Kuwekeza Pesa Kwenye Hisa Ambayo Mkataba Wake Unasema Faida Unayopata Ni Ribaa

SWALI:

 

Asalam alaykum.

Kuna biashara nimejiunga nayo but kwa sasa napatwa na wasiwasi then naomba nipate uhakika kama nifanyalo ni sahihi au la.. Kuna mama anafanya biashara mwenyewe anasema anahisa kwenye makampuni mbalimbali. Anawekeza pesa huko then kila mwezi anapate share yake. Unakuwa unampa kiasi fulani cha fedha anapeleka huko kwa mfano wampa laki1 hapo kila mwezi utapata faida ya elfu ishirini kwa miezi mtakayokubaliana na mwezi wa mwisho mlokubaliana ukifika anakurudishia zile pesa zako ulizotoa mwanzoni na faida kwa mwezi huo. Kwa mfano ulotoa laki mmekubaliana miezi mitano kila mwezi utachukua elfuishirini na mwishoni ule mwezi wa tano ukifika anakupa laki na ishirini then umepata faida ya laki. Akiuulizwa anasema yeye ana hisa kwenye kampuni tofauti ila hakunambia kampuni na ndipo huko anapotoa hizo faida. But kwenye makataba wake anaandika kwamba unamkopesha pesa na atakulipa kwa interest. Akiulizwa anasema hivyo anakwepa ushuru na mambo mengine. Je biashara hii inaruhusiwa kwa misingi ya dini ya kiislam? Kabla kujiunga niliuliza baadhi ya watu wakasema inafaa ila hapo ilikuwa kabla sijaona mkataba, nilipoona mkataba nikawa na wasiwasi, Natumai nitajibiwa kabla sijachelewa maana kama haifai nijitoe mapema. Shukrani. stay gud n b blecd! bbe!!!

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza tunapenda kukumbusha tu kuwa unapouliza maswali, tafadhali usitumie lugha ya kufupisha kwani huenda isieleweka kwetu  unalokusudia kuandika na vyema zaidi kutumia maagano ya Kiislamu kama kusema Assalamu ‘alaykum au  Fiy-AmaniLlaah (bakia  katika amani  ya Allaah).

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kuwekeza pesa kwenye hisa.

Hakika sote tunafahamu kuwa hakuna biashara ambayo una dhamana ya kupata faida kila wakati bali kuna wakati utapata faida na mwengine upate hasara. Hisa takriban zote zinazotolewa na makampuni yote ni ile ya kukudhamini kuwa kila mwaka au mwezi utapata kiwango fulani cha Ribaa (interest). Ribaa ni haramu katika Dini yetu ya Kiislamu.

 

Kwa minajili hiyo kuwekeza pesa kupitia kwa mwanamke huyo ni Ribaa na ni haramu kwako kuwekeza hapo. Lau kutakuwa na kampuni yenye kuuza hisa kwa misingi kuwa mwanzo biashara yao ni ya halali na unaweza kupata hasara kampuni ikipata hasara wakati huo utakubaliwa kuwekeza venginevyo hairuhusiwi.

 

Na Allaah Aliyetukuka Anajua zaidi

 

Share