'Aaishah (رضي الله عنها): Ndoa Changa Ya Mama Wa Waumini -5

Imetafsiriwa na Naaswir Haamid

 

 

MAAMUZI NI YEPI SASA?

 

Sio rahisi mtu kujizuia kufuata tamaduni nyengine au kukubali ya kwamba yeye ni kizabzabina (misimamo miwili kwa wakati mmoja). Kwa watu wengine inachukua muda wa miaka kukubali ya kwamba wamekuwa ni wanafiki. Mategemeo ni kwamba, mawazo yaliyowasilishwa humu yatachipua mizizi mingi kwa baadhi ya watu ili waone ukweli. Kawaida ni nusu ya shari kukubali ya kwamba kuna tatizo, kwa hivyo kabla ya msomaji kukimbilia kufanya maamuzi ya wapi anasimama katika suala hili, ninahitaji kutoa mawazo zaidi.

 

Msomi wa zamani wa masuala ya Uislamu, Montgomery Watt, alikuwa na maneno muhimu kwa watu wa Magharibi wanavyotakiwa kumhukumu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Daima nimekuwa napingana na maamuzi ya Watt kuhusu (anavyouchora) Uislamu, lakini nimemuweka kuwa ni mtu mmoja ambaye ni mtaalamu wa elimu ya Mashariki aliyekuwa wazi na mwenye kufungua moyo wake. Bila ya shaka, hii ni kwa sababu alikuwa ni mshajiishaji zaidi wa kuelewa kuliko mtu aliyejifunga kwenye mishionari ya Kikristo. Watt alifikia maamuzi yafuatayo baada ya miaka ya masomo kwenye Uislamu:

 

“Tuhuma nyengine kuu yenye kumshushia heshima Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kwamba alikuwa mdanganyifu na mwenye tamaa nyingi. Mengi yamesemwa kuhusiana na fafanuzi ya matokeo haya kuonesha kwamba tuhuma dhidi ya Muhammad ni nyepesi kuliko inavyofikiriwa kwa baadhi ya wakati. Majadiliano ya tuhuma hizi, hata hivyo, yanaibua suala kuu. Ni namna gani tumhukumu Muhammad? Je ni kwa viwango vya wakati wake na nchi yake? Au kwa maoni ya sasa ya watu wa Magharibi walio wepesi? Pale vyanzo vinavyochujwa vizuri, ni wazi kwamba yale matendo ya Muhammad yasiyokubaliwa na watu wa Magharibi wa kisasa, yalikuwa sio kiini cha lawama za kukiuka maadili kwa wakati wa kipindi chake.

 

Walilaumu baadhi ya vitendo vyake, lakini msukumo wao zaidi ulikuwa ni mambo ya kishirikina au khofu ya athari ya vitendo hivyo. Kama walilaumu matokeo ya Nakhlah, ilikuwa ni kwa sababu waliogopa baadhi ya adhabu kutokana na miungu ya kipagani au kuwalipizia kisasi watu wa Makkah.

 

Kama walistaajabishwa na mauaji mabaya ya Wayahudi kwa wingi wa kabila la Qurayzah, ilikuwa ni kutokana na kiwango cha hatari cha kumwaga damu ya watumwa inayoweza kumwagwa. Ndoa pamoja na Zaynab inaonekana kuwa ni ya uzinzi baina ya maharimu, lakini dhana hii ya uzinzi ilitokana na mazoea ya kale yanayotokana na hadhi duni ya kijamii kwenye matawi ya kiukoo ambapo asili ya upande wa baba wa mtoto haukujulikana kwa uhakika; na hadhi hii duni ilizuiliwa na Uislamu...

 

Kwa mujibu wa msimamo wa wakati wa Muhammad, bila ya shaka, tuhuma za udanganyifu na matakwa ya kimwili hayakupatiwa nafasi. Maisha yake hayakumuona kuwa ni mpungufu wa adabu kwa namna yoyote. Kwa kulinganisha, baadhi ya vitendo vinavyolaumiwa na watu wa Magharibi wa kisasa, vinaonesha kwamba hadhi ya Muhammad ilikuwa juu zaidi kuliko kipindi ilivyo wakati wake.

 

Alikuwa ni mwenye kuleta mabadiliko ya kijamii kwa wakati wake na kizazi chake, alikuwa pia ni mwenye kufanya mabadiliko ndani ya tamaduni. Alianzisha mfumo mpya wa hifadhi ya jamii na muundo mpya wa ukoo, ambapo zote mbili zilikuwa ni hatua kubwa mojawapo ya maendeleo kulingana na kulivyokuwa huko nyuma. Kwa kuangalia lipi bora ndani ya tamaduni za watu wanaohamahama (wasio na makazi ya kudumu) na kuzitumia kwa jamii zilizotulia kimakaazi, alianzisha muundo wa kijamii wa mwanzo kwa ajili ya maisha ya watu wengi walio na makabila tofauti. Hiyo sio kazi ya msaliti au ‘kizee kisicho na adabu’.”[1]

 

 

KUTOKA IBRAAHIYM HADI “DINI YA KUDONOA-NA-KUCHAGUA/ KUJISKIA VIZURI”

 

 

Yote tuliyozungumzua hapo juu yanamuweka huru Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutokana na lawama zisizo adilifu ambazo amezipata (hata kwa wale waliokuwa na elimu wenye mawazo yasiolenga upande wowote). Hata hivyo, kitu kimoja kinahitaji kuwekwa wazi kidogo. Ingawa tumekitaja hapo nyuma, lakini bado kinahitaji kuchambuliwa na kubainishwa, ni kuhusu unafiki na viwango maradufu vya Wakristo ambao wanamlaumu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu ya maadili yake.

 

Kabla ya kupiga hatua mbele katika kuchambua Maadili ya Kibiblia, nitapendelea kuwapatia mawazo fulani na maneno ya hamasa kwa Waislamu wenzangu. Kikubwa ninachohitaji kuwapatia maoni ni kutovunjika moyo kutokana na maneno ya tashtiti yanayotolewa juu ya Uislamu au vile ambavyo unavyovunjiwa heshima ndani ya vyombo vya habari. Bila ya shaka sote tunakereka kuona mambo kama hayo, lakini ndani ya “Zama za Habari” “Information Age” zilizoletwa na tamaduni ambazo (zinadai) kutilia mkazo mno uhuru wa kuzungumza, hakuna kubwa tunaloweza (kufanya) kuizuia hali hiyo. Ghafla (tukigeuza) upande wa pili wa sarafu hii, ni sahihi kwamba Ukweli kuhusu Uislamu upo huko nje na watu wanaendelea kuutafuta. Ndio, Uislamu unaenea hata kwa vikwazo vya kinafiki ambavyo Wakristo na wengineo wanavitumia kuuzuia.

 

Kuanzia uongo wa “mungu wa mwezi” wa Robert Morey hadi uharibifu wa kila siku ndani ya vyombo vya habari, Uislamu bado unakua ndani ya Magharibi. Hakika ukweli ni kwamba, wale wanaofanya uharibifu wa Uislamu kuwa ndio kazi yao, kwa mfano mishionari za Kikristo, ni lazima warudie mara kwa mara kwenye uongo na uharibifu pale wanapojadili kwamba Uislamu ni alama nzuri. Bila ya shaka, kama watajadili namna ambavyo inahitaji kueleweka, watajiumiza kwa walichokianzisha wao wenyewe. Uislamu unapowasilishwa na wasiokuwa Waislamu ndani ya Magharibi, ni yale mambo muhimu yaliyo mepesi ndio kawaida yanazungumzwa na kulaumiwa. Msingi wa imani za Uislamu, kama zitajadiliwa, basi zinawasilishwa kwa njia ya kupotosha. Hawana haja ya kuufanya hivi Uislamu, kana kwamba ni Dini puuzi ya “Ulimwengu wa Tatu” isiyokuwa na haki ya kusikilizwa. Kutokana na hayo, ukweli ni kwamba, maandiko mengi dhidi ya Uislamu ambayo yanajazwa ndani ya maduka ya vitabu ya Wakristo (na ndani ya mtandao) hayana lengo la kuwabadili Dini Waislamu, bali kuwatupa watu wa Magharibi nje ya Uislamu (wasiuone kabisa).

 

 

Hata hivyo, njia zao zinaanguka. Haswa kwa Ulaya, Dini ya Kikristo ipo kwenye hali yake mbaya ya kuporomoka na watu wanautafuta ukweli kwengineko. Daima, Wakristo wamekashifika kutokana na kushindwa kumbadili Dini Muislamu mashuhuri (aliyebobea kielimu) kuingia katika Ukristo kikweli kweli. Bila ya shaka, wanao wartadi wao ambao wanawashikilia kama ni mfano, hata hivyo, wote wanaonesha kwamba walikuwa ni Waislamu wa kawaida (juu ya ubora wao) pale waliportadi. Hata hivyo, hivi karibuni na hata huko nyuma, watu wa Magharibi walio mashuhuri wameukubali Uislamu. Kitu kimoja kinachostaajabisha kuhusu hili ni wengi (kama sio wote) wanaweza kuitwa: “Watafutaji wa Ukweli” “Searchers for the Truth”.

 

 

Kwa hili, ninamaanisha kwamba walikuwa ni watu wenye roho, akili zilizo tayari kuelewa open-minded na wakisoma vitabu kwenye mada tofauti. Sio watu ambao ni wajinga na waliosafishwa akili brainwashed simpletons, ambao walitaka kuingia kwenye Dini nyepesi na iliyobeba utamaduni wa wakati huo. Walikuwa ni watu waliojua mambo mengi sio tu katika Dini, bali kuhusu historia, filosofia na nyanja nyenginezo. Inatosha kusema kwamba Ukweli wa Uislamu upo huko nje, juu ya kwamba hii leo unapokea matope kutoka kwenye vyombo vya habari.  Kiapo kifuatacho, ni mfano tu wa namna Uislamu unavyokuwa ndani ya Magharibi:

 

 

“Idadi isiyoeleweka ya Waingereza, takribani wote wakiwa ni wanawake, wanaingia kwenye Uislamu kwenye kipindi cha mgawanyiko mkubwa ndani ya makanisa ya Anglikana na Katoliki. Kiwango cha waliobadili kimepanda juu hadi kwamba Uislamu utakuja kuwa ni zana muhimu ya kidini ndani ya nchi hii. Ndani ya miaka 20 inayofuata, idadi ya Waingereza watakaobadili dini itakuwa sawa au itawazidi wahamiaji wa jamii ya Waislamu waliokuja nayo hapa imani hiyo”, anasema Rose Kendrick, mwalimu wa elimu ya dini katika ufahamu wa Hull na mwandishi wa kitabu cha muongozo wa Koran.

 

 

Anasema: “Uislamu ni zaidi ya imani ya ulimwengu mzima kama ambavyo ilivyo kwa Katoliki ya Roma. Hakuna utaifa unaodai kuwa ni ya kwake”. Uislamu pia unakuwa kwa haraka ndani ya bara (Ulaya) na Marekani. (The Times, London, Jumanne, Novemba ya 9, 1993, Home-News page).

 

 

Shukrani ziende kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwamba wengi wetu tuliokuwa wahamasishaji wa Kikanisa “pew warmers”, hatimaye tumeamua kwenda nje na kuchunguza yale wanayojaribu kutulisha kutoka kwenye mimbari na TV. Kwanini Uislamu umefanikiwa kuwavuta Wakristo na wengineo? Kwa sababu ndio Njia Sahihi ya Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam). Hivi leo, hakuna dini nyengine inayoweza kudai hili kwa uadilifu! Uislamu sio tu Dini ya “kujisikia vizuri” ambapo unaambiwa yale unayohitaji kusikia na kusoma Aayah za Biblia zilizochaguliwa. Wakristo wengi hivi leo wanaiendea dini kama vile wanavyofanya kwa chakula cha asubuhi cha Jumapili: wanachukua wanayopenda na kuacha wasiyopenda.

 

 

Ingawa ukweli ni kwamba Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) anatukuzwa ndani ya Biblia yao kama ni mfano wa juu wa imani, lakini bado wana tabia hii (ya unafiki). Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) ambaye alikuwa anakwenda kumtoa sadaka mwanawe kwa sababu Ameamrisha Mola Mtukufu, bila ya shaka alielewa msingi wa kimaadili. Ipo wazi ndani ya Biblia na Qur-aan kwamba Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) alielewa kuwa amri ya Mola Mlezi ni sahihi kuifanyia kazi. Hata hivyo, ni Wakristo wangapi hivi leo wanaweza kusema kidhati wanaamini kwamba ni hivyo kwa masuala yote? Ni wangapi wanaojaribu kuiga maadili ya sehemu iliyokuwemo ndani ya Biblia zao? Tunaona kwamba sio hata wasamehevu (mapadri, wachungaji) wao wanaoshambulia Uislamu wanaoiga hayo kwa ndani kabisa!

 

 

Suala la “Ni upi msingi wetu wa maadili?” ni jepesi kwa wale wanaofuata imani ya Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) – na hivyo ndivyo ulivyo Uislamu. Uislamu ni unyenyekevu mbele ya Uwezo wa Mola Mtukufu – “Tunasikia na Tunatii” – imani ya baba yetu Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam). Kama ni zuri kwa Ibraahiym, Muusa, ‘Iysaa na Muhammad (‘Alayhim swalaatuLlaahi was-salaamuhu ajma’iyn), basi ni zuri kwangu! Ni ukweli huu na tabia hii ambayo inawavuta watu kwenye Uislamu. Msingi mzima wa Uislamu, unaozalisha tabia hii, ni Umoja – Umoja wa Mola Mtukufu na umoja wa mwanaadamu. Ili kuwa na uhakika, ujumbe wa Uislamu unahimiza kwa kila asili ya mwanaadamu. Hukuna mshangao wa kwamba unaenea! Hivi karibuni, mwanafunzi mkristo wa elimu ya tabia na sifa za Mungu na dini ametambua:

 

 

“Inawezekana kwamba mwanzoni mwa karne ya ishirini na moja, Uislamu utakuja kuwa na idadi ya juu ya dini za duniani.”[2]

 

Hilo linawezekana, kama utahisabu Waislamu wa Kisunni tu (ambao sio chini ya asilimia 85 ya Waislamu), tushakuwa ni Dini ya juu kabisa katika ulimwengu inapolinganishwa na sio “Wakristo” kwa ujumla, bali, aidha kwa Wakristo wenye msimamo mkali Orthodox, Wakatoliki wa Roma Roman Catholics au Waprostanti Protestants, kila dhehebu (lihisabiwe) mbali mbali.

 

 

 

KISA NDANI YA MAADILI YA KIBIBLIA

 

 

Kwa kuwa sasa tumepata uoni wa kina kuhusiana na tuhuma za mashaka ya maadili katika maisha ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa mnasaba wa kuweka mizani sawa, tuangalie mashaka ya kimaadili ndani ya Biblia. Tumeshatoa matamko hapo juu kuhusiana na asili ya maadili ya Kibiblia, lakini wasomaji wengi wanaweza kuwa hawaelewi baadhi ya “mashaka yake”.  Kwa uzuri au ubaya, kawaida ndani ya shule za Jumapili huwa wanaziruka aya ambazo tutazijadili hapa chini.

 

Hata hivyo, aya hizi bila ya shaka ni zana muhimu kwa kuwaweka wataalamu wa Kikristo walio adilifu katika mezani moja ya “mashaka ya maadili” moral dilemma ambayo wanawadhania Waislamu kuwa nayo juu ya ndoa changa ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha). Ni bora ikawekwa akilini kwamba lengo la mjadala huu ni msingi wa kimaadili, sio kutia hamasa ya Biblia (au kukosoa). Kwa malengo ya mjadala huu, tunaikubali Biblia kama “ilivyo”. Hata hivyo, hili lisitafsiriwe ya kumaanisha kwamba tunalikubali “Neno la Mungu” bila ya pingamizi. Kwa upande mwengine, isitafsiriwe kumaanisha kwamba tunavamia “Neno la Mungu”, kwani tunaijadili kwa kuwa Wakristo wanaiamini kuwa ni “Neno la Mungu” (namna yoyote wanayoitafsiri wenyewe).

 

 

Kipande cha Biblia tunachohitaji kukiangalia kinaanza na Book of Numbers, Sura ya 31, aya ya 17 na 18. Hapa, baada ya kupata amri ya Mungu, Musa anawaamrisha wana wa Izraili kuwauwa watoto wa kiume (kutoka kabila la) Wamidiani[3]. Amri inaendelea kama ifuatavyo:

 

 

"…Kwa hiyo basi, waueni watoto wote wa kiume na kila mwanamke aliyewahi kulala na mwanamume. Lakini msiwaue wasichana wote ambao hawajapata kulala na mwanamume; waacheni hai kwa ajili yenu wenyewe”. 

 

 

Mtu anaweza kuagua namna Waizraili walivyotambua ni nani bikira. Kwa uhakika, walifanya hivi kwa kuangalia umri na kubalehe, wakidhani kwamba wanawake wote “watoto” waliokuwa hawajafika kubalehe ni bikira. Weka makini kwamba hili lilitendeka, kwa mujibu wa Biblia, kuhusu amri ya Mungu kwa “Avenge the Israelites on the Midianites” – “Lipizeni Kisasi Waizraili kwa Wamidiani”.

 

Baadaye, Mungu anampa Musa maelezo ya namna ya kugawa mateka nyara, “iwapo ni mtu, ng’ombe dume, punda, kondoo au mbuzi”. Kwa kuegemea kwenye amri hii, "thirty-two thousand persons in all, women who had not known a man by lying with him" waligaiwa. Hili lilifanyika ili kwamba maaskari wa Izraili wawapate wanawake hawa wachanga “kwa manufaa yao wenyewe”. Sitarajii kwamba mtu yeyote anayesoma hili anaona ugumu au ujinga kwa Mfalme James English kutotambua ni nini maana ya hili!

 

Tukisonga mbele kwenye mfano mkuu wa maadili ya Kibiblia...

 

Ndani ya Biblia; Deuteronomy 21:10-14 "Mapenzi ya Mungu" inatoa amri ifuatayo:

 

 

“Mkienda kupigana vita na adui, naye Mungu akawapeni ushindi mkawachukua mateka, kama mmoja wenu akiona miongoni mwa mateka mwanamke mzuri, ukamtamani na kutaka kumuoa, basi, wewe mwanamume mhusika utamchukua nyumbani, umnyoe kichwa chake na kukata kucha zake, na kubadili nguo zake za kifungoni. Atakaa muda wa mwezi mzima kumwomboleza baba yaka na mama yake. Kisha unaweza kumwoa, akawa mke wako nawe mume wake. Kama baadaye hapendezwi naye, utamwacha aende anakotaka; hutamwuza kupata fedha, wala usimtendee kama mtumwa kwa sababu umemnyenyekesha”. 

 

 

Ushahidi huu ni tosha kuonesha kwamba maadili ambayo yamefundishwa ndani ya Biblia, sio kawaida kwa Wakristo kuyatenda ingawa hayo yanafundishwa ndani ya Shule za Jumapili. Aya iliyotajwa hapo juu inafafanua yafuatayo:

 

Mungu Mtukufu, angalau kwa mujibu wa Biblia:

·         Aliamrisha watoto wasio na hatia kuuawa, na

·         Aliwaruhusu wanawake wachanga kulazimishwa kwenye vitendo vya ngono bila ya ridhaa yao.

 

 

Kabla ya kupiga hatua mbele, ieleweke kwamba kuua wanawake na watoto kwenye vita hairuhusiki hata kidogo ndani ya Shari’ah ya Kiislamu (matendo yanayofanywa na Waislamu wajinga duniani kote hayana uhalali). Baadhi ya Wakristo wanaweza kulichukulia jambo hili kwa maneno ya “watoto wasio na hatia” hapo juu, kwa vile wanaamini kwamba hata watoto wameambukizwa “Dhambi Halisi”.

 

 

Hata hivyo, mada hii sio ya kujadiliwa katika sehemu hii. Inatosha kusema ni mkanganyo mkubwa kwake Biblia kukubali Dhana ya Dhambi Halisi. Kuna baadhi ya aya ambazo zinaonesha kuikubali hio (Dhambi Halisi), lakini kuna baadhi ya nyengine ambazo zinaonesha wazi kuikataa.

 

 

Pigo moja dhidi ya “Dhambi Halisi”, tukiachilia nyuma ukweli kwamba sio haki hata kidogo, ni dhahiri kwamba Mayahudi – waliosoma Agano la Kale – hawakuiamini kwa namna wanavyoiamini Wakristo. Lakini hata hivyo  ... wanapokutana na sehemu zinazotatiza na Agano la Kale, Wakristo wanajibu kwa namna tofauti. Wengi wao wanakubaliana na fikra tetezi ya ugonjwa wa “Hiyo-Imo-Ndani-Ya-Agano-La-Kale

 

 

Juu ya ukweli kwamba hawapendelei kutumia hata kidogo Agano la Kale pale wanapooneshwa tuhuma za utume zinazofanana na Yesu, baadhi ya fikra nyengine zinaweza kuwasilishwa. Baadhi ya mambo yanayofanya vigumu kuitumia Agano la Kale (angalau kwa Wakristo waadilifu wanaohitaji kubakia na elimu yao) ni:

 

1.    Mungu huyo huyo “aliyelifungulia heri” Agano la Kale ndie “aliyefungulia heri” Agano Jipya;

2.    Mungu huyu huyu “asiyebadilika” kwa mujibu wa Biblia;

3.    Yesu ndani ya Agano Jipya ameikubali “Sheria na mitume” (yaani Agano la Kale) ndani ya sehemu tofauti; na

4.    Bila ya Agano la Kale hakuna msingi wa Ukristo.

 

Wanapowekwa ndani ya mashaka haya, Wakristo, wana chaguzi moja kati ya mbili:

 

1.    Kuacha kuifikiria na (badala yake) kuteleza kwenye usasa wa dini ya “kudonoa-na-kuchagua” inayowafanya “kujisikia vizuri” lakini isiyojibu matatizo sugu ya maisha yoyote; au

2.    Wakubali (tuhuma) maadili Yaliyoshushwa ya Kiungu ya Biblia “kama ilivyo” na bila ya gharama.

 

 

Kuna Wakristo huko nje wanaodai kukubali maadili Yaliyoshushwa ya Kiungu ya Biblia. Wanaelewa ni lipi lililo na umuhimu na suala lipi linalohitaji kutatuliwa. Kama watu wataruhusiwa kutoa uamuzi wa kimaajabu ajabu ni lipi sahihi na lipi kosa, kutakuwepo vurumai.

 

 

Ndivyo ilivyo umuhimu, kama watu wataamua nini “Neno la Mungu” na ni lipi sio neno Lake kwa kuegemea kwenye fikra zilizojikita huko kale za hisia za “usasa”, hakuna kitu kitakachobaki ndani ya Biblia. Kwani, kuna Wakristo, kwa mujibu wa kanuni, wanasema kwamba kuua watoto ni “maadili” kwani Mungu ameamrisha hilo wazi wazi.

 

 

Kwa mtu anayeelewa asili ya maadili Yaliyoshushwa ya Kiungu, itabidi tukubaliane naye kwa kanuni lakini mengine hatutoyakubali. Kama ilivyotajwa hapo juu, Mola Mtukufu – kwa mujibu wa Uislamu – Hajapatapo kuamrisha kuua watoto wasio na hatia. Hilo ni jambo moja “gumu” ambalo nina furaha kwamba Waislamu hawana haja ya kuelezea njia ya kutokea! Kuua watoto ni sawa alimuradi Mungu anaamrisha?!  Kuwa makini kuwaweka Wakristo kama ni walezi wa watoto! (baby-sitters).

 

Jambo muhimu ni kwamba maadili yanatokana na Mola Mlezi na ni kutokana na Kwake Yeye Pekee. Hata hivyo, kama mtu atasoma Biblia, ni wazi kuona kwamba (hilo) sio msingi wa maadili. Mifano ya hapo juu ni michache tu inayoweza kutolewa kutoka Agano la Kale na Jipya. Watu wanaohamasisha “Maadili ya Kibiblia” wanadonoa na kuchagua kutoka kwenye maandiko kama wanavyopenda.

 

 

Ni ndani ya Uislamu tu pekee, mtu mwenye akili timamu atakubaliana na “mfumo mzima” bila ya ujinga au unafiki wa kukataa vitu wasivyovipenda. Hivi ndivyo ukweli wa utulivu wa roho na mizani unavyofanikiwa. Kama mtu yupo kwenye Dini bila ya kukubali kila kitu ndani ya maandiko (yakiwa ni ya kweli au ya tuhuma), basi mtu hatokuwa tu shahidi wa kujiongopea yeye mwenyewe bali dhidi ya Mungu Mwenyewe.

 

 

Ni rahisi kupelekwa njia potofu kutokana na uongo ulioenea ndani ya zama za sasa. Ni mfano wa sokwe lililo na uzito wa paundi mia nane (kilo 362.88) kwa namna wanaharakati wa maadili ya Kimagharibi walivyogusa pembe zote za ulimwengu. Ni vigumu mno kumshinda nguvu au kuzungumza kwa kumpinga. Hata hivyo, imekuwa ni tatizo la kudumu kwa watu kuwashajiisha wengine kufuata “matashi ya kishetani”, kama Mola Mtukufu Anavyoweka wazi ndani ya Qur-aan:

 

{{Sema: “Mimi nimekatazwa kuwaabudu wale mnaowaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu (peke yake).” Sema: “Sifuati matamanio yangu, maana hapo nitapotea na sitakuwa miongoni mwa walioongoka.”}} [6: 56]

 

 

UJUMBE/UONGOZI TUNAOLAZIMIKA KUUSHUKURU

 

 

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mfano bora kwa wanaadamu wote na watu wa makabila tofauti (kuanzia Wazungu wa “kisasa” hadi Waasili wa Australia). Sio tu alikuwa ni Mtume bora na Mjumbe, bali alikuwa ni kiongozi wa taifa, amiri jeshi, mtawala, mwalimu, jirani na rafiki.

 

 

Mfano wake kwenye maisha ya kifamilia ndio nyanja muhimu kabisa, kwani alikuwa ni mume na baba kwa wakati mmoja. Kutokana na hekima za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), Mtume Wake wa mwisho alishuhudia mazingira tofauti ya kindoa na kifamilia. Kutokana na hili, yeye ni mfano kwa watu wenye ndoa moja, wenye ndoa zaidi ya moja, kwa wale wanaopendelea kuoa wakiwa wenye umri mkubwa zaidi yao na kwa wale wanaowaza ni mapema mno kwa mtu kuwa tayari kuoa. Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameirudisha tena Dini ya Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) ili ipate kuendelea hadi Siku ya Mwisho.

 

Kama (kweli) ni Waislamu, ni lazima tuwe na shukrani kwa miongozo (kama hii) kwenye msafara wetu wa maisha yaliyo na maadili. Kwa kuliangalia hilo, inatuzuia kutumbukia katika njia potofu ya “uhusiano wa kimaadili”. Hii ni hatari kubwa, kwani inaweza kupelekea kwenye madhambi makubwa – kumshirikisha pamoja na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwenye ‘ibaadah, imani na/au Ufalme. Kwa kuelewa maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), tunaweza kujichunga kukaa ndani ya mipaka iliyowekwa na Mola Mtukufu na kukaa kwenye Dini Asili ya Uislamu ambayo imefanywa kutosheleza maumbile (fitrah) ya mwanaadamu.

 

Ninaomba kwa Mola Mtukufu Atuchunge ndani ya mipaka yetu (ya Uislamu), na kwamba tusirubuniwe na jamii na tamaduni nyengine. Kama ni zuri kwa Ibraahiym na Muusa, basi ni zuri kwangu mimi pia...

 

Hivyo ndivyo nionavyo mimi, Allaah Anajua zaidi...

 

 

[1] W. Montgomery Watt, Muhammad: Prophet and Statesman - Muhammad: Nabii na Mtawala, Imechapishwa na Oxford University Press, 1961, uk. 229.

 

[2] John Hick, The Metaphor of God Incarnate, Imechapishwa na Westminster/John Knox, 1993, uk. 87.

 

[3] Kwa mujibu wa Biblia – Kitabu cha Genesis, Midiani alikuwa ni mtoto wa Ibrahimu aliyemzaa kutoka kwa mke wake wa mwisho aitwaye Ketura aliyemuoa baada ya kufariki mke wake wa pili Sara. Wajukuu wa Ibrahimu kupitia kwa mwanawe Midiani ambao ndio walizaa kizazi kinachoitwa Wamidiani ni; Efa, Efari, Enoki, Abida na Eldaa. Neno “Midiani” inawezekana limetokana na mzizi wa Kishemi lenye maana ya “hukumu” ambalo pia linamaanisha taifa la Wamidiani. Kwa mujibu wa historia kutoka Biblia, Midiani yasemekana pia kuwa ni sehemu aliyoishi Musa kwa miaka 40 baina ya alipokimbia Misri baada ya kumuua Mmisri aliyekuwa akimpiga Muizraili na baina ya kurudi kwake kuongoza Wanaizraili. Ndani ya kipindi hicho, Musa alimuoa Zipora, binti wa Yethro aliyekuwa padri wa Midiani. [Mfasiri]

 

 

Share