Saladi Ya Fattuwsh -1 (Lebanon)

Saladi Ya Fattuwsh -1 (Lebanon)

Vipimo

Majani ya saladi (lettuce) - ½ Msongo

Tango - 1 kubwa

Nyanya - 1

Parsley - ¼ Kikombe

Nanaa (mint) - Kiasi

Pilipili tamu la kijani - 1

Pilipili kubwa jekundu tamu - 1

Kitunguu cha majani kijani - 1 Msongo

Majani ya methi -½ Kikombe 

Mkate wa pita - 1

Salsali (salad dressing)

Ndimu - 2 Vijiko vya supu

Mafuta ya zaituuni - ¼ Kikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 chembe

Chumvi - Kiasi

Pilipili manga - ¼ Kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha

  1. Katakata majani ya saladi na vipimo vyote isipikuwa mkate wa pita.
  2. Choma mkate wa pita katika oveni ibadilike rangi ya browni, kisha vunja vipande vipande.
  3. Changanya vyote vizuri katika bakuli la kiasi.
  4. Kisha changanya vitu vyote vya salsali pamoja.
  5. Karibu na kula mwagia dressing uchanganye vizuri ikiwa tayari kuliwa

 

Majani ya Parsley

Share