Hamtoweza Kuufikia Wema Uliokunjuka Mpaka Mtoe Katika Vile Mnavyovipenda!

 

Hamtoweza Kuufikia  Wema Uliokunjuka Mpaka Mtoe Katika Vile Mnavyovipenda!

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 لَنْ تَنَالُواْ الْبِرَّ حَتَّى تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللّهَ بِهِ عَلِيمٌ

Hamtoweza kuufikia wema uliokunjuka mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho ni Mjuzi. [Al-'Imraan: 92]

 

Katika kutoa sadaka anatakiwa Muumini atoe katika vile vilivyokuwa ni vizuri na bora kabisa hapo ndipo atakapokuwa kafikia wema mkunjufu kama inavyotaja kauli hiyo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

Kisha cha Abu Twalhah na bustani yake kipenzi Al-Bayruhaa:

 

 عن أنس بن مالك يقول: كان أبو طلحة أكثر أنصاري بالمدينة مالا وكانَ أحبَّ أمواله إليه بيْرَحاءُ  , وكانت مُسْتقْبلة المسجد، وكان النبي صلى الله عليه وسلم يدخلها ويشرب من ماء فيها طيّب , قال أنس: فلما نزلت: ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) قال أبو طلحة: يا رسول الله، إن الله يقول: ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) وإن أحبَّ أموالي إلَيَّ بيْرَحاءُ وإنها صدقة لله أرجو بِرَّها وذُخْرَها عند الله تعالى، فَضَعْها يا رسول الله حيث أراك الله [تعالى]  فقال النبي صلى الله عليه وسلم: ((بَخٍ، ذَاكَ مَالٌ رَابِحٌ، ذَاكَ مَالٌ رَابِح، وَقَدْ سَمِعْتُ، وَأَنَا أرَى أنْ تجْعَلَهَا فِي الأقْرَبِينَ)). فقال أبو طلحة: أفْعَلُ يا رسول الله. فَقَسَمها أبو طلحة في أقاربه وبني عمه (رواه  أحمد )

 

Imetoka kwa Anas bin Maalik Radhwiya Allaahu ‘anhu kwamba Abu Twalhah alikuwa na mali kuliko yeyote miongoni mwa Answaar wa Madiynah na kilichokuwa kipenzi kabisa katika mali yake ni bustani ya Bayruhaa ambayo ilikuwa mbele ya msikiti wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Mara nyingine Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akienda katika bustani hiyo na kunywa maji yake baridi. Anas akaongeza kusema: Aayah hii ilipoteremka:

 

لَنْ تَنَالُواْ الْبِرَّ حَتَّى تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللّهَ بِهِ عَلِيمٌ

Hamtoweza kuufikia wema uliokunjuka mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda

 

Abu Twalhah akasema "Ee Rasuli wa Allaah, Allaah Anasema, (Hamtafikia kabisa wema   mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda) bila ya shaka bustani ya Bayruhaa ni kipenzi katika mali zangu. Kwa hiyo nataka kuitoa sadaka kwa ajili ya Allaah nikitegemea thawabu zake na malimbikizo kutoka kwa Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa. Ee Rasuli wa Allaah, itumie popote Anapokuonyesha Allaah kuwa ni bora kuitumia". Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Umefanya vizuri, Ni mali yenye faida, ni mali yenye faida.  Nimesikia ulivyosema na nafikiri itakuwa ni bora kuwapa walio karibu yako (jamaa zako). Abu Twalhah akasema "Nitafanya hivyo ee Rasuli wa Allaah". Abu Twalha akagawa kwa jamaa zake na watoto wa ami yake”. [Al-Bukhaariy, Muslim, Ahmad]

 

Hawa ndio Swahaba walioamini kweli na kusabilia mali zao katika njia ya Allaah bila ya kujali lolote.  

 

Naye 'Umar bin Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu)alitoa mali yake iliyo kipenzi kabisa.

 

 عُمَر رضي الله عنه   قال :  " يا رسول الله، لم أُصِبْ مالا قطُّ هو أنْفَسُ   عندي من سهمي الذي هو بِخَيْبَرَ، فما تأمرني به؟"   قال : ((حَبِّس الأصْل وسَبِّل الثَّمَرَةَ))  مسلم والنسائي من إبن ماجاه

 

‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema: "Ee Rasuli wa Allaah, Sijapata kumiliki kipande cha mali kilicho cha thamani kwangu kama sehemu yangu ya Khaybar. Kwa hiyo unaniamuru niifanye nini?"  Nabiy (Swalla Allaahu ‘alyahi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ibakishe ardhi  na utoe mazao yake kwa ajili ya Allaah (Fiy Sabili-Llah)”.  [Muslim na An-Nasaaiy kutoka kwa Ibn Maajah]

 

Na kutoa sadaka ni kama mkopo wa kumkopesha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hili ni jambo kubwa, zuri, lenye kuzidisha iymani zetu na lenye kustaajabisha vilevile, kwa kuwa Mola wetu Mtukufu Ndiye Anayemjaalia mja Wake kumpa mali, kisha Yeye Anatuambia tumkopeshe hiyo mali na kuwa Atatulipa zaidi kuliko hiyo tutakayoitoa kwa ajili Yake! Na Juu ya yote, Atatupa malipo ya ukarimu! SubhaanaAllaah! Ukarimu ulioje wa Mola Mtukufu! Kama anavyosema:

 مَن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ

 Nani ambaye atamkopesha Allaah karadha nzuri kisha (Allaah)Amuongezee maradufu na apate ujira mtukufu. [Al-Hadiyd: 11]

 

Na tutambue kwamba chochote utoacho ndugu Muislamu ikiwa kikubwa au kidogo mno vipi basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Haghafilika nacho bali Atakulipa malipo yake duniani kama Anvyotuambia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَمَا تُنفِقُونَ إِلاَّ ابْتِغَاء وَجْهِ اللّهِ وَمَا تُنفِقُواْ مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لاَ تُظْلَمُونَ

Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika khayr mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa. [Al-Baqarah: 272]

 

Pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

 وَأَقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Na mkopesheni Allaah karadhi nzuri. Na chochote kile kheri mnachokadimisha kwa ajili ya nafsi zenu, mtakikuta kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Ni bora, na ujira mkubwa zaidi. [Al-Muzzammil: 20]

 

Share