Ee Mwana-Aadam! Nini Kikudanganyacho?

Ee Mwana-Aadam! Nini Kikudanganyacho?

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  

 

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾

  Ee mwana Aadam! Nini kilichokughuri kuhusu Rabb wako Mkarimu? [Al-Infitwaar: 6]

 

 

  • Utukufu ulioje wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa Kauli Zake kama hii yenye kushtua nyoyo na kusisimua mwili!

 

  • Siku utakayoitwa "Ee Mwana-Aadam, uliye maskini, uliye dhaifu, kitu gani kikudanganyacho?"

 

  • Nini kilichokughilibu hata ukamu'asi Allaah ('Azza wa Jalla)?   

 

  • Nini kilichokudanganya hata ukavuka mipaka ya Rabb wako?

 

  • Nini kilichokudanganya hata ukapuuza Swalaah?

 

  • Nini kilichokudanganya hata ukatenda maovu mchana na usiku?

 

  • Nini kilichokudanganya hata ukapeleka macho yako kutazama yalio haraam?

 

  • Nini kilichokudanganya hata ukawa humuogopi Rabb wako bali unaoogopa  viumbe?

 

  • Nini kilichokudanganya hata ukawa huna khofu ya kukutana na Rabb wako na kuhesabiwa?

 

Je, ni dunia? Je, hujui kama dunia ni nyumba ya kupita tu? Au ni matamanio?  Je, hujui kuwa matamanio ya hii dunia ya kutoweka?  Au ni Shaytwaan aliyekuhadaa? Kwani hujui kama yeye kwako ni adui mkubwa?  Basi ni kipi kilichokudanganya? Zingatia leo ndugu Muislamu kabla ya kusubiri kesho kwani hakuna dhamana kuwa utafika kesho. Amesema    Mshairi:

 

تزود من التقوى فإنك لا تدري   ****    إذا جن عليك ليل هل تعيش إلى الفجر

Zidisha taqwa kwani hujui

Usiku utakapokufunika, je, utaishi hadi Alfajiri?

 

 

 

 

فكم من صحيح مات بغير علة  ***  وكم من سقيم عاش حينا من الدهري

Kwani wangapi waliokuwa na siha zao wamekufa bila ya maradhi

Na wangapi walio wagonjwa wameishi miaka?

 

 

 

وكم من صغار يرتجى طولة عمرهم  ***  وقد دخلت أجسادهم ظلمة القبر

Na wangapi miongoni mwa wadogo wametumainiwa maisha marefu

Na miili yao imekwishaingia katika kiza cha kaburi

 

 

 

 

فكم من فتى يمسي ويصبح ضاحكا  ***   وقد نسجت أكفانه وهو لايدري

Na vijana wangapi wameamka huku wanacheka

Kumbe huku sanda yao inashonwa (inaandaliwa) naye hajui

 

 

 

وكم من عروس زينوها لزوجها  ***  وقد قبضت أرواحهم ليلة القدر

Na bi harusi wangapi amepambwa kwa ajili ya mume wake

Na roho zao zimechukuliwa usiku wa Laylatul-Qadri?

 

 

 

وكم من ساكن عند الصباح بقصره  ***  وعند المساء قد كان من ساكن القبر

Na wangapi asubuhi walikuwa katika maqasri yao wakikaa

 Na jioni yakawa makazi yao ni kaburi?

 

 

 

فكن مخلصا وأعمل الخير دائما   ***  لعلك تحظى بالمثوبة والأجر

Kuwa mwenye ikhlaas na utende mema daima

Huenda ukawafikishwa kupata thawabu na jazaa

 

 

 

وداوم على تقوى الإله فإنها أمان   ***   من الأهوال في موقف الحشر

Na dumisha Taqwa ya Mola Wa Pekee kwani ni hifadhi

Itakayokulinda na hali katika siku ya kukufuliwa

 

 

 

 

Basi ndugu Muislamu, kumbuka madhambi yako na amka usiku ujikuribishe kwa Rabb wako  Mwenye kughufuria na kusamehe madhambi, na Mwenye Rahmah na rudia kuisoma hii Aayah mara kwa mara ili ikuguse moyoni:

 

 

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾

 Ee mwana Aadam! Nini kilichokughuri kuhusu Rabb wako Mkarimu? [Al-Infitwaar: 6]

 

Na pia zingatia Aayah zinazofuatia katika  Suwrah hiyo tukufu inayotaja matukio ya Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo    hutoweza kujisaidia wala kusaidiwa!

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾

1. Mbingu zitakapopasuka.

 

وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ ﴿٢﴾

2. Na sayari zitakapoanguka na kutawanyika.

 

وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ ﴿٣﴾

3. Na bahari zitakapolipuka.

 

وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾

4. Na makaburi yatakapopinduliwa chini juu na kufichuliwa.

 

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾

5. Nafsi itajua yale iliyoyakadimisha na iliyoyaakhirisha.

 

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾

6. Ee mwana Aadam! Nini kilichokughuri kuhusu Rabb wako Mkarimu?

 

الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾

7. Ambaye Amekuumba Akakusawazisha (umbo sura, viungo) na Akakupima na kukulinganisha sawa.

 

فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ ﴿٨﴾

8. Katika sura Aliyotaka Akakutengeneza.

 

كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ ﴿٩﴾

9. Laa hasha! Bali mnakadhibisha malipo.

 

 

وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ﴿١٠﴾

10. Na hakika juu yenu bila shaka kuna wenye kuhifadhi (na kuchunga).  

 

 

كِرَامًا كَاتِبِينَ ﴿١١﴾

11. Watukufu wanaoandika (amali).

 

 

يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾

12. Wanajua yale myafanyayo.

 

 

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿١٣﴾

13. Hakika Waumini watendao mema kwa wingi bila shaka watakuwa katika neema (taanasa, furaha n.k).

 

 

وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ ﴿١٤﴾

14. Na hakika watendao dhambi bila shaka watakuwa katika moto uwakao vikali mno.

 

 

يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ ﴿١٥﴾

15. Watauingia waungue Siku ya malipo.

 

 

 

وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ ﴿١٦﴾

16. Nao hawatokosa kuweko humo.

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٧﴾

17. Na nini kitakachokujulisha Siku ya malipo?

 

 

ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٨﴾

18. Kisha nini kitakachokujulisha Siku ya malipo?

 

 

يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًاۖ وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّـهِ ﴿١٩﴾

19. Siku ambayo nafsi haitokuwa na uwezo wowote juu ya nafsi nyingine; na amri Siku hiyo ni ya Allaah Pekee.

 

 

[Al-Infitwaar (82)]  

 

 

 

Share