Kutahiriwa Ni Fardhi Au Sunnah?

SWALI

 

 

Assalamu Alaykum,
 
RAMADHAN KARIM
 
Hakika ndugu zangu jambo la kusikitisha kuwa niliuliza suali mbeleni kama ifuatavo :-Swali la KUTAHIRIWA ni FaARADHI au SUNNA

 


 

   

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kutahiriwa ni haki ya Kiislamu inayohusu fitrah kama tunavyopata maamrisho kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

 

 

 عن أبي هريرة رضي الله عنه، عن النبي   قال: (( الفطرة خمسة، أو خمس من الفطرة . الختان، والاستحداد، وتقليم الأظفار، ونتف الإبط، وقص الشارب))   متفق عليه السلام

 

 

 

Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema; ((Fitrah ni tano, au (vitu) vitano ni miongoni mwa Fitrah, Kutahiri (Circumcision), kunyoa (au kupunguza) nywele za sehemu ya siri (pubic hair), kukata kucha, kunyofoa (au kunyoa) nywele za kwapani, na kupunguza mashurubu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  

 

Pia asili yake ni kutoka kwa Baba yetu Nabii Ibraahiym ambaye tumeamrishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) tufuate mila zake:

 

  

 

((ثُمَّ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ أَنِ اتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفاً ))    

 

((Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibraahiym, mwongofu)) [An-Nahl: 123]

 

 

Dalili nyingine ni Hadiyth ifuatayo:

 

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) amesema: ((Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) ametahiriwa alipokuwa na umri wa miaka themanini  [Al-Bukhaariy]


Kwa hiyo kutahiriwa kwa wanaume wa Kiislamu ni jambo la fardhi. Lakini ikiwa kuna dharura fulani mfano kusababisha madhara kutokana na nasaha za daktari, basi ili asiathirike na madhara hayo fardhi hii huwa si lazima kwake na haitakuwa ni dhambi kwake.

 

Ama kwa mtu alnayetaka kusilimu, hilo si sharti kwake la kusilimu, ni vizuri akiweza kufanya hivyo kabla lakini asilazimishwe akaja kuukataa Uislam, na kisha baada ya kusilimu kwake hapo anatakiwa aelezwe umuhimu wa kutahiriwa na kuwa ni usafi na afya na pia ni alama muhimu ya Uislam.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share