Skip to main content

Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani)

Biskuti - Cookiess

Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani)

Vipimo:

Unga  -   3 mug za chai

Samli  -  ½  mug ya chai

Maziwa - 1¼ mug ya chai

Baking powder -  2 vijiko vya chai

Mjazo

Njugu zilizomenywa vipande vipande - 2 vikombe cha chai

Sukari -  ½ kikombe cha chai

Iliki  - 1 kijiko cha chai

Nazi iliyokunwa  - 2  vikombe vya chai

Shira

Sukari  - 2  vikombe vya chai

Maji - 1  kikombe cha chai

Ndimu -  1 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1-Changanya unga na samli kisha tia baking powder na maziwa.  Ukande ulainike kisha

    uwache kama dakika 5 uumuke.

2-Kwenye bakuli nyingine changanya njugu, sukari na iliki.

3-Kata madonge madogo dogo  sukuma kila donge duara jembamba, kisha tia kijiko cha mchanganyiko wa njugu juu yake ifunikie juu yake na ibane pembeni kama inavyoonyesha katika picha.

       

 

4-Panga kwenye treya isiyoganda (non stick)  kisha choma kwenye oven   kwa moto wa chini

   (bake) 350° C kwa dakika kama 15-20.

5-Chemsha maji na sukari katika sufuria ndogo kisha tia ndimu acha ichemke mpaka inatenate unapoigusa.  

6-Kwenye sahani ya chali mimina nazi iliyokunwa.

7-Vibiskuti vikiwa tayari vya motomoto chovea kwenye shira kisha zungushia katika nazi iliyokunwa,

   panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Kidokezo:

Unaweza kutumia tende badala ya njugu.