Wudhuu Unatenguka Ukimuosha Mtoto Mchanga?

 

Wudhuu Unatenguka Ukimuosha Mtoto Mchanga?

SWAL LA KWANZA:

A.alk ndugu zangu katika uislamu. Ningependa kujua kama wudhuu utatenguka kwa kumsafisha mtoto mchanga anapoingia chooni. Je, itanipasa kutia wudhuu tena ama kuosha mkono tu? Shukran, wajazakatul-llahukheyra.

SWALI LA PILI:

 a.a.m ndugu zangu wa alhidaaya. Nimefurahi sana kupata majibu kulingana na swali niliowauliza mbelini na nimefahamu kila kitu nawapa shukran tena ALLAH awazidishie elmu na imani nyingi kuweza kutusaidia sisi ndugu zenu wa kiislam. Swali langu la leo ni kuwa mtu akiwa na udhu kisha akamtamba mwanawe huwa ametangua udhu au la nitafurahi sana kupata majibu yangu kwa email yangu shukran.

 

Maasalam

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza kabla hatujajibu maswali hayo, tunakukumbusha kuwa unapoandika  Salaam hazifai kufupishwa kwa kuandikwa (A.A) au (A.A.W.W.) au kama ulivyoandika kwani haijafundishwa hivyo na pia ni kujikosesha fadhila za Salaam kama tulivyoelezwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo nayo tujizoeshe kuandika (Assalaamu ‘alaykum) au (Assalaamu ‘alaykum wa rahmatullaah) au (Assalaamu ‘alaykum wa Rahmatullaah wa Barakaatuh) kwa ukamilifu na tutakuwa tumeiga mafunzo ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na pia tutakuwa tumezoa thawabu zote za Salaam kama tulivyofundishwa. Na Mafunzo yote na fadhila zake zimo Alhidaaya katika kiungo kifuatacho: Maamkizi Ya Kiislamu.  

Pia hiyo shukurani ya muulizaji wa kwanza: wajazakatul-llahukheyra.sivyo ipasavyo kutamkwa, bali ni kusema “Jazaaka Allaahu Khayra” au ‘Jazaakumu Allahu Khayra”  

 

Kuhusu swali hilo la kumuosha mtoto mchanga Uislamu kwa kutazama maslahi ya wafuasi wake imewaondolea mashaka kwa kutomlazimisha mwanamme au mwanamke mwenye kufanya hivyo. Kwa hiyo, hakuna haja ya kuchukua wudhuu pindi unapomsafisha mtoto na ukawa umegusa uchi wake. Hii imeafikiana na kauli ya Maalik, az-Zuhriy na al-Awzaa‘iy. Utaosha tu mikono yako na sehemu zilizogusa najisi.

Kama tulivyotangulia kusema ni kuwa kumchambisha mtoto mchanga hakutengui wudhuu) na huko ni kupatiwa wepesi na usahali Muislamu. Uislamu umeletwa na Allaah Aliyetukuka ili kuondosha uzito wote uliokuwa katika sheria zilizopita

(Taz. Swahiyh Fiqhus Sunnah cha Abu Maalik kilichopo ndani ya ALHIDAAYA katika kiungo kifuatacho:

Yasiyotengua Wudhuu

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share