Skip navigation.
Home kabah

Kizazi Kinapotea Kwa Maisha Ya Ulaya Na Marekani

'Abdun-Naaswir Hikmany

 

Shaykh Ibn Al-'Uthaymiyn anasema: "Hakuna ruhusa ya kuhama kuelekea nchi za Kikafiri isipokuwa kwa masharti matatu: Awe na elimu ya diyn itakayomzuia kupotoka, awe na msimamo wa diyn utakaomzuia kuhadaika na awe ni mwenye kulazimika kwa hilo analoendea."

 

Hakuna shaka yoyote kwamba, makundi mengi ya Waislamu yanayokimbilia Ulaya na Marekani hayajatimiza masharti hayo yaliyotajwa hapo juu.

 

Kinachotafutwa huko nacho kimegawika kwenye makundi matatu: rizki, elimu na maisha. Kwa bahati mbaya, pongezi hutolewa kwa yule aliyehamia Magharibi na kudharauliwa aliyeacha nafasi ya kwenda huko.

 

Waungwana wanasema: "Kawia ufike kuliko kulala njiani" haraka hizo za nini kuelekea Majuu hali ya kuwa baadhi yao wana maisha mazuri ndani ya nchi zao walizozaliwa? Basi iwapo Muislamu anashikilia msimamo wake wa kuparamia huko Majuu kwa hoja zisizo na maana, ni vyema tumkumbushe maneno ya Wahenga: "Mwenye pupa hadiriki kula tamu".

 

Kwa hakika athari mbaya nyingi tumezishuhudia kwa vijana wetu kuondoka mijini wakaenda huko Magharibi. Wapo mashababu ambao walikuja matembezini katika nchi zao za asili wakiwa wamevaa vidani na wasichana wamevaa nguo zilizochupa juu ya magoti na wengine hadi kuonyesha vitovu vyao. Hali sio hiyo tu, wale baadhi ya mashekhe na maustadhi wetu waliohamia huko, nao kwa masikitiko makubwa wameelemewa na dunia wakaigawa diyn yao bure!

 

Mzee naye kwa upande wake anamuhimiza mwanawe kwenda nchi za Kimagharibi, mara nyengine mzee anadiriki kumdhamini na kumpatia kila anachokihitajia kwa lengo la kumfikisha mwanawe Ulaya au Marekani. Uhuru anaopatiwa huko unamfanya awe kama mwehu wa kutimiza shahwa zake, kila kinachotendwa katika ardhi hizo za Magharibi anakiona ndio ustaarabu. Ndio sababu hata kina mama kushindwa kutembea na mabinti zao pale wanapozuru miji yao ya asili. Maana afadhali mama mtu atajiheshimu, lakini kwa binti zake, ni kinyago.

 

Uhamiaji wa nchi za Kimagharibi bila ya dharura nzito ni dhulma ya nafsi. Kwani Muislamu hatakuwa huru kutekeleza masharti ya diyn yake vile inavyotakiwa. Qur-aan inatupatia mjadala wa kuhama (hijrah) baina ya Malaika na watu wa motoni baada ya kutolewa roho zao:

 

{{Wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamedhulumu nafsi zao, (Malaika) watawaambia: "Mlikuwa katika hali gani (katika jambo la diyn yenu?)" Watasema: "Tulikuwa madhaifu katika ardhi hiyo (kwa hivyo hatukuweza kufanya ibada yetu)." (Malaika) watasema: "Ardhi ya Allaah haikuwa wasaa na nyinyi kuhamia humo?" Basi hao makazi yao ni Jahanamu; nayo ni marejeo mabaya kabisa.}} [An-Nisaa: 97]

 

Waislamu tufunuke macho na tuelekee kule kilipo Qiblah chetu, nacho kipo Makkah hakipo Marekani. Leo Waislamu wanakimbia jivu wanatumbukia kwenye moto. Akili zimeruka kwa Ulaya badala ya kufikiria kwenda Hijjah na kutenda ya maana.

 

Tukumbuke kwamba kila hatua na maamuzi tunayofanya tunatakiwa tuegemeze kwenye Uislamu wetu. Awali ya yote, ni Uislamu wetu. Hivyo, sio vyema kwa Muislamu kuacha mji wake ambao unampatia nafasi ya kumuabudu Mola wake kwa wasaa na akaelekea miji ambayo fitna imejaa na  utekelezaji wa ‘Ibaadah zake si kwa wepesi na wasaa.

 

 

 

Ni kweli baadhi ya maneno

Ni kweli baadhi ya maneno aliyosema Sheikh hapo juu. Kuna baadhi yetu tuliyohamia nchi za ulaya tumebadilika na tumekuwa worse. Lakini pia wapo tunaojitahidi kufuata maelekezo ya dini yetu na kuwalea watoto wetu kwa misingi ya dini yetu na hata kuanzisha vyuo na Madrassah kusomeshea watoto wetu masomo ya dini.

Jengine ni kuwa hizo nchi zinazojiita ni za Kiislamu kama Saudi Arabia, Oman n.k. hazikubali kupokea Waislamu wakaishi huko hata kama umepata mateso ya kidini nchini mwao. Mfano mzuri ni mimi mwenyewe nilikwenda Saudi Arabia mwaka 1989 kutokana na ukandamizaji wa kidini nchi kwetu na baada ya kuwaeleza matatizo yote niliyopata wakakataa kuniweka pale hata kwa muda mchache, walinipa wiki mbili tu niondoke nchini. Kwa hivyo tunawaomba Masheikh katika nchi zinazojiita kuwa ni za Kiislamu wazishinikize Serikali zao kuwasaidia Waislamu wanaotaka kuhamia katika nchi hizo. Naamini wako Waislamu wengi wengependa kwenda kuishi katika nchi hizi za "Kiislamu" lakini serikali zao haziko tayari kuwachukua.

Wibillah Tawfiq

NI KWELI KABISA NAMI PIA

NI KWELI KABISA NAMI PIA NINAUNGA MKONO MANENO HAYO HAPO. ILA PIA NA SISI WAISLAM TUMEZIDI KUIGA AU KUVUMBUA MAMBO NA HAYO MAMBO MENGINE YANATIA AIBU KWA WAISLAM WOTE, MFANO UTAONA MWANAMKE NAKWENDA KUSEMA YEYE HANA MUME NA KILA MWAKA AU MIAKA MIWILI ANAPATA MTOTO AKIULIZWA ANSEMA ETI AMEPATA MWANAMUME KWA USIKU MMOJA NDIO AMEMPA HIO MIMBA NA HAPO AKIENDA KUSEMA HAYO ATAKUA MWENYEKUVAA VAZI LA KIISLAM AMEJITANDA VIZURI MTANDIO WAKE ILI AZIDI KUUPAKA MATOPE UISLAM SI TU AVAE KIHUNIHUNI ILI AONEKANE HAWA NI WALE WALIO POTEA, HATA HAO WAZUNGU WENYEWE WANA TUSHANGAA UONANE NA MTU SIKU MOJA UMPE URODA BILA YA HATA HINGA, JAMANI TUMEZIDI HIVI KWELI HIZO NCHI ZA KIISLAM ZITAKUBALIANA NA HAYA,SIDHANI. NA MASHEHE WETU WA HAPA ULAYA KIMNYA KATIKA MAWAIDHA YAO WATASEMA TU MENGI LAKINI HILI BADO SIJA PATA KULISIKIA NA KAMA LIMESEMWA HALIKUENEA NINGEOMBA LIZUNGUMZIWE AU NDIO TUAMINI KWAMBA MAHEKHE WENYEWE NAO WAMO KATIKA MKUMBO HUO BASI LIZUNGUMZIENI TU HATA KAMA WAO YENYEWE HAWALIFATI HUENDA JAPO MMOJA WAWILI WAKALIFIKIRIA, KWANI LIKIACHWA BILA KUZUNGUMZIWA LINA ZIDI KULETA FITNA .

WABILLAHI TAWFIQ.