Ameacha Mke, Watoto Wa Kike Wawili, Ndugu Wa Kike Watatu

SWALI:

 

ASALAM ALEYKUM. Aliyefariki ameacha watoto wa kike wawili, mjane, ndugu wa kiume mmoja, na ndugu wa kike wa tatu. Je, asilimia ngapi kila mtu atapata?

 

 


JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mirathi ya baba aliyeaga. Muulizaji hakututajia kama aliyefariki aliacha wazazi wote wawili au mmoja hivyo tunachukulia kuwa hakuacha.

 

Katika hilo hakika ni kuwa mjane aliyebaki anapata fungu lake maalumu, nalo ni thumuni (1/8) kwa sababu ya aliyefariki kuwa na watoto. Allaah Aliyetukuka Anasema:

Na wake zenu watapata robo mlichokiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu yao ni thumuni ya mlichokiacha, baada ya wasia mliousia au kulipa deni” (4: 12).

Na mabinti kwa kuwa wao ni wawili watapata kila mmoja thuluthi (1/3).

 

Ama ndugu wa aliyefariki watarithi kwa sababu ya kutowepo watoto waaliyefariki wa kiume.

 

 

Jadwali ya wirathi itakuwa kama ifuatavyo:

 

 

Namba

Uhusiano na Aliyefariki

Kiwango

Asilimia

1

Mjane

Thumuni (1/8)

12.5

2

Binti 1

Thuluthi (1/3)

33.33

3

Binti 2

Thuluthi (1/3)

33.33

4

Kaka

 

8.34

5

Dada 1

 

4.17

6

Dada 2

 

4.17

7

Dada 3

 

4.17

 

Jumla

 

100.01

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share