Amali Za Kuwatendea Wazazi Waliofariki Waendelee Kupokea Thawabu

 

‘Amali Za Kuwatendea Wazazi Waliofariki Waendelee Kupokea Thawabu

 

 Alhidaaya.com

 

 

‘Amali za mwana Aadam zinakatika baada ya kufariki kwake isipokuwa matatu kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 ((إذا مات إبن آدم إنقطع عمله إلا من ثلاث: صدقة جارية  أو علم ينتفع به أو ولدٌ صالح يدعوا له))  مسلم

((Anapokufa mja, hukatika amali zake zote isipokuwa mambo matatu, swadaqah inayoendelea, au elimu yenye kunufaikiwa, au mtoto mwema anayemuombea)) [Muslim]

 

Lakini Muislamu anaweza kuendelea kuwatendea wema wazazi wake wawili kwa ‘amali nyenginezo ambazo zimethibiti kuwa thawabu zake zinawafikia kama ifuatavyo:

 

 

1-Kuwaombea du’aa na kuwaombea maghfirah:

 

 عن أبي أسيد مالك بن ربيعة رضي الله عنه قال:  بينا نحن جلوس عند رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا جاءه رجل من بني سلمة فقال يا رسول الله هل بقي من بر أبوي شيء أبرهما به بعد موتهما ؟ قال: ((نعم! الصلاة عليهما والاستغفار لهما وإنفاذ عهدهما من بعدهما وصلة الرحم التي لا توصل إلا بهما وإكرام صديقهما)) رواه ابن حبان في صحيحه  أبو داود وابن ماجه

Kutoka kwa Abuu Asyad Maalik bin Rabiy’ah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Tulipokuwa tumekaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi   wa aalihi wa sallam) alikuja mtu kutoka [kabila la] Bani Salamah akasema: Ee Rasuli Allaah, je, kuna kilichobakia katika wema ninaoweza kuwafanyia wazazi wangu baada ya kifo chao? Akasema:  ((Naam! Kuwaombea du’aa, kuwaombea maghfirah, kuwalipa deni zao, na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao, na kuwakirimu rafiki zao)) [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake, Abu Daawuwd na Ibn Maajah]

 

 

Kuwaombea Maghfirah Ni Kupandishwa Kwao Daraja Ya  Jannah (Peponi):

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْه ِ وَ سَلَّمَ: ((إِنَّ الرَّجُلَ لَتُرْفَعُ دَرَجَتُهُ فِي الْجَنَّةِ فَيَقُولُ : أَنَّى هَذَا ؟ فَيُقَالُ :باسْتِغْفَارِ وَلَدِكَ لَكَ)) لإمام أحمد  و في سنن ابن ماجة أيضاً بإسنادٍ صحيح  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mtu hupandishwa daraja yake Jannah (Peponi). Kisha huuliza: Kwa ajili ya nini? [huku kupandishwa kwangu daraja?] Huambiwa: Kwa ajili ya kuombewa maghfirah na mtoto wako)) [Ahmad, na katika Sunan Ibn Maajah ikiwa na isnaad Swahiyh]

 

Miongoni mwa du’aa za kuwaombea ni zilizotajwa katika kauli za Allaah ('Azza wa Jalla)

 

 رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾

Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni. [Al-Israa: 24]

 

 

 رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾

Rabb wetu! Nighufurie na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu. [Ibraahiym: 41]

 

Katika Sunnah wanaposaliwa Swalaah ya Janaazah:

 

Maiti mwanamume:

 

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُ وَارْحَمْـه، وَعافِهِ وَاعْفُ عَنْـه، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـه، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَه، وَاغْسِلْـهُ بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِ مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِه،  وَأَدْخِـلْهُ الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُ مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

Eee Allaah, Mghufurie na Mrehemu, na Muafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Mpanulie kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Jannah (Peponi) na Mkinge na adhabu ya kaburi na adhabu ya moto.

 

Maiti mwanamke:

 

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُا وَارْحَمْـها، وَعافِهاِ وَاعْفُ عَنْـها، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـها، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَها، وَاغْسِلْـهُا بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِا مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُا داراً خَـيْراً مِنْ دارِها، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـها، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِها،  وَأَدْخِـلْهُا الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُا مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

 

Kuwaombea Wazazi Wawili:

 

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُما وَارْحَمْـهما، وَعافِهِما وَاعْفُ عَنْـهما، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـهما، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَهما، وَاغْسِلْـهُما بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِما مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُما داراً خَـيْراً مِنْ دارِهما، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـهما، وأَزَوْاجَـاً خَـيْراً مِنْ اَزْوَاجِهِما  وَأَدْخِـلْهُما الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُما مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

 

 

 

2. Kuwalipia Deni La Swawm:

 

Kuwalipia deni la Swawm ikiwa ni la fardhi (Ramadhwaan) au Swawm ya nadhiri au ya kafara. Ama ikiwa amefariki kabla ya kumalizika Ramadhwaan na amewahi kufunga siku za nyuma, hakuna haja kumlipia:

 

عن ابن عباس رضي الله عنهما ، قال :جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه و سلم فقال : يا رسول الله إن أمي ماتت، و عليها صوم شهر أفأقضيه عنها ؟ قال : (( لو كان على أمك دين أكنت قاضيه عنها ؟)) قال : نعم. قال: (( فدين الله أحق أن يُقضى)) البخاري و مسلم

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Ee Rasuli wa Allaah,  Mama yangu amefariki naye ameacha  deni la mwezi la Swawm, je nimlipie? Akasema: ((Je angelikuwa mama yako ana deni [la fedha] ungelimlipia?)) Akajibu:  Ndio. Akasema ((Basi deni la Allaah lina haki zaidi ya kulipwa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na pia:

 

عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قال رسول الله صلى الله عليه و سلّم: ((من مات و عليه صيامٌ صام عنه وليُّه)) البخاري و مسلم 

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aliyefariki akiwa na [deni la] Swawm, walii wake amfungie)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

3-Kuwafanyia Hajj Ikiwa Hawakufanya Au Kuwafanyia ‘Umrah: 

 

عن ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما أَنَّ امْرَأَةً جَاءَتْ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، فَقَالَتْ : إِنَّ أُمِّي نَذَرَتْ أَنْ تَحُجَّ ، فَمَاتَتْ قَبْلَ أَنْ تَحُجَّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ ، حُجِّي عَنْهَا أَرَأَيْتِ لَوْ كَانَ عَلَى أُمِّكِ دَيْنٌ أَكُنْتِ قَاضِيَتَهُ ؟ )) قَالَتْ : نَعَمْ . فَقَالَ : ((اقْضُوا اللَّهَ الَّذِي لَهُ ، فَإِنَّ اللَّهَ أَحَقُّ بِالْوَفَاءِ ))   رواه البخاري    

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Alikuja mwanamke kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Nina mama ambaye aliweka nadhiri kuwa atahiji, akafariki kabla ya kuhiji, je nimhijie? Akasema: ((Ndio, mhijie je ingelikuwa mama yako ana deni ungelimlipia?)) Akasema: Ndio. Akasema: ((Mkidhieni Allaah (deni) Lake, kwani Allaah Ana Haki zaidi kutimiziwa)) [Al-Bukhaariy]

 

Pia:

 

عن عَبْد اللَّهِ بْن بُرَيْدَةَ عَنْ أَبِيهِ رَضِي اللَّه عَنْهما ، قَالَ : بَيْنَما أَنَا جَالِسٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، إِذْ أَتَتْهُ امْرَأَةٌ ، فَقَالَتْ:   إِنِّي تَصَدَّقْتُ عَلَى أُمِّي بِجَارِيَةٍ ، وَ إِنَّهَا مَاتَتْ . فَقَالَ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : (( وَجَبَ أَجْرُكِ وَ رَدَّهَا عَلَيْكِ الْمِيرَاثُ)) قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ كَانَ عَلَيْهَا صَوْمُ شَهْرٍ أفأصُومُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((صُومِي عَنْهَا)) قَالَتْ : إِنَّهَا لَمْ تَحُجَّ قَطُّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا؟ قَالَ: ((حُجِّي عَنْهَا)) مسلم

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah kutoka kwa baba yake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Nilipokuwa nimekaa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja mwanamke akasema: Nimemtolea mama yangu swadaqah ya kijakazi. Naye amefariki. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Umewajibika kupata ujira na mirathi itakurudia)). Akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, alikuwa ana deni la mwezi la Swawm, je nimfungie?” Akasema: ((Mfungie)). Akasema: “Yeye hakuwahi kuhiji, je nimhijie?” Akasema: ((Mhijie)) [Muslim]

 

 

4-Kuwatolea Swadaqah:

 

عن أمّ المؤمنين عَائِشَةَ رَضِي اللَّه عَنْهَا ، أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أُمِّي افْتُلِتَتْ نَفْسُهَا ( أي ماتت فجأةً ) وَ أَظُنُّهَا لَوْ تَكَلَّمَتْ تَصَدَّقَتْ ، فَهَلْ لَهَا أَجْرٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ)) البخاري

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Mama yangu imesokoteka nafsi yake [kwa maana amefariki ghafla] na nadhani kama alizungumza kutaka kutoa swadaqah. Je, atapata ujira nikimtolea swadaqah?” Akasema: ((Ndio)) [Al-Bukhaariy]

 

Pia

 

 عن ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِي اللَّه عَنْهمَا ، أَنَّ سَعدَ بْنَ عُبَادَةَ رَضِي اللَّه عَنْهما تُوُفِّيَتْ أُمُّهُ وَ هُوَ غَائِبٌ عَنْهَا فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أُمِّي تُوُفِّيَتْ وَ أَنَا غَائِبٌ عَنْهَا أَيَنْفَعُهَا شَيْءٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ بِهِ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ )) قَالَ: فَإِنِّي أُشْهِدُكَ أَنَّ حَائِطِيَ الْمِخْرَافَ ( اسم لبستان كان له) صَدَقَة ٌ عَلَيْهَا .-  البخاري

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Sa’ad bin ‘Ubaadah (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) alifiwa na mama yake naye alikuwa hayupo akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, Mama yangu amefariki nami sikuweko. Je, itamfaa lolote nikimtolea swadaqah?”  Akasema: ((Ndio)) Akasema: “Basi nashuhudia kwako kwamba ukuta wangu wa al-Mikhraaf [jina la bustani yake] ni swadaqah kwa ajili yake.” [Al-Bukhaariy]

 

Pia,

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أَبِي مَاتَ ، وَ تَرَكَ مَالاً وَ لَمْ يُوصِ ، فَهَلْ يُكَفِّرُ عَنْهُ أَنْ أَتَصَدَّقَ عَنْهُ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ))   روى مسلم و ابن ماجة و النسائي

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Baba yangu amefariki na ameacha mali wala hakuiusia. Je, itakuwa kafara yake (atapata ujira na malipo) nikimtolea swadaqah kwayo?” Akasema: ((Ndio)) [Muslim, Ibn Maajah na an-Nasaaiy

 

 

5-Kuunga Ukoo Ambao Hauungiki Ila Kutokana Na Wao:

 

Dalili ni Hadiyth iliyotangulia katika nukta ya kwanza ambayo imetaja:

((na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao))

 

Ni kuwasiliana na ndugu, jamaa wenye uhusiano wa damu, wa karibu na wa mbali, mfano ‘ammu (kaka wa baba) ‘ammat (shangazi), khaal (kaka wa mama), khaalat (mama mdogo au mkubwa), watoto wao wote, bibi wa baba, bibi wa mama na wanaouhusiana wote kwa damu kwa kila upande.

 

Tutamube kwamba kuunga undugu wa uhusiano wa damu ni kitendo ambacho kimesisitizwa sana. Dalili zake zinapatikana katika Qur-aan na Sunnah kwamba mwenye kukataa kuunga undugu amelaaniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), rizki yake itadhikika, umri wake utapunguka, Allaah ('Azza wa Jalla) Atamkatilia mbali na hatoingia Jannah (Peponi).

 

 

   

6-Kuwakirimu Rafiki Zao

 

عن عبد الله بن دينار عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما أن رجلا من الأعراب لقيه بطريق مكة فسلم عليه عبد الله بن عمر وحمله على حمار كان يركبه وأعطاه عمامة كانت على رأسه . قال ابن دينار : فقلنا أصلحك الله إنهم الأعراب وهم يرضون باليسير , فقال عبد الله بن عمر إن أبا هذا كان ودا لعمر بن الخطاب وإني سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: (( وإن أبر البر صلة الولد أهل ود أبيه )) مسلم

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Diynaar na kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba bedui mmoja alikutana naye njiani akielekea Makkah, akamsalimia ‘Abdullaah bin ‘Umar kisha akampakia juu ya punda aliyekuwa amempanda akavua kilemba chake na kumpa. Akasema Ibn Diynaar: Tukasema: “Allaah Akuwekee vizuri. Hao ni mabedui nao  wanaridhika na kichache.”  ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: “Baba yake huyu alikuwa mpenzi wa ‘Umar ibnul Khattwwaab [Baba yangu] nami nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Kitendo chema kabisa ni mtoto kumpenda (kuungana na) rafiki wa baba)) [Muslim]

 

Na pia:

 

عن أبي بردة قال: قدمت المدينة فأتاني عبد الله بن عمر فقال أتدري لم أتيتك ؟ قال قلت لا . قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:  ((من أحب أن يصل أباه في قبره فليصل إخوان أبيه)) وأنه كان بين أبي عمر وبين أبيك إخاء وود فأحببت أن أصل ذاك   -  ابن حبان في صحيحه

Pia kutoka kwa Abuu Bardah ambaye amesema: Nilikuwa naelekea Madiynah akanijia ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: “Je, unajua kwa nini nimekujia?” Akasema: Nikasema: “Hapana!” Akasema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Anayependa kuungana na baba yake katika kaburi lake basi awasiliane na ndugu zake (rafiki zake) baba yake)) Na baina ya baba yangu ‘Umar na baba yako walikuwa na undugu wa mapenzi, basi nimependa kuwaunga.”   [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]

 

 

 

Share