Kila Kitu Kinamsujudia Allaah (سبحانه وتعالى) Je,Wewe Mwana Aadam?

 

Kila Kitu Kinamsujudia Allaah (سبحانه وتعالى), Je,Wewe Mwana Aadam?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah   (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّـهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ﴿٤٨﴾

Je, hawaoni vile vitu Alivyoumba Allaah ambavyo vivuli vyake vinasogea huku na kule, kuliani na kushotoni vikimsujudia Allaah na huku vinanyenyekea?  

 

 

وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ﴿٤٩﴾

Na ni kwa Allaah pekee vinasujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo, na Malaika, nao hawatakabari.

 

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩﴿٥٠﴾

Wanamkhofu Rabb wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa.   [An-Nahl: 48-50]

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hana mshirika wala msaidizi bali Yu Pekee Naye Ndiye Apasaye kuabudiwa. Viumbe vyote vinapasa kumsujudia Yeye, kama Anavyosema:

 

وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلَالُهُم بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ ۩﴿١٥﴾

Na kwa Allaah (Pekee) Humsujudia waliomo mbinguni na ardhini wakipenda wasipende na vivuli vyao pia (vinamsujudia) asubuhi na jioni.   [Ar-Ra'd: 15].

 

Na katika Hadiyth ifuatayo imethibiti kuwa jua linamsujudia Allaah (‘Azza wa Jalla):

 

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم لأَبِي ذَرٍّ حِينَ غَرَبَتِ الشَّمْسُ ‏"‏ تَدْرِي أَيْنَ تَذْهَبُ ‏"‏‏.‏ قُلْتُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَإِنَّهَا تَذْهَبُ حَتَّى تَسْجُدَ تَحْتَ الْعَرْشِ، فَتَسْتَأْذِنَ فَيُؤْذَنَ لَهَا، وَيُوشِكُ أَنْ تَسْجُدَ فَلاَ يُقْبَلَ مِنْهَا، وَتَسْتَأْذِنَ فَلاَ يُؤْذَنَ لَهَا، يُقَالُ لَهَا ارْجِعِي مِنْ حَيْثُ جِئْتِ‏.‏ فَتَطْلُعُ مِنْ مَغْرِبِهَا، فَذَلِكَ قَوْلُهُ تَعَالَى ‏  وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَهَا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ‏

 

Amesimulia Abuu Dharr (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniuliza wakati wa machweo: “Je, unajua jua linapokwenda (wakati wa kuzama kwake)?”  Nikamjibu: “Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi.” Akasema: “Hakika linakwenda mpaka linasujudu chini ya ‘Arsh, na kutaka idhini kuchomoza tena, nalo linaruhusiwa. Na inachelewa kuwa (itafika wakati ambapo) litakaribia kusujudu lakini sijda yake haitokubaliwa, na litaomba idhini lakini litakataliwa (kutimiza mizunguko yake). Litaambiwa: ‘Rudi ulipotoka’. Hivyo, litachomoza Magharibi. Na hiyo ndiyo Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٣٨﴾

“Na jua linatembea hadi matulio yake.[1] Hayo ni Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.” [Yaasiyn 36:38)- Hadiyth ameipokea Imaam Al-Bukhaariy]

 

 

Na pia:

 

عن ابن عباس قال: "جاء رجل فقال: يا رسول الله، إني رأيتني الليلة وأنا نائم، كأني أصلي خلف شجرة، فسجدتُ فسجَدَت الشجرة لسجودي، فسمعتُها وهي تقول:  اللّهُـمَّ اكْتُـبْ لي بِهـا عِنْـدَكَ أَجْـراً ، وَضَـعْ عَنِّـي بِهـا وِزْراً ، وَاجْعَـلها لي عِنْـدَكَ ذُخْـراً ، وَتَقَبَّـلها مِنِّـي كَمـا تَقَبَّلْتَـها مِنْ عَبْـدِكَ داود)). قال ابن عباس: فقرأ  النبي صلى الله عليه وسلم سجدة ثم سَجَد، فسمعته وهو يقولُ مثلَ ما أخبره الرجل عن قول الشجرةرواه الترمذي، وابن ماجه، وابن حبّان في صحيحه

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa)  amesema: "Mtu moja alikuja na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah, nilijiona katika ndoto jana usiku nikiswali nyuma ya mti. Niliposujudu na mti ukawa unasujudu. Kisha nikausikia unasema: ((Ee Allaah,  Niandikie Kwako kwa sijda hii malipo, na Nifutie kwayo madhambi, na Ijaalie kwangu mbele yako ni akiba, na Nikubalie kama ulivyomkubalia mja wako Daawuwd)) Ibn 'Abbaas akasema: "Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   akasoma Aayah inayotaja kusujudu kisha akasujudu na nikamsikia akisema maneno hayo hayo aliyosimulia mtu yaliyotajwa na mti."  [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake, na ameisahihisha Imaam Al-Albaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3424), Swahiyh At-Targhiyb (1441)].

 

Na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ah   Anasema:

 

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ ۖ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَابُ ۗ وَمَن يُهِنِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن مُّكْرِمٍ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ۩﴿١٨﴾

Je, huoni kwamba wanamsujudia Allaah walioko mbinguni na ardhini, na jua, na mwezi na nyota, na majabali na miti na viumbe vinavyotembea, na wengi miongoni mwa watu? Na wengi imewastahiki adhabu. Na ambaye Allaah Amemdhalilisha, basi hatopata wa kumkirimu. Hakika Allaah Anafanya Atakavyo.   [Al-Hajj: 18].

 

 

Aayah hiyo mwisho inasema kuwa ((Na wengi imewastahiki adhabu)) kwa maana kwamba wale ambao hawataki kusujudu. [Ibn Kathiyr 6:540].

 

Basi ndugu Muislamu tunatumai kuwa hutokuwa miongoni mwa wanaostahiki adhabu. Hivyo timiza Swalaah zako tano za fardhi zipasavyo kuswaliwa kwa kuzidumisha na kuziswali kwa wakati wake. Kisha utakapokuwa umezidumisha Swalaah zako tano basi jiongozee kuswali Swalaah za Sunnah uzidi kumnyenyekea Rabb wako na kupata fadhila nyingi za kusujudu na za kuswali Swalaah za Sunnah. Na pia kila unaposoma Aayah iliyo na Sajdah, pinduka umsujudie Allaah ('Azza wa Jalla).

 

 

 

Share