Kukamua Chunusi Usoni Kunabatilisha Swawm?

 





SWALI:

 

 

Asalaam Aleykum Warahmatulah Wabarakatuhul,

 

Namshkuru Mwenyezi mungu mwingi wa rehema mwenye kutuwezesha kufunga na kufanya ibada kama alivyoamrisha.

 

Kwanza awali ya yote napenda kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kutuelemisha na kutupatia mambo mbalimbali yanayohusiana na dini yetu ya Kiislam. Mungu awazidishie kwani wengi tunajifunza mambo mengi kupitia mtandao wenu

 

Nina swali naomba mnijibu: Kama mtu umefunga halafu usoni ukawa na chunusi ambayo imeiva (yaani inausaha sana), Je ukiikamua utakuwa umefungulia au haibatilishi swaum?

 

Wabilah Tawfiq.

 

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

 

Shukurani kwa Swali lako. Kukamua chunusi usoni   hakubatilishi Swawm.   Hali kadhalika hukmu itakuwa sawa kuhusu kukamua vijipu n.k. Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo kuhusu mambo yanayobatilisha Swawm na yasiyobatilisha.

 

 

Mambo Muhimu Kuhusu Swawm

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share