Maulidi: Anataka Tarjama Ya Maulidi Barzanji Ili Ajue Nini Hasa Kimeandikwa Ndani Yake
Maulidi: Anataka Tarjama Ya Maulidi Barzanji
Ili Ajue Nini Hasa Kimeandikwa Ndani Yake
SWALI:
Assalam laykum
tumekua tukisma mara nyingi makala zinazokataza mawlid na zinazo kubali mawlid na kuzusha mijadala mingi sehemu mbalimbali na wengi wa wanaotoa mada hizi huwa na hoja zao japo nyengine si za msingi, kwa hiyo ombi langu kwenu naomba mtutilie tafsiri ya kiswahili ya mawlid al barzanji ili tupate nafasi ya kujua nini hassa kimeandikwa ndani ya kitabu hichi. Natanguliza shukran.
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Hakika inatosha kwa Muislamu kujua kuwa Mawlid ni jambo la uzushi na lisilomsaidia Muislamu katika Dini yake wala kumpatia Jannah (Pepo) yake.
Ikiwa ni hivyo basi, hakuna maana yoyote wala haja ya Muislamu kutaka kujua Tarjama ya hivyo vijitabu vinavyotumika kusomea Mawlid.
Hata hivyo yafuatayo ni baadhi ya ambayo yamezushwa na kumtukuza mno kuvuka mipaka katika kitabu hicho cha Barzanjiy:
“Katika saa ya kuzaliwa Mtume alihudhuria Aasiyah na Maryam kutoka Mbinguni.”
“Wanyama walitamka kwa Kiarabu kuwa leo imechukuliwa mimba ya Mtume.”
“Wanyama wakapeana khabari ya kuchukuliwa mimba ya Mtume.”
“Majini wakatoa khabari kwa watu kuwa imechukuliwa mimba ya Mtume.”
“Katika saa ya kuzaliwa Mtume alihudhuria Aasiyah na Maryam kutoka Mbinguni.”
“Wanavyuoni wameona ni jambo zuri watu kusimama wakati inapotajwa kuzaliwa Mtume.”
“Akamwona Allaah kwa macho yake.”
Pia soma upate faida katika viungo vifuatavyo:
Na Allaah Anajua zaidi