Kheer - Pudini Ya Mchele (Pakistani)

Vipimo
Mchele wa basmati ½ Kikombe
Siagi 1 Kijiko cha chai
Maziwa mazito (full cream milk) 4 Vikombe
Iliki ½ Kijiko cha chai
Sukari ½ Kikombe au zaidi
Zaafarani au vanilla Kidogo
Lozi na njugu (pistachios) zilizosagwa sio
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mchele na roweka kiasi ya nusu saa.
- Katika sufuria, tia siagi iache ipate moto, tia mchele na ukoroge.
- Kisha mimina maziwa na iwache ichemke pole pole kwa muda wa nusu saa hivi.
- Tia zaafarani (ukipenda), iliki na sukari.
- Iwache ichemke kwa muda wa dakika 10 zaidi.
- Halafu tia lozi na njugu, changanya vizuri kisha mimina kwenye vibakuli na iyache ipate baridi na tayari kuliwa.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
