Masanamu Ya Michezo Ya Watoto Yanafaa Kuwekwa Nyumbani?


SWALI:

1. Masananu ao toys tunazonunuliwa watoto wetu for their pleasure zina hatari gani kwetu hasa tunaposwali katika hayo majumba yetu at the same time hizo toys zipo elsewhere into our houses?

Naomba ufafanuzi zaidi kwani issu hii unadadisi zaidi

SWALI  LA PILI

1 JE, MADHARA GANI APATAYO MWANADAMU MWENYE KUDIRIKI SWALAH ZAKE NDANI YA NYUMBA AO SEHEMU YENYE KUWA NA TOYS?

2. TOYS ZA AINA GANI ZENYE KUHARIBU SWALAH NDANI YA NYUMBA NA ZIPI ZISIZOHARIBU?

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.

Kuweka masanamu katika nyumba bila ya sababu yoyote haifai kabisa kutokana na makatazo kutoka kwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa Malaika huwa hawaingii katika nyumba iliyo na sanamu:

 

قوله صلى الله عليه وسلم : ((أتاني جبريل عليه السلام، فقال لي: أتيتك البارحة، فلم يمنعني أن أكون دخلت إلا أنه كان على الباب تمثال [الرجال]، وكان في البيت قرام سترٍ فيه تماثيل، وكان في البيت كلب، فمر برأس التمثال الذي في البيت يقطع فيصير كهيئة الشجرة، ومُر بالستر فليقطع، فليجعل منه وسادتين توطآن، ومر بالكلب فليخرج فإنا لا ندخل بيتاً فيه صورة ولا كلب]))   حديث صحيح.

 

Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   amesema: ((Jibriyl 'alayhis-salaam  alinijia na akaniambia: Nilikujia jana usiku na hakuna kitu  kilichonizuia kuingia ndani ila kulikuwa na picha (binaadamu, yaani vinyago) katika mlango na pazia katika nyumba lililokuwa lina picha na kulikuweko na mbwa katika nyumba. Kwa hiyo kata kichwa cha picha mpaka kiwe kama ni mti tu, liendee pazia na lifanye mito miwili ya kuikalia na amrisha mbwa aondoshwe. Hakika sisi hatuingii nyumba ambazo zina picha au mbwa)) [Hadiyth sahiyh Abu Daawuud, An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy na wengineo]

 

 

Kupata maelezo zaidi ya makatazo ya picha na viumbe tafadhali soma jibu la swali katika kiungo kifuatacho:

 

 Hukmu Ya Kuchora Au Kupiga Picha Za Viumbe Vyenye Roho

 

Ama kuhusu michezo ya watoto, imeruhusiwa na Maulamaa wachezee michezo kama watoto wa sanamu n.k. kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo:  

 

   من حديث عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا ، قَالَتْكُنْتُ أَلْعَبُ بِالْبَنَاتِ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم ،َ وَكَانَ لِي صَوَاحِبُ يَلْعَبْنَ مَعِي ..  .  ) البخاري، مسلم)

Hadiyth kutoka bibi 'Aishah (Radhiya Allahu 'anhaa) ambaye amesema: "Nilikuwa nachezea watoto wa sanamu mbele ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nilikuwa na rafiki zangu ambao walikuwa wakicheza na mimi……."  [Al-Bukhaariy na Muslim]

Ibn Hajar amesema: Hadiyth hii inaonyesha kwamba inaruhusiwa kuwa na watoto wa sanamu kwa watoto wa kike. 

Imeruhusiwa hivyo ili wasichana wawe wanapocheza nao ni kama mazoezi na mafunzo kwao ya kama kujifanya mama kuwa wanalea watoto wao. 

Hadiyth nyingine inayotuonyesha kuwa imeruhusiwa ni kutoka kwa bibi 'Aishah vile vile ambaye amesema:

  " قَدِمَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ غَزْوَة تَبُوك أَوْ خَيْبَر " فَذَكَرَ الْحَدِيث فِي هَتْكه السِّتْر الَّذِي نَصَبَتْهُ عَلَى بَابهَا قَالَتْ : " فَكَشَفَ نَاحِيَة السِّتْر عَلَى بَنَات لِعَائِشَة لُعَب فَقَالَ:  ((مَا هَذَا يَا عَائِشَة)) , قَالَتْ : بَنَاتِي . قَالَتْ : وَرَأَى فِيهَا فَرَسًا مَرْبُوطًا لَهُ جَنَاحَانِ فَقَالَ : ((مَا هَذَا؟ )) قُلْت فَرَس. قَالَ:  ((فَرَس لَهُ جَنَاحَانِ؟ )) قُلْت : أَلَمْ تَسْمَع أَنَّهُ كَانَ لِسُلَيْمَان خَيْل لَهَا أَجْنِحَة ؟ فَضَحِكَ "          والرواية التي ذكرها ابن حجر عند أبي داود ، وصححها الألباني في غاية المرام 129  

 "Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alirudi katika vita vya Tabuuk au Khaybar……." Na akataja (ibn Hajar) Hadiyth kuhusu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipochana pazia ambalo lilikuwa lina picha ambalo bibi 'Aishah alilitundika mlangoni mwake. Akasema: Alifungua shubaka la pazia ambako kulikuwa na watoto wa sanamu aliokuwa akichezea 'Aishah, akasema: ((Nini hii ewe 'Aishah?)) Akasema: "Watoto wangu" (yaani watoto wa sanamu) Akasema: "Aliwaona kuwa wako pamoja na farasi ambaye alikuwa ana mbawa mbili zimeungwa naye, akasema: ((Nini hichi?)) Nikasema: "Farasi". Akasema: ((Farasi mwenye mbawa mbili?)). Nikasema: "Kwani hukusikia kuwa Sulaymaan alikuwa na farasi mwenye mbawa mbili?".  Akacheka (Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Imetajwa na ibn Hajar na imesimuliwa na Abu Daawuud na imepewa daraja ya sahiyh na Shaykh Al-Albaaniy katika Ghayaat Al-Maraam 129]

 

Kuzidi kupata maelezo kuhusu mas-ala haya tafadhali ingia katika kiungo kifuatacho:

Michezo Ya Watoto

Kama ilivyoulizwa katika Maswali haya, nukta inayotaka kufafanuliwa ni kuhusu michezo au vinavyoharibu Swalah katika nyumba navyo ni kama kuweka michezo ambayo imewekwa bila ya sababu ya kwa ajili ya watoto. Ama kuna masanamu ambayo hayampasi Muislamu kuyaweka nyumbani kwake kwa vile Malaika hawaingii katika nyumba hiyo. Na tunaona makosa haya yanafanyika sana katika nyumba za ndugu zetu wengi ambao huweka vinyago, au kutundika ukutani picha za viumbe kama mfano picha za harusi zao, na za watoto wao, na hapo hapo wengine huswali. Hakika hili jambo la muhimu kuepukana nalo ili ibada yake Muislamu ya Swalah ambayo ni fardhi anayoitimiza kila siku mara tano ipate ujira uliokamilika na Malaika waweze kuingia katika nyumba na kuwaingizia baraka katika nyumba zao.

Na wengi wetu huwa hatulioni kama jambo hili ni muhimu, bali huona ufakhari  kutundika picha za harusi au za watu tunaowaona ni maarufu hapa duniani kama marais, wacheza sinema, wacheza soka, waimbaji n.k. kuliko kujali makatazo ya dini kama hayo.

Ubaya mwingine ambao unatokana na kutundika picha ni kwamba mwanamke anaonekana picha yake na kila anayeingia katika nyumba hiyo ambao sio mahram wake.

Na Allah Anajua zaidi

 

 


Share