Maelezo Kuhusu Hukmu Za Mirathi Kwa Ujumla

SWALI:

 

Assalaam Alaikum

 

Jazakum-llahu Kheir, Nimejifunza mengi kuhusu miirathi, naomba lau maelezo ya urithi kutajwa kwa ujumla kama ilivyo kuja kwenye Quran. Jawabu la miirath ya urith wa mama na mtoto wa kike na mamake bwana lilikua makhsus. Shukran, Wassalaam alaikum!

 


JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mirathi. Kawaida sisi huwa tunajibu swali kama tulivyoulizwa na muulizaji. Hilo swali ambalo umelitaja ni mfano wa maswali kuhusu urithi ambalo tumeulizwa na mmoja wa ndugu zetu. Ama maelezo ya kijumla kuhusu mirathi kama yafuatayo:

 

  1. Vigawanyo lazima vifuate hukumu zilizotolewa na Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam).
  2. Kabla ya kugawanywa kwa mirathi zitolewe pesa za maziko na madeni aliyonayo.
  3. Muislamu anaweza kuandika wasiya kwa mgao aliotoa lakini ukiwa utakwenda kinyume na Uislamu wasiya huo hautafuatwa.
  4. Haifai kwa mtu kumuandikia chochote mtu ambaye anarithi (yaani ana fungu lake maalumu kisheria).
  5. Wasiya alioandika aliyefariki kabla ya kufa kwake kwa wasiorithi usizidi thuluthi (1/3).
  6. Kuna wenye kupata fungu maalumu kama wazazi, mke na mume bila kujali waliobaki miongoni mwa warithi.
  7. Mgao wa mali ya aliyefariki unategemea waliobaki miongoni mwao ni wazazi, mke, mume, watoto, wajukuu, ndugu na kadhalika.

 

Soma Aayah katika Suratun Nisaa Namba : 7, 11, 12-13 176- zenye maelezo yote kuhusu Mirathi

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share