Mchuzi Wa Mumunye (Zuchini) Na Viazi

Vipimo
Zucchini 3
Viazi 2
Kitunguu 1
Nyanya 2
Nyanya kopo 2 vijiko vya supu
Pilipili manga kidogo
Pilipili mbichi 2
Kidonge cha supu (stock) 1
Ndimu Nusu
Mafuta 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katakata mamumunya (zucchini) vipande vya duara, viazi vipande vya kiasi, nyanya, na kata kitunguu vidogo vidogo (chopped).
- Tia mafuta katika sufuria, kaanga viitunguu hadi viigeuge rangi kidogo tu.
- Tia nyanya endelea kukaanga hadi ziwive, tia nyanya kopo
- Katia pilipili mbichi, tia pilipilimanga, chumvi .
- Tia maji kiasi, viazi, tia kidonge cha supu, funika weka moto mdogo acha hadi karibu viazi kuwiva, tia mamumunya.
- Bakisha kidogo motoni uwivishe mamumunya kidogo tu .
- Kamulia ndimu na tayari kuliwa kwa wali au mikate yoyote upendayo.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


