subhaanahu wa Ta’ala, na baada ya watu kuona dhiki na kuanza kuwaendea Manabii Nuwh kisha Ibraahiym kisha Muwsaa kisha ‘Iysaa (Alayhimus-Salaam) mpaka watakapoishia kwake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Na tunaamini pia kuwa wale watakaoingia Motoni katika Waislamu (tu) nao pia wataombewa Shafaa’ah watolewe humo, na Shafaa’ah hii ni kwa ajili ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Rusuli wengine na watu wema na Malaika, na tunaamini kwamba Allaah Atawatoa Motoni pia makundi kwa makundi ya Waislamu kwa fadhila Zake tu na rehma Yake, bila hata kuombewa Shafaa’ah.

 

 

 

Hodhi na Swiraatw

 

 

Na tunaamini kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ana hodhi lake, na maji yake ni meupe kuliko maziwa na matamu kuliko asali, na yenye harufu nzuri kuliko hal miski. Urefu wake hodhi hilo ni mwendo wa mwezi mzima, na upana wake mwendo wa mwezi mzima.na vyombo vyake vinang'aa kama nyota za mbinguni.

 

Waislamu watakunywa humo, na atakayekunywa hatopata kiu tena.

 

Tuaamini kuwa ipo 'Swiraatw' itakayowekwa juu ya Jahannam, na watu watapita juu yake, na kasi zao zitakuwa kiasi cha ‘amali zao. Wapo watakaopita kama umeme, na wengine kama upepo, na wengine kama ndege, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa juu yake huku akisema: "Ya rabbi Sallim sallim" (Allaah Salimisha Salimisha)

 

 

Na tunaamini kila kilichokuja katika mafundisho ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Siku hiyo pamoja na vitisho vyake - Tunamuomba Allaah Atusaidie.

 

 

 

Jannah Na Moto

 

 

Na tunaamini juu ya Jannah na Moto, na kwamba Jannah ni nyumba ya neema Aliyowaandalia Allaah waja wake wema wamchao. Ndani yake mna yale ambayo macho hayajapata kuyaona, wala masikio kuyasikia wala halijapata kumpitikia mtu yeyote nafsini mwake.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنِ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ 

Basi nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [As-Sajdah:17]

 

 

Na Moto ni nyumba ya adhabu Aliyoitayarisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa ajili ya makafiri madhalimu. Ndani yake mna kila aina ya adhabu ambazo hazijapata kumpitikia mtu yeyote nafsini mwake.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلظَّالِمِينَ نَارًا أَحَاطَ بِهِمْ سُرَادِقُهَا ۚ وَإِن يَسْتَغِيثُوا يُغَاثُوا بِمَاءٍ كَالْمُهْلِ يَشْوِي الْوُجُوهَ ۚ بِئْسَ الشَّرَابُ وَسَاءَتْ مُرْتَفَقًا ﴿٢٩﴾

Hakika Sisi Tumewaandalia madhalimu moto ambao kuta zake zitawazunguka. Na wakiomba uokozi watapewa maji kama masazo ya zebaki nyeusi ziliyoyeyushwa yanayobabua nyuso. Ubaya ulioje kinywaji hicho, na uovu ulioje mahali pa kupumzikia.  [Al-Kahf: 29]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ اللَّـهَ لَعَنَ الْكَافِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمْ سَعِيرًا ﴿٦٤﴾ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَّا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿٦٥﴾ يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّـهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا ﴿٦٦﴾

 

Hakika Allaah Amewalaani makafiri, na Amewaandalia moto uliowashwa vikali mno. Ni wenye kudumu humo abadi. Hawatopata mlinzi na wala mwenye kunusuru. Siku zitakapopinduliwa nyuso zao motoni, watasema: Laiti tungelimtii Allaah, na tungelimtii Rasuli. [Al-Ahzaab: 64- 66]

 

 

 

Maswali Ya Kaburini

 

 

Na tunaamini juu ya mtihani wa kaburini, wakati mtu atakapoulizwa nani Rabb wake na ipi Dini yake na yupi Rasuli wake.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ﴿٢٧﴾

Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah Anafanya Atakavyo. [Ibraahiym: 27]

 

 

Na tunaamini juu ya neema za kaburini.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾

Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema watasema: “Salaamun ‘Alaykum, (amani iwe juu yenu) ingieni Jannah kwa yale mliyokuwa mkitenda.” [An-Nahl: 32]

 

 

 

Adhabu Ya Kaburini

 

 

Na tunaamini juu ya adhabu ya kaburini kwa madhalimu na makafiri.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٩٣﴾

Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti, na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na mlikuwa mkitakabari kuhusu Aayaat Zake. [Al-An’aam: 93]

 

 

Katika mlango huu zipo Hadiyth nyingi zilizo sahihi, na kila Muislamu anatakiwa aamini yote yaliyomo ndani ya Qur-aan na ndani ya Sunnah (Mafundisho ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yanayohusu mambo ya ghaibu na wala asiyakatae kwa sababu hayalingani na mambo yanayotendeka duniani, kwani ya Aakhirah hayakisiwi na haya ya duniani kutokana na hitilafu kubwa sana iliyopo baina ya mawili hayo -  Wa-Allaahul-Musta’aan.

 

 

 

 

Qadar

 

 

Tunaamini juu ya Qadar (kudra – majaliwa - yale yaliyokwisha andikwa) kheri yake na shari yake kuwa yote yamekwisha andikwa na yote yanatokana na Allaah na kwamba kisha waqadiria waja wake kwa elimu yake iliyokienea kila kitu.

Na Qadar imegawika sehemu nne.

 

 

1. Ujuzi:  Tunaamini kuwa Allaah ni Mjuzi wa kila kitu, Anajua kilichotokea na kitakachotokea na namna inavyotokea, na hii inatokana na elimu yake isiyo na mwanzo wala mwisho ilichokienea kila kitu. Hakitokei kipya ikawa Allaah Hakuwa na elimu nacho, na tunaamini kuwa Allaah hasahau.

 

 

2.  Maandishi: Tunaamini kuwa Allaah Ameandika katika ubao wa Lawh al-Mahfuudh yote yaliyotokea na yatakayotokea mpaka siku ya Qiyaamah.

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٧٠﴾

Je, hujui kwamba Allaah Anajua yale yote yaliyomo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yamo katika Kitabu. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi. [Al-Hajj: 70]

 

 

3.    Kutaka: Tunaamini kuwa Allaah Ametaka kiwepo kila kilicho mbinguni na ardhini, kwani hakiwezi kuwepo kitu chochote bila Yeye kutaka kiwepo. Anachokitaka kinakuwa na Asichokitaka hakiwi.

 

 

4.    Kuumba: Tunaamini kuwa Allaah ndiye Aliyeumba kila kitu.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ﴿٦٢﴾

Allaah ni Muumbaji wa kila kitu, Naye juu ya kila kitu ni Mdhamini. [Az-Zumar: 62]

 

 

 

Kutaka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

Na sehemu hii ya tatu imekusanya kutaka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kutaka kwa viumbe Vyake, kwa sababu Allaah Anakijuwa kila kinachotendwa na waja Wake, na kwamba Yeye mwenyewe Ametaka kiwepo, ama sivyo kisingewezekana kutendeka.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ ﴿٢٨﴾ وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٩﴾

 

Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke (katika haki) Na hamtotaka isipokuwa Atake Allaah Rabb wa walimwengu. [At-Takwiyr: 27 – 28]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿٢٥٣﴾

Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Ayatakayo. [Al-Baqarah: 253]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١١٢﴾

Na lau Angetaka Rabb wako wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga. [Al-An’aam: 112]

 

 

Lakini juu ya yote hayo, tunaamini pia kuwa Allaah Amempa mwanaadamu uhuru wa kuamua na Akampa uwezo wa kutenda. Na ufuatao ni ushahidi kuwa mwanaadamu amepewa uwezo huo.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ ۚ

Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. Na kadimisheni (mema) kwa ajili ya nafsi zenu.  [Al-BaqaraH; 223]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَوْ أَرَادُوا الْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا لَهُ عُدَّةً

Na ingelikuwa wametaka kutoka, bila shaka wangeliandaa maandalizi yake [ At-Tawbah: 46]

 

 

Kwa hivyo Allaah Amempa mwanaadamu uwezo wa kutaka, kuamua na wa kwenda atakapo na kujiandalia atakavyo.

 

 

Pili, kule kuamrishwa kufanya mema na kukatazwa kufanya mabaya ni dalili kuwa mwanaadamu anao uwezo wa kufanya atakalo, maana kama asingekuwa na uwezo huo kule kukatazwa na kuamrishwa kusingekuwa na maana yoyote.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ    

Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.  [Al-Baqarah: 286]

 

 

Tatu, Allaah Anamsifia Atendaye mema kwa wema wake, na Anamlaumu atendaye ovu kwa ovu lake. Mwanaadamu asingekuwa na uwezo wa kutenda atakalo basi pasingekuwa na haja ya kumsifia mwema wala kumlaumu muovu kwa sababu huko ni kumpa mtu sifa asiyoistahiki.

 

 

Nne, Allaah Ameleta Rusuli.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٦٥﴾

Rusuli ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa) Rusuli. Na Allaah daima ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [An-Nisaa: 165]

 

 

 

Yangelikuwa matendo ya watu hayafanyiki kwa uwezo wao na uchaguzi wao, hoja yao isingebatilika kwa kuletewa Rusuli.

 

 

Tano, kila mtu anapotenda jambo huhisi kuwa ametenda au ameacha kutenda. Utamuona anaposimama, anapokaa, anapoingia, anapotoka, anaposafiri, anapolala. Anapotenda lolote katika haya hufanya kama anavyotaka na wala hahisi kama yupo yeyote anayemlazimisha kufanya hayo, bali anaiona tofauti iliyopo anapofanya jambo kwa hiari yake mwenywe na anapolazimishwa, na hata shari’ah inatofautisha pale mtu anapofanya jambo kwa hiari yake na anapolazimishwa wakati Allaah Hamuhesabii kuwa ametenda kosa mtu anayefanya jambo kwa kulazimishwa.

 

 

Wakati huo huo anayefanya maasi kwa hiari yake huyo anahesabiwa kama ni mkosa, kwa sababu amechagua kufanya hayo kwa hiari yake mwenyewe bila kuelewa kuwa Allaah Keshamuandikia. Kwa hivyo hapana anayejua nini alichoandikiwa ila baada ya kutenda.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ 

“Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho [Luqmaan: 34].

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ ﴿١٤٨﴾

Watasema wale walioshirikisha: Lau Allaah Angetaka, tusingelifanya shirki, wala baba zetu pia na wala tusingeliharamisha chochote. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao mpaka walipoonja adhabu Yetu.  Sema: Je, mna elimu yoyote mtutolee? Hamfuati isipokuwa dhana tu, nanyi si lolote ila mnabuni uongo. [Al-An’aam: 148]

 

 

Kwa hivyo tunamuambia mwenye kufanya maasi; 'Kwa nini usitende mema huku ukitegemea kuwa Allaah ndiye Alokuandikia uyatende? Kwa sababu hapana tofauti kwako baina ya mema na maovu kwa vile hujui nini ulichoandikiwa kabla ya kukitenda.'

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowaambia Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum);  "Kila mmoja keshaandikiwa makao yake ya Jannah (Peponi) na ya Motoni." Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wakamuuliza: "Si bora tuache kufanya ‘amali na tuyategemee tuliyokwishaandikiwa?" Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia: "Hapana! Bali fanyeni, kwani kila mtu amewepesishiwa yale ambayo kwa ajili yake ameumbiwa."

 

 

Na tunamuuliza mwenye kutenda maasi: 'Kwa mfano wewe unasafiri kwa gari kuelekea Makkah, ukakuta mbele yako njia mbili, mtu mkweli akakuambia kuwa ukipita njia ya mwanzo utakutana na vitisho vingi na utapambana na tabu, ama njia ya pili ni nyepesi na haina matatizo yoyote. Bila shaka utapita njia ya pili, na haiwezekani ukapita ya mwanzo ukasema; 'Nishaandikiwa', na kama utafanya hivyo, watu watakuona mwendawazimu.

 

 

Mfano mwengine; Ukifanikiwa kupata kazi mbili, mojawapo ina mshahara mkubwa sana na nyengine mshahara mdogo, ukaambiwa uchague, bila shaka utachagua ile yenye mshahara mkubwa. Basi vipi unajichagulia nafsi yako katika ‘amali za Aakhirah zile zilizo duni kisha unasema kuwa 'Hivi ndivyo nilivyokadiriwa (nishaandikiwa)?

 

 

Unapoumwa kwa mfano, utawatafuta madaktari bora na utakubali kustahamili kupigwa sindano zenye kuuma au kufanyiwa operesheni na kustahamili kunywa dawa chungu, unafanya yote hayo ili upate kupona. Kwa nini basi huachi kujitibia na kusema; 'Nishaandikiwa?'

 

 

 

 

Baadhi Ya Faida

 

 

‘Aqiydah (Itikadi) hii tukufu yenye mizizi mitukufu ina matunda mengi yenye faida nyingi ndani yake, na zifuatazo ni baadhi tu ya faida hizo:

 

 

Imani ya kumuamini Allaah na majina Yake na sifa Zake vinaongeza mapenzi yetu kwa Allaah na kumtukuza. Mambo ambayo kupatikana kwake kunasababisha kuzidisha hima ya kuisimamia dini na kujiepusha na makatazo ya Allaah na kufuata maamrisho Yake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa ajili ya kupata furaha ya duniani na ya Aakhirah.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾

Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, Tutamhuisha uhai mzuri, na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.  [An-Nahl 16: 97].

 

 

 

 

Matunda Ya Kuamini Malaika

 

 

Kwanza:  Tunapata kujua utukufu wa Aliyewaumba (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kuzijua nguvu Zake na Ufalme wake.

 

 

Pili:    Kumshukuru Allaah kwa kuwalinda waja Wake, kwani Malaika hawa wamo miongoni mwao wenye kazi ya kuwalinda Waislamu na kuandika ‘amali zao n.k.

 

 

Tatu; Kuwapenda Malaika kwa kumuabudu kwao Allaah kwa ukamilifu, na kwa kuwaombea kwao maghfira Waislamu.

 

 

 

 

Matunda Ya Kuviamini Vitabu

 

 

Kwanza: Tanapata kuielewa rehma ya Allaah juu ya waja Wake, kwa vile Amewateremshia Kitabu kila umati kwa ajili ya kuwaongoza.

 

Pili: Tunaiona hekima ya Allaah Aliyeweka ndani ya Vitabu hivi shari’ah zenye kunasibiana na kila umati, na akakifanya Kitabu cha mwisho kuwa Qur-aan tukufu ili kiwe kwa umati wote uliobaki katika zama zote na wakati wote mpaka Siku ya Qiyaamah.

 

Tatu: Tunapata kumshukuru Allaah kwa neema Yake hiyo.

 

 

 

 

Matunda Ya Kuamini Rusuli

 

Kwanza: Tunaijua rehma ya Allaah kwa waja wake Aliyewapelekea Rusuli kwa ajili ya kuwaongoza.

 

 

Pili: Tunapata kumshukuru Allaah kwa neema Yake hiyo.

 

Tatu: Kuwapenda Rusuli (na Manabii) na kuwaheshimu na kuwapa sifa wanazozistahiki, kwani wao ni Rusuli wa Allaah waliochaguliwa miongoni mwa watu wote, wakamuabudu Allaah kama Anavyostahiki kuabudiwa, wakaifanya kazi ya kuwalingania watu huku wakisubiri na kustahamili udhia.

 

 

 

 

Matunda Ya Kuiamini Siku Ya Qiyaamah

 

 

Kwanza: Kumtii Allaah kwa kutegemea kupata thawabu zitakazokufaa Siku ya Qiyaamah, na kuepukana na kufanya madhambi kwa kuihofia adhabu ya Siku hiyo.

 

 

Pili: Kumliwaza Muislamu kwa yale anayoyakosa katika neema za hapa duniani na anasa zake, akitegemea neema na anasa za Siku ya Aakhirah.

 

 

 

Matunda Ya Kuamini Qadar

 

 

Kwanza: Kumtegemea Allaah katika kila jambo, kwa vile vyote ni kwa uwezo Wake Allaah.

 

 

Pili: Starehe ya nafsi na utulivu wa moyo, maana mtu anapotambua kuwa hapana kinachoweza kutokea bila Allaah kutaka, moyo hutulia na nafsi huingiwa na matumaini akaridhika na kile alichomuandikia Rabb wake. Na hapana mtu anayeishi maisha mazuri na mwenye nafsi iliyotulia kupita yule mwenye kuamini juu ya Qadar.

 

 

Tatu: Kuondoa majisifu pale mtu anapofanikiwa kupata analolitaka, kwani kupata chochote ni neema itokayo kwa Allaah na kwa kuwa keshaandikiwa (keshajaaliwa) mtu huyo kuyapata mafaniko yale au kheri ile, kwa hivyo mtu huyo anatakiwa amshukuru Allaah badala ya kujisifu.

 

 

Nne; Kuondosha hofu na uoga pale mtu anapokikosa anachokitaka au anapopata msiba kwani yote hayo yanatokana na Allaah.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٢٢﴾

Hausibu msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla hatujautokezesha. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi. [Al-Hadiyd: 22]

 

 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuthibitishe katika ‘Aqiydah (Itikadi) hii na Atuonjeshe matunda yake na atuongezee katika fadhila Zake na asizipoteze nyoyo zetu baada ya kuziongoza, na atumiminie rehma kutoka Kwake kwani Yeye ndiye Mpaji.

 

 

WalhamduliLlaahi Rabbil ‘Aalamiyn – Rabb wetu, Mswalie  Nabiy wako Muhammad pamoja na Swahaba wake na ‘Aali zake wema, na kila atakayemfuata kwa wema na uongofu mpaka Siku ya Qiyaamah. Aamiyn.

 

 

 

 

Share