032-Kutoa Zakaah: Kuinunua Zakaah
Kuinunua Zakaah
Nabiy (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amekataza mtu kuinunua Zakaah yake. Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Llaahu ‘anhu), amesema:
"‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alimtoa farasi wake Swadaqah fiy sabiyli Llaah, kisha akamkuta farasi huyo anauzwa na akataka kumnunua. Akamuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya jambo hilo, akamwambia:
"Usimnunue na wala usirudie (kutaka kuimiliki tena) Swadaqah yako" [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
Baadhi ya maulamaa wakasema kuwa kukataza huko ni kwa ajili ya kujiepusha tu, na si kwa ajili ya kuharamisha, wakiegemea Hadiyth nyingine inayoruhusu mtu kuipokea Swadaqah yake kama zawadi itokayo kwa masikini aliyempa.