Ibaadhi Hawaswali Nyuma Yetu; Je, Tuswali Nyuma Yao?

Ibaadhi Hawaswali Nyuma Yetu; Je, Tuswali Nyuma Yao?

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalam Alaikium Warahmatullah wabarakatu, Tunawashukuru ndugu zetu kwa kazi mnayoifanya kwa kutuelimisha Inshaallah ALLAH Atawalipa kwa lililokuwa bora zaidi yeye ndio mlipaji wa kila kitu, Suala langu lipo kwenye masuala ya madhehebu ya ibadhi nilisoma kuhusu ibadhi humu alhidaaya lakini kuna kitu amabacho nintaka kukielewa zaidi kwani mimi ni sunni na ninaswali nyuma ya ibadhi kwenye misikiti yao suala langu lipo hawa ibadhi wanatuthamini vipi sisi kwani utakuta kama kuswali tunaswalisha sisi wao hawatufuati wao huwa wanasimamisha swala yao mbali na sisi mimi baada ya kufuatilia nimepata jawabu ya kuwa wao wanadai kuwa sisi tumetoka kwenye rehma ya ALLAH sasa nilikuwa ninataka kujua haya ni kweli na kama ni kweli sisi tunatakiwa tuwafuate kwa kuswali nao au tufanye kama wanavyofanya wao kwetu sisi ninaomba jawabu kwa kirefu Sukran

 


 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.  

 

Asli katika mas-alah ni kuwa Swalah nyuma ya kila Muislamu inasihi na inajuzu hata kama huyo Imaam ni katika wenye kufanya baadhi ya maasi, na hii ndio kauli iliyo sahihi zaidi katika kauli za Maulamaa.  Hata hivyo Swalah nyuma ya aliyeshikamana na mafundisho ya Uislamu ni bora zaidi bila ya shaka yoyote ile.

 

Ama ikiwa Imaam ni katika wenye kufanya vijitendo vya ukafiri vyenye kumtoa mtu katika Uislamu basi Swalah nyuma ya Imaam kama huyo huwa haifai, kwani yeye mwenyewe huyo Imaam Swalah yake huwa si sahihi, kwani ametoka katika Uislamu na Swalah ya asiyekuwa Muislamu sio sahihi, na inapokuwa Swalah ya Imaam sio sahihi basi kumfuata Imaam huyo huwa hukufai.

 

Imaam At-Twahaawiy katika kitabu chake cha ‘Aqiydat Twahaawiyyah ameweka mlango wenye kusema: Tunaona Swalah nyuma ya kila mtenda wema na mtenda maovu miongoni mwa Ahlul Qiblah hata hivyo Hadiyth zenye kusema hivyo karibu zote ni dhaifu ila imethibiti kuwa baadhi ya Swahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) waliswali nyuma ya watu waovu kama Ibn Umar na Anas walikuwa wakiswali nyuma ya Hajjaaj bin Yusuf ambaye ni faasiq dhaalim.

 

Hata hivyo Imaam At-Twahaawiy amesema kuwa inajuzu kuswali nyuma ya asiyeeleweka uzushi wake -bid’ah zake- wala ufusqa wake, na si miongoni mwa shuruti za kumfuata Imaam kuelewa Maamuma itikadi ya Imaam anayemfuata au kumfanyia jaribio kwa kumuuliza maswali kuhusiana na itikadi yake; bali unatarajiwa kuswali nyuma ya Imaam huyo ambaye haeleweki hali yake.

 

Umesema hivi, ibadhi wanatuthamini vipi sisi kwani utakuta kama kuswali tunaswalisha sisi wao hawatufuati wao huwa wanasimamisha swala yao mbali na sisi

 

 

Swali kama hili liliulizwa kwa jopo la Wanachuoni wa kamati ya utafiti wa kielimu an utoaji Fatwa:

Swali: Je, Ibadhi ni kundi la Khaawarij linalohesabiwa kuwa ni potofu? Na je, inafaa kuswali nyuma yao?

Jibu: Ibaadhi ni kundi linalohesabika katika makundi potofu kwa sababu ya uhalifu wao na kumuasi Khalifah 'Uthmaan bin 'Iyfaan na 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu 'anhum), na haifai kuswali nyuma yao.

Na Allaah ni Mjuzi zaidi

Kamati ya Utafiti wa Kielimu na Utoaji Fatwa (mwisho wa kunukuu)

 

Unaweza vilevile kusoma makala hii muhimu Khawaarij

 

Umesema, wao wanadai kuwa sisi tumetoka kwenye rehma ya Allaah

 

 

Hayo kama ulivyosema ni madai yao, ama katika kanuni za Kiislam ni kuwa mwenye kuleta madai ya aina yoyote yale ni vyema alete dalili na ushahidi wa madai yake kama inavyotushauri Qur-aan kwa kusema:

“… Hayo ni matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli.” Al-Baqarah: 111.

 

Ikiwa makafiri na washirikina katika huu uhai wote hawakutoka kwenye rehema za Allaah vipi atatoka kwenye rehma za Allaah mwenye kusema: Laa ilahaa illa Allaah?  Aliyetoka kwenye rehma za Allaah kama inavyothibitisha Qur-aan ni Ibiliys, kwa kiburi chake cha kukataa amri ya Mola wake Mlezi, alimwambia: Basi toka kwenye kundi la watukufu walio juu, kwani wewe umekwishafukuzwa kutokana na rehema yangu! Qur-aan inasema:

 

“Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika.  Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo”. Swaad: 77-78.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share