Saladi Ya Orzo Ya Kigiriki (Greek Orzo Salad)
Saladi Ya Orzo Ya Kigiriki (Greek Orzo Salad)
Vipimo:
Orzo (makaroni madogo dogo kama picha) - 2 Vikombe/200gms
Tango - 1
Nyanya - 1
Pilipili Tamu La kijani - 1
Pilipili Tamu La manjano - 1
Pilipili Tamu La jekundu - 1
Pilipili Tamu La orenji (rangi ya orange) - 1
Zaituni za kijani - ½ kikombe
Zaituni nyeusi - ½ kikombe
Kitunguu chekundu - 1
Kitunguu cha majani (spring onions) - 3 miche (bunch)
Parsley (aina ya kotmiri) - 3 miche (bunch)
Jibini ya feta (feta cheese) au jibini nyeupe (cottage cheese) - 200 gms
Oregano - ¼ kijiko
Nanaa(mint leaves) - 2 misongo
Chachadu Ya Saladi (Salad Dressing)
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe
Siki ya zabibu au yoyote - 2 vijiko vya supu
Mafuta za zaituun (olive oil) - ¼ kikombe
Chumvi - kiasi
Pilipili nyekundu ya unga - ½ kijiko cha chai
Namna ya Kutayarisha Na Kupika:
- Chemsha orzo kama ilivyo maelezo katika paketi yake. Usiivishe kupindukia mpaka uliowekwa zikawa laini sana. Chuja maji utie katika bakuli la saladi.
- Katakata tango, nyanya, mapilipili yote ya mboga, kitunguu vipande vidogo vidogo, tia katika bakuli la orzo.
- Katakata (chop) parsely na nanaa, vitunguu vya majani tia katika bakuli la orzo.
- Tia zaituni zote, oregano, katakata jibini uchanganye vyote pamoja katika bakuli. Funika vizuri
- Wakati tayari kuliwa nyunyizia chachadu ya saladi ikiwa tayari kuliwa kwa kitoweo upendacho.
Namna ya kutengeneza Chachadu (Dressing ya saladi)
- Changanya vitu vyote katika mashine ya kusagia (blender) usage.
- Wakati wa kupakua au karibu na kupakua ndio umimine juu ya saladi na uchanganye vizuri na saladi.
Kidokezo:
Unaweza kufanya nusu yake ikiwa ni watu kidogo.