Vikate Vya Ufuta Vya Shimari

 

Vikate Vya Ufuta Vya Shimari 

Vipimo                                                          

Unga - 3 vikombe 

Mafuta - 1 kikombe cha kahawa 

Yai - 1

Sukari -  ¾ kikombe 

Chumvi -  ½ kijikco cha chai  

Bizari shimari (cammomile seeds) - 1 kijiko cha chai 

Ufuta (sesame seeds) - 1 kijiko cha chai 

Hamira - 1 kijiko cha chai 

Maji ya vuguvugu (warm) - 1 kikombe 

Vya Kupakazi (brush) 

Yai  lilopigwa  

Siagi/samli   

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Katika kibakuli kidogo changanya hamira na maji acha kwa muda ifure. 
  2. Weka  unga, mafuta, sukari, yai, bizari shimari, chumvi  katika bakuli kubwa, changanya vizuri, kisha changanya pamoja na  hamira iliyofura.
  3. Changanya tena vizuri kanda kidogo tu ulainike.   Funika kwa kitambaa au karatasi ya plastiki (Plastic wrap) . 
  4. Weka sehemu ya joto, au washa jiko (oven) muda mdogo tu, kisha zima liwe lina joto kiasi. Weka mchanganyiko wa unga ufure.

  1. Katakata vidonge vidogodogo, kisha  sukuma viduara vidogodogo bila ya kukandamiza. Tia unga juu na chini ya kibao cha kusukumia au sakafu ya kabati  ili yasigande au sivyo havitaumuka . 
  2. Epua, pakaza (brush) na yai lilopigwa kisha mwagia ufuta .  
  3. Panga katika treya, choma (bake ) katika oveni kidogo, kisha zima moto uache moto wa juu (grill) kidogo tu, vikate vigeuke rangi. 
  4. Epua pakaza (brush) kwa siagi au samli vikate vikiwa tayari.

 

 

 

Share