Kusoma Halal Badiri au Albadiri (Ahlul-Badr) Kwa Ajili Ya Kinga Na Kuapiza
SW
Assalama alikum warahmatullah taala wabarakatu.
Napenda kuanza kwa kumshukuru Mola mlezi wa ulimwengu kwa kuwapa nguvu, afya na uwezo ndugu zetu wa alhidaaya kwa kutuelimisha sisi ndugu zenu Waislam katika musuala mengi yanayohusu dini yetu ya haki. Mola awape kheir, baraka na pepo inshaalah. Ameen.
Na suali langu ni kutaka kujua
Asanteni....assalam aleykum.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Halali Badiri. Awali twataka kurekebisha ibara hiyo kwani haina maana yoyote. Ibara hiyo imetoka katika lugha ya Kiarabu lakini kupotolewa au kuandikwa na kusomwa makosa katika Kiswahili. Wapo wanaosema Alibadiri lakini inafaa iwe Ahlul Badr, yenye maana watu wa Badr (wale waliopigana vita vya Badr). Badr ni sehemu iliyo karibu na Madiynah na ndio iliyokuwa sehemu ambayo Waislamu wakiongozwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walipambana na mushirikina wa Makkah katika vita vya kwanza baina ya pande hizo mbili. Waislamu waliohudhuria walikuwa baina ya 313 – 317, lakini pamoja na idadi
Kisomo cha Ahlul Badri inakuwa ni kutaja majina ya Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) mmoja baada ya mwingine. Katika kutaja huko ni Imani ya mwenye kusoma hao Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wanamsaidia kwa njia moja au nyingine. Ima kupata kitu alichopoteza au kilichoibiwa au kulaaniwa aliyefanya. Na hii katika Uislamu ni njia moja ya shirki ambayo Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameikema na kuipiga vita
“Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya
Ingia Katika Kiungo Kifuatacho pia upate maelezo yam as-ala haya:
Wazazi Wangu Wako Kwenye Maasi,Ushirikina Wa Waganga Na Albadiri (Ahlul-Badr)
Ikiwa unataka kinga basi kinga ni nyingi
Utakipata kitabu hicho ndani ya Alhidaaya kwenye kiungo hiki:
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
