Vazi Lipi Lililo Bora Mbele Ya Allaah?
Bint Ahmadah
Amri kuu aliyopatiwa mwanamke wa Kiislamu inayomtofautisha na ndugu yake wa kiume ni ile inayosema: "Ewe Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane wasiudhiwe." (Suratul-Ahzaab: 59)
Vipi kuvaa nguo leo hii imekuwa viroja kwa Waislam? Kwani wamesahau mavazi
Kwani kuiga mavazi yaliyokuwa si yetu Waislam hayajatuhusu kabisa. Lakini kwa mtizamo wa leo ndio tunakwenda na wakati. Ati kuvaa nguo kwenye magoti ndio kustaarabika kwa ulimwengu wa leo, kumbe kinyume chake ni kupotoka kimaadili. Ustaarabu wa kweli tunaotakiwa kujinasibisha nao ni ule uliokuwepo zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘Anhum).
Wanawake katika zama hizo walikuwa ni wastaarabu wa maneno, vitendo na hata mavazi. Kwani akisimuliwa Bibi Faatwimah binti Rasuuli-Llaah vipi alivyokuwa mstaarabu si kwa watu wake tu, bali hata kwa ndugu zake wa kike pia anawagusa. Alijichunga ulimi wake, mwili wake, mpaka vitendo vyake hadi akawa mmoja kati ya wanawake bora duniani.
Pia tukitizama maana ya ustaarabu ni kuelimika kutokana na kitu fulani. Je wewe mwenzangu kuvaa mavazi yasiyostahiki mbele za watu ndio kustaarabika wakati dini yetu ya Kiislam imekwisha weka mavazi yanayotakiwa yavaliwe kwa mwanamke wa Kiislam. Elimu ya Qur-aan ndio ustaarabu wetu na tunalazimika kuitekeleza. Sio kuvaa kimini wala kijinzi. Je ikiwa wewe ni mama unavaa mavazi hayo mtoto naye avae vipi? Japo kuna baadhi
Aya za Mungu tunazigeuza tunavyotaka sisi kwa kujitupia kitandio kichwani ukiambiwa useme si ushajisitiri. Kuna wengine wakiwa hawana vyeo huvaa vizuri tu, wakipata vyeo ndio huvua hijabu mpaka inafika wakati hata ule wa kujitupia haukai kichwani. Kwa hiyo Mungu ulimjua ulipokuwa na dhiki, wakati wa raha Hajulikani. Umesahau kwa kupata 'chako' kwenye dunia hii 'nzuri' iliyojaa starehe hatimaye ukamsahau Mungu. Je huu ndio uungwana tuliofunzwa na Uislamu? Tunashindwa na paka au mbwa anayefugwa na mwanaadamu. Paka au mbwa aliyefunzwa na akafunzika wanapoamrishwa na bwana wake hakaidi. Hata kama paka akifunzwa kukataa kula samaki asiyepikwa hatakula na atakula aliyepikwa tu.
Lakini wewe dada yangu unasahau kwamba kuna mafunzo maalum ya Qur-aan uliyopatiwa kuyafuata na kwamba hapa ulimwenguni umeletwa kwa lengo la kumuabudu Mola Mlezi tu. Lakini leo wasema unakwenda na wakati. Ole wako kwa kuifanya dunia ni yako
"Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo; hivyo vyote vitaulizwa." (Suraatul-Israa: 36)
Ni juu yetu kina dada wenzangu kujikamata vilivyo kwenye mafunzo sahihi ya Uislam wetu. Tusione hayyaa kumrekebisha dada mwenzetu anayeporomoka kimaadili. Msimamo unahitajika kwenye kivazi hasa kwa wale wanawake wanaofanya kazi. Kibarua kisiwe ndio sababu ya kumuasi Mola Mlezi. Vazi la Uislam kwa mwanamke ndio heshima yake na yetu sote kwa ujumla. Shime tukamatane masikio dada zangu!
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



Asalaam Aleykum, Siku hizi
Asalaam Aleykum,
Siku hizi mbona tunashindwa kuchapisha hizi aticles? Tunaomba msaada wenu tuweze chapisha kwa maana wengine tunatumia kwa darasa kwa maana si wengi wenye mtandao.
Wabilah tawfiq!
Wa 'alaykumus-salaam wa
Wa 'alaykumus-salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh
Tuwe radhi kuchelewa kutatua tatizo hizo kutokana na kuzongwa na mengi ya hizi kazi.Tunapenda kukujulisha kwamba tumeshasawazisha na hivi sasa mtaweza kuchapisha makala zozote mtakazo.
Tunashukuru kujua kwamba hizi kazi mnafaidika nazo na kuwanufaisha wengine pia. Shukurani na Neema zote ni za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
Ndugu Zako
AL HIDAAYA