Sharbati Ya Maziwa Na Lozi

Sharbati Ya Maziwa Na Lozi

 

Vipimo

Juisi ya barafu (frozen juice)

yoyote upendayo - 1 Pakitti

Maziwa - 3 gilasi

Sukari - Kiasi

Lozi - ¼ Kikombe

Strobberri - Kiasi ya kupambia

 

Namna Ya Kutayarisha

  1. Katika mashine ya kusagia (blender) tia Juisi ya barafu, maziwa, lozi na sukari kisha saga hadi ichanganyike vizuri.
  2. Ikiwa nzito sana unaweza kuongeza barafu ukipenda.
  3. Mimina katika gilasi, pambia strobberri na itakuwa tayari.
Share