Maharage Ya Nazi

Maharage Ya Nazi

  

Vipimo 

Maharage -  3 Vikombe 

Tui la nazi zito - 1½ kikombe 

Kitunguu - 1 kikubwa 

Nyanya -  1  

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu  

Pilipili mbichi -  3 

Chumvi -  Kiasi  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Roweka maharage, kasha chemsha maharage  hadi yawive haswa yalainike  
  2. Katakata kitunguu, nyanya,  na thomu kisha miminia katika maharage  
  3. Tia tui la nazi na subiri kidogo lichemkie humo  
  4. Weka chumvi kiasi na koroga iliuonje, kisha tupia pilipili mbichi na kisha funika kwa muda kadhaa hadi libaki rojo rojo  
  5. Baada ya hapo pakua na tayari kuliwa

  

 

 

Share