Umri Gani Mtu Anaweza Kutoa Mawaidha?

SWALI:

 

asallam allaikum

            

je, ni umri upi  mtu afa kutoa mawaitha ama kuna masharti yoyote  ki sheria

   


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu umri wa mtu kutoa mawaidha.

Uislamu haujaweka umri maalumu wa mtu kutoa mawaidha isipokuwa masharti yanayohitajika kuwepo. Yakiwepo masharti hayo mtu ataweza kutoa mawaidha na yakikosekana hata mtu awe mkubwa namna gani hatofaa kutoa mawaidha. Masharti ni kama yafuatayo:

 

1.     Awe Muislamu.

2.     Awe mwenye akili timamu, yaani asiwe mwendawazimu.

3.     Awe anaweza kutofautisha mambo.

4.     Awe ana elimu ya hayo anayozungumza.

 

Kwa minajili hiyo, Imaam ash-Shaafi‘iy alipokuwa na miaka kumi na nne (14), Imaam Maalik alimpatia fursa ya kutoa mawaidha ndani ya Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Madiynah. Na Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) naye alikuwa akiingia katika Shuuraa ya ‘Umar bin al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) akiwa ni kijana hata wakongwe miongoni mwa Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) walioshiriki katika Vita vya Badr wakaanza kulalamika.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share