Kusoma Aayah Fulani Au Surah Mara Kadhaa

SWALI:

 

A.W.W.KATIKA IBADA ZETU TUNAAMBIWA SOMA AYA HIYI MARA KADHA ALLAH ATAKUZAWADIYA HIKI. JE HIYO NI SHIRKI?


 

JIBU:

 

AlhamduliLlaah - Himdi Na Sifa Zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kusoma baadhi ya Aayah mara kadhaa.

Tunatakiwa tufahamu kuwa ikiwa kusoma huko mara hizo kumetokana na Hadiyth zilizo Swahiyh utakuwa ni mwenye kupata thawabu na kupata hicho ulichoambiwa.

 

Ikiwa kusoma huko ni katika Itikadi zetu, au maneno ya kutungwa kwa kuzuliwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) utakosa thawabu na kukuingiza katika madhambi. Hivyo, ni muhimu kutazama usahihi wa visomo hivyo kabla ya kuvishika na kuvifuata.

Lazima kutahadhari na mas-ala ya uzushi kwani yamezidi mno kutokana na wepesi wa mawasiliano. Hivyo ni wajibu wa Muislamu kuhakikisha kwanza habari inayomfikia kuhusu ibada zake kabla ya kuzifanyia kazi au kuzisambaza.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Hatari Ya Kueneza Hadiyth Dhaifu Na Visa Vya Uongo

Suratul-An'aam Isomwe Siku 40 Kuondosha Mitihani Ya Dunia?

Kusoma Majina Ya Allaah Kwa Idadi Maalum

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share