Hilaal: Utata Wa Swawm Na Kufungua Kutokana Tofauti Ya Mwandamo Wa Mwezi

 

 

Hilaal: (Mwandamo Wa Mwezi)

 

Utata Wa Swawm Na Kufungua Kutokana Tofauti Ya Mwandamo Wa Mwezi

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Assalama alaykum

Naomba kuuliza tena swali langu niko uturuki nanchi hii wanafuata kalenda na sie ijumaa tumefunga kuja kufunguwa alhidaya nikaona tangazo ndio nikaamuwa kuuliza hili swala je hiyo ijumaa itakuwa tumefunga bure? Na wakila iddy mie nitata kiwa kufunga? Au vipi niondoweni ktk utata huu.

 

 

JIBU: 

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaa zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hakika suala la mwandamo halina utata lakini sisi Waislamu ndio tunalitilia utata usiokuwepo.

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuelekeza: “Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi ..” [Al-Bukhaariy].

 

Hivyo, hakutuachia fursa ya kufanya mahesabu yetu bali tunatakiwa tufanye juhudi kuutazama na kuuona kwa macho au kufuatilizia maeneo ambayo ndugu zetu wameuona. 

 

Jambo unalotakiwa kufanya ni kuwa mwaka huu ushapita kwani umefanya makosa kwa kutojua. Kuanzia sasa unatakiwa uwe unafuatilia mwezi kutoka katika zile nchi ambazo zinatazama, hivyo wakifunga nawe unafunga na wakifungua nawe utafungua hata ukiwa peke yako. 

 

Zaidi soma katika viungo vifuatavyo:

 

Hilaal: Kila Mji Ufuate Mwezi Unapoonekena Kwao Au Mwandamo Wa Kimataifa?

 

Hilaal: Waislamu Wote Duniani Wafunge Siku Moja Na Kula ‘Iyd Siku Moja ?

 

Hilaal: Mwezi Ulionekana Siku Moja Nchi Nyingine Mapema Zaidi Yetu Je, Tulipe Siku Hiyo?

 

Hilaal:  Afuate Mwandamo Wa Mwezi Nchi Anayoishi Au Unapoandama Nchi Yoyote?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share