Mwenye Kufanya Maasi Ya Liwati Anaweza Kurudi Kwa Allah Kutubia?
SWALI:
Asalam Alaikum, mimi ninaishi ulaya na huku kuna wanaume wenye kulalana.
Swali langu ni je
JIBU
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
Shukurani kwa swali lako hili ambalo linaonyesha mwenye kufanya dhambi hizo anataka kurudi kwa Mola wake. Hakika ni jambo la kushukuriwa kwani wengi wamo katika maasi
Maasi yoyote yale yakiwa ni madogo au makubwa vipi, hata ikiwa ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hupokea tawbah ya mja Wake, wala mja asikate tamaa kabisa kwani Rahma Za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni nyingi na pana mno
((Sema: Enyi waja Wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na Rahma ya Allaah. Hakika Allah Husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu)) [Az-Zumar 39: 53].
Naye Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anampenda mja Wake aliyefanya dhambi kisha Akarudi kuomba tawbah. Hivyo basi linalokupasa ni haraka kukimbilia kufanya tawbah na baada ya hapo la muhimu ni kuwa ufuate masharti yake ambayo ni:
1-Kuacha maovu aliyokuwa anayafanya na kutenda vitendo vyema
kwa wingi
2-Kujuta Ayajutie makosa aliyoyafanya na kuazimia kutokurudia maasi hayo
3-Aazimie kutourejea tena uovu huo katika maisha yake.
Na endapo kosa
4-Ni kumuomba msamaha uliyemkosea kwa ulichomkosea ikiwa ni kuhusu haki za binaadamu
Hii ni fursa kwako kurudi kwa Mola wako haraka katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhaan ambao ni mwezi wa Rahma na Maghfirah. Hivyo basi kimbilia haraka kufanya tawbah na uazimie kuacha kabisa maasi haya na badala yake ufanye mema mengi.
Bonyeza kiungo kifuatacho upate makala muhimu kuhusu tawbah na uzifanye kazi ili utambue fadhila za tawbah na ubakie salama na maasi hayo:
Na Allaah Anajua zaidi