Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah

 

Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Nimepitia website yenu nzuri Maa shaa Allaah, Allaah awazidishie na kazi hiyo nzuri. Tafadhali kuhusu suala la Rukyah, tafadhali nitumie utaratibu kamili, yaani ayas na sura za rukyah zote na utaribu wa kuzisoma hizo sura. Pia nielimishe vipi nitajiyarisha ninapo jisomea rukyah, yaani kuhusu udhu, mavazi na kadhalika. Shukran

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Katika mas-ala ya Ruqyah zipo Aayah za kusomwa na mtu mwenyewe za kutaka kinga kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa) na zipo zile za kumsomea mtu aliyekumbwa na jini au kufanyiwa sihri.

 

Ama njia ya kujikinga mwenyewe ni kuwa uwe unasoma Aayah zifuatazo asubuhi na jioni. Nazo ni kama zifuatazo:

 

  1. Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
  2. Al-Baqarah (Aayah nne za mwanzo, Ayatul Kursiy na Aayah mbili baada yake na Aayah tatu za mwisho).
  3. Aal-‘Imraan (3: 1 – 2).
  4. Suratut Tawbah (9: 129 mara saba).
  5. Al-Israa’ (17: 110 – 111).
  6. Al-Mu’minuun (23: 115 – 118).
  7. Al-Hashr (59: 22 – 24).
  8. Al-Kaafiruun (109).
  9. Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas (mara tatu tatu).

 

Ama kipengele cha pili cha kumsomea mwengine inafaa usome Aayah zifuatazo:

Mwanzo unaanza na A’udhu Billaahi minash Shaytwaanir Rajiym.

  1. Al-Faatihah (Suwrah ya kwanza).
  2. Al-Baqarah (aayah 1 – 5, 102, 163 – 164, 255, 285 - 286).
  3. Aal-‘Imraan (3: 18 – 19).
  4. Suwrah Al-A‘raf (7: 54 – 56, 117 - 122).
  5. Yunus (10: 81 – 82).
  6. Twaaha (20: 69).
  7. Al-Hajj (22: 19 – 22).
  8. Al-Mu’minuun (23: 115 – 118).
  9. An-Naml (27: 30 – 31).
  10.  Asw-Swaaffaat (37: 1 – 10).
  11.  Ad-Dukhkhaan (44: 43 – 48).
  12.  Al-Ahqaaf (46: 29 – 32).
  13.  Al-Fath (48: 29).
  14.  Ar-Rahmaan (55: 33 – 36).
  15.  Al-Hashr (59: 21- 24).
  16.  Al-Jinn (72: 1 – 9,
  17.  Al-Buruuj (85).
  18.  Zilzalah (99).
  19.  Al-Humazah (104).
  20.  Al-Ikhlaasw, Al-Falaq na An-Naas.

Ama unapokuwa unasoma unafaa uwe twahara (nguo na mwili) na umejisitiri kwa kujifunika vizuri sehemu zipasazo kusitiriwa na pia usome kwa unyenyekvu.

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share