Anajaribu Kufanya Mema Lakini Ana Tabia Chafu Ya Kuondosha Matamanio Kwa Mkono Na Vifaa, Afanyeje Kujiepusha Shaytwaan ?
SWALI:
Assalam alaikum
Naomba munisaidie kuhusu suala hili. Mr X anapata taabu
NAOMBA TUMSAIDIE MR X>
SHUKRAN>
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ndugu anayejaribu kufanya mema lakini kuzidiwa na uchu wa nafsi yake dhaifu.
Hakika ni kuwa mwanaadamu ana maumbile ya kutamani na kufanya maovu. Maovu yanavutia na yanazidi kujikita katika maisha ya mwanaadamu kwa njia moja au nyingine. Baadhi yake ni kutokana na mtu kuwa mbali na Allaah Aliyetukuka kwa matendo na maneno, kutojiweka katika kufuata Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kufuata matamanio, upungufu wa Imani, kuwa na marafiki wabaya, kutoishi na Qur-aan, kuwa na wakati mwingi wa faragha, kutokumbuka mauti na mengineyo.
Kwa kuwa nafsi inaamrisha mabaya inabidi Muislamu ajitahidi kujitoa katika nafsi mbaya, kuifikia nafsi yenye kujilaumu na hatimaye kupanda na kufika katika nafsi iliyotulia. Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Nami sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni mno kuamrisha maovu, isipokuwa ile ambayo Mola wangu Aliyoirehemu. Hakika Mola wangu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu” (Yuusuf [12]: 53).
Hata hivyo kulingana na maelezo juu ya kumhusu huyo ndugu, inaonekana kuwa yupo baina ya nafsi inaoamrisha maovu na ile yenye kujilaumu. Na kwa ajili hiyo ni lazima ajinasue kutoka katika hali hiyo ambayo si nzuri na itamfikisha mahali ambapo ni pabaya.
Kulingana na maelezo inaonyesha kuwa ameshindwa kujizatiti na kujiondoa katika mabaya mbali ya kuwa yeye anaamrisha mema. Na lau atakuwa ni mwenye kuzingatia Aayah zifuatazo basi huenda zikamtoa kwa aliyonayo.
Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda? Ni chukizo kubwa mno kwa Allaah kuwa mnasema msiyoyatenda” (Asw-Swaff [61]: 2 – 3).
Na pia kutazama Hadiyth zinazozungumzia adhabu anayopata mwenye kuamrisha mema naye akawa anafanya mabaya. Tukumbuke Hadiyth ya Usaamah bin Zayd bin al-Haarith (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
“Ataletwa mtu Siku ya Qiyaamah, naye ataingizwa Motoni. Matumbo yake yatatoka nje, naye atayashikilia akiwa anazunguka
Huyo ndugu anahitaji ushauri nasaha kwa yale anayokumbana nayo. Inatakikana akalishwe chini na kuzungumziwa kwa anayoyafanya na jinsi ya kujitoa, kwani akitopigana na nafsi yake itampeleka mahali pabaya. Kwa kutazama yanayomfika, twaona lau atafanya yafuatayo, basi ataweza kujiondoa katika madhambi hayo:
1. Inaonyesha ana wakati wa faragha mwingi
2. Kwa mtu mwenye matamanio
3. Inabidi ajizoezeshe kufunga kwani kufunga kunaondoa hayo matamanio ya ziada ya mwanamme. Awe na ada ya kufunga Jumatatu na Alkhamiys.
4. Kuwa na marafiki wema na wazuri ambao watakuwa kioo kwake na kumnasihi katika hayo mambo na mengineyo.
5. Kuisoma Qur-aan kwa kuielewa na kujaribu kuitia kimatendo maishani mwake.
6. Kukumbuka mauti na kuwa siku moja atasimamishwa mbele ya Allaah Aliyetukuka na hakutakuwa na mkalimani baina yake na Mola Wake.
7. Kutaamali zile adhabu ambazo anatarajiwa kuzipata kwa kufanya kinyume na anayoamrisha. Hasa aitaamali hiyo Hadiyth tuliyoitaja hapo juu.
8. Awe kila wakati anaomba kinga kutoka kwa Allaah Aliyetukuka hasa anapopata zile pepesi za Shaytwaan na wasiwasi wake.
9. Awe anasoma zile Adhkaar za asubuhi na jioni na kumuomba kwa dhati Allaah Aliyetukuka kumuondoshea hayo.
10. Afanye juhudi kubwa kujirekebisha, kwani Allaah Aliyetukuka Humsaidia anayejisaidia. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Hakika Allaah Habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao” (Ar-Ra‘d [13]: 11).
Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:
Nini Hukumu Ya Kujichua Sehemu Za Siri Au Kujisaga?.
Kutumia Kitu Kujitoa Matamanio Nini Hukmu Yake
Na tunatarajia kwa tawfiki ya Allaah Aliyetukuka atakuwa ni mwenye kutengea katika yaliyo bora na ya kheri zaidi.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
