Skip to main content

Mkate Wa Mofa (Yemen)

Mkate Wa Mofa  (Yemen)

 

Vipimo

Unga wa mahindi - 1 mug

Unga wa mtama - 2 mugs

Kitunguu maji - 1 kikubwa

Chumvi - 1 kijiko cha chai

Sukari - 1 kijiko cha chakula

Hamira - 1 kijiko cha chai

Maji -  3 mugs

Namna Ya Kutayarisha Na  Kupika

  1. Upike unga wa mahindi kama uji kwa dakika kama tano na maji mug mbili.
  2. Uache upoe tia unga wa mtama na vitu vyote vilivyobaki pamoja na ile mug moja ya maji iliyobaki.
  3. Uache mpaka uumuke.
  4. Fanya maduara duara halafu tandaza uchome kwa moto mdogo kama chapati bila ya mafuta kwenye kikaango (frying pan). Choma mmoja mmoja yote hadi umalize..
  5. Iipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa na mchuzi wa nazi wa samaki au kuku au vyovyote upendavyo.