Amewaandikia Nyumba Watoto Wa Mke Wa Mwisho, Watoto Wa Mke Wa Mwanzo, Wanadai Mirathi Baada Ya Miaka 12
SWALI:
A'aleykum. Mzee alikua na wake watatu. Mzee aliwaandikia nyumba watoto wa mke mwisho kwa sababu hawa watoto walikua wadogo na yeye mzee
Tunaomba ushauri nini kifanyike ili amani ipatikane?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Mirathi ya watoto kutoka kwa baba
Hakika ni makosa kwa mzazi kuacha wasiya nani arithi nini wakati anaaga dunia au kabla ya hapo. Mirathi kawaida kishari’ah haandikiwi chochote bali anapata kile kilichopangwa na Allaah Aliyetukuka. Wasiya mtu anaweza kumuandikia asiyerithi na haifai kuzidi thuluthi moja.
Ama katika kadhiya hii, inatakiwa
1. Mke au wake atapata au watapata thumuni (1/8). Ikiwa aliyebaki hai ni mmoja atapata thumuni na ikiwa wapo wote watatu watagawa hiyo thumuni.
2. Watoto watapata kilichobaki, mtoto wa kiume akipata sehemu mbili ilhali msichana akipata moja. Sasa inategemea aliacha watoto wangapi.
Inatakiwa kwa sasa waliobaki wafanye haki kwa kuigawa inavyotakiwa na Uislamu. Na wenye kufanya uadilifu huo watapata thawabu nyingi kutoka kwa Mola wao Mlezi. Ikiwa baadhi ya wake wameaga dunia au watoto wengine wamefariki, sehemu zao watagawiwa warithi wao.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
