Akitajwa Allaah Tuseme Nini?

SWALI:

 ASSALAM ALEIKUM WARAHMTULLAHI WBARAKATU.

Niliuliza swli hili kwa watu wingi lakini wote hawajuwi. Swali lang ni mtu akisikia Mtume Mohammad (S.A.W) akitajwa watu wasema ALLAAHUMA SWALI WASALIM ALEI. Je Allaah (S.W.A) akitajwa mtu wafaa kusema nini?

 

 


 JIBU:

 Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Akitajwa Allaah utasema: “SUBHAANAHU WA TA‘ALA”, au “AZZA WA JALLA” au “JALLA JALAALUH” au “JALLA SHA-ANUHU” au “TA‘ALA” au kumtukuza Allaah kwa njia nyingine yoyote kama ilivyopokewa kwa Athari  zilizo sahihi.

Kama ambavyo Mtume akitajwa pia unaweza kusema: “SWALLA ALLAAHU ‘ALAYHI WA SALLAM” au “SWALLA ALLAAHU ‘ALAYHI WA ‘AALIHI WA SALLAM” au “ALAYHI SWALAATU WA SALAAM”, na kadhalika.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share