Zakaatul-Fitwr: Anajitegemea Mwenyewe Anachangia Katika Futari Je, Anawajibika Zaatul-Fitwr?

Anajitegemea Mwenyewe, Anachangia Katika Futari; Je, Anawajibika Kutoa Zakaatul-Fitwr?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

salam alaykum.

Swali langu ni kwamba. Mimi nataka kutoa zaka ni msichana ninae jitegemea lakini nimekua nafturu kwa ndugu tofauti mwezi mzima. Na pia huko ninako enda kufuturu nachanigia kitu katika ftar. Je zakaah yangu niitoe vipi?

Waaleykum saam.

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himdi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu Swalaah na salamu zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kufuturu kwa watu au kuchangia futari haihusiani na hukmu ya kutoa Zakaatul-Fitwr kwani hikma ya kutoa Zakaatul-Fitwr ni kuitwaharisha Swawm ya mwenye kufunga kutokana na maneno maovu, machafu ambayo ameyatamka. Vile vile ili kuwapatia masikini nao chakula kizuri siku ya 'Iyd nao wafurahi. Dalili ifuatayo ni uthibitisho:    

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاس ٍقَالَ فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ طُهْرَةً لِلصَّائِمِ مِنْ اللَّغْوِ وَالرَّفَثِ وَطُعْمَةً لِلْمَسَاكِينِ مَنْ أَدَّاهَا قَبْلَ الصَّلاةِ فَهِيَ زَكَاةٌ مَقْبُولَةٌ وَمَنْ أَدَّاهَا بَعْدَ الصَّلاةِ فَهِيَ صَدَقَةٌ مِنْ الصَّدَقَاتِ . " رواه أبو داود  بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ .

 

Kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kuwa ni twahara ya mwenye kufunga kutokana na maneno ya upuuzi na machafu, na kulisha masikini. Atakayeitoa kabla ya Swalaah basi hiyo ni Zakaah iliyotakabaliwa, na atakayeitoa baada ya Swalaah basi hiyo ni Swadaqah miongoni mwa Swadaqah" [Abu Daawuwd kwa isnaad iliyo nzuri].

 

Kwa hiyo  ni waajib wako kuota Zakaatul-Fitwr maadam una uwezo na unajitegemea mwenyewe.

 

Kwa maelezo zaidi bonyeza viungo vifuatavyo upate  faida zaidi kuhusu hukmu za Zakaatul-Fitwr:

Fataawaa: Za Zakaatul-Fitwr

Fataawaa: Mukhtasari Wa Fataawaa Za Zakaatul-Fitwr

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share